Kiukweli haya ni mambo ambayo hatuwezi yaweka hadharani maana ni kufru lakini kwa hapa jamiiforums hakuna anaemjua mwenzake kuna privacy hivyo uhuru wa kutiririka siro zetu upo.
Mimi niliwahi kuwa na feelings na mtoto wa mamamdogo wangu ambae niliishi nae miezi miwili akiwa likizo ya form 6 anasubiri kwend chuo, mwanzoni nilikuwa napingana sana na hizo feelings zisinitawale akilini lakini ilikuwa ni ngumu sana kuzuzuia.
Nilianza kumpenda sana, tulikuwa tumezoeana sana kama ndugu tu lakini shida ikawa inakuja kwenye uzito wa kumpa live mbele yake kwamba nimemzimia, tuliwahi kucheza sana utotoni kwahio tulikuja kutana tena ukubwani.
Nilianza hadi kumuwaza mara kwa mara na kum fantacize kimapenzi, moyo wa kutaka kumfungukia ukawa unanipa msukumo mkubwa sana nimwambie ukweli nami nikaanza kujiamini kwamba hakuna linaloshindikana, kilichopo moyoni kinanitesa kwanini nikishikilie sana, mda huo yani sijali cha tamaduni wala undugu nipo full mkoko kutaka kumwambia ukweli. ila kiukweli kila nikitaka kumwambia moyo unasita.
Tulikuwa na michezo ya kugombania rimoti, kugombaniana siti, n.k nilianza kuianzisha maksudi ili niwe naitumia kumgusa gusa na kumkumbatia.
Siku ilifika akaondoka kwenda kuanza chuo ndio tukawa mbali na ndio ikawa ponea yangu
Nashukuru nilichotaka hakikufanikiwa, kingekua ni doa kubwa sana huku maisha ya ukubwani