CONFIRMED: Manara alikuwa anaihujumu Simba SC

CONFIRMED: Manara alikuwa anaihujumu Simba SC

Leo kwenye kipindi cha sports HQ kinachorushwa na E-fm aliyewahi kuwa msemaji wa club ya simba 'simba sports club' Ndg. Haji Manara ameweka bayana kuwa hajawahi kuipenda club hiyo na hajawahi kuwa miongoni mwao. Kwa kinywa chake haji manara amesema "sijawahi kuwa simba"

Itakumbukwa kuwa ni wiki chache zimepita tangu msemaji huyo aaminishe mashabiki wa simba na watanzania kuwa aliipenda club hiyo kutoka moyoni na kuwa alijitolea kwa nguvu zake zote kwa jasho na damu kuipigania kufa na kupona hadi kufikia hapo ilipofikia.

Lakini kwa kauli yake aliyoitoa leo naungana na wana soccer wengine kuamini pasina shaka kwamba huyu bwana alikuwa yupo simba kwa kazi maalum ya kuhijumu na baada ya kushitukiwa na kutimuliwa ameamua kujitangaza hadaharani kwa kinywa chake mwenyewe.

Kufuatia kauli yake hiyo, mimi kama mdau wa soccer na mkereketwa wa dar es salaam young africans 'yanga' naishauri kuwa makini na huyu mtu kwa sababu 'what goes around is what comes around'. Kama mtu huyu huyu alitumiwa na wao kututukana na kutukejeli leo amewageuka wale wale waliomtuma na kumlipa kututukana basi ipo siku hata sisi atarudi tena kutugeuka na kututukana vile vile na hapo ndipo msemo wa "what goes around is what comes around" unapodhihirika. Tuwe makini na huyu walking bomb he can erupt anytime.
Siku akienda Azam atasema hivyohivyo
 
Hajji Manara ni shabiki wa hela tu! Hata huku Yanga amekuja tu kutafuta hela. Hivyo tunatakiwa kuishi naye kwa akili. Maana ipo siku atatugeuka!
Kwa akili zake mbovu najua ipo siku atanyea kambi na kuhamia timu nyingine na akifika huko atatusema kama alivyokuwa akitusema akiwa simba. Ngoja tuendelee kumchekea lakini ipo siku kiama kitatugeukia tena. Time will tell
 
Anawandoa Mashabiki wa YANGA kwenye issue ya wachezaji walio pegwa Ban na CAF wasicheze Jumapili. .....kwahiyo kaanzisha kituko ile ndio kiwe issue cha kuzungumzwa. Kweli WABONGO ukiwajua huwawezi kukusumbua hata kidogo.
 
Huyo njaa ndio imemfikisha hapo halafu amenogewa na umaarufu hivyo atafanya kila kitu ambacho mwenyewe anaamini vitafanya aendelee kuwa maarufu zaidi lakini kumbe ndio anajiharibia na hata kuweka rehani maisha yake,walio karibu naye wamshauri madhara ya baadhi ya kauli zake.
 
KAMA UTOPOLO WANA AKILI WAJUE KABISA KWA MANENO HAYA HATA WAO MANARA HAWAAMINI YUPO PALE KWA AJILI YA KIPATO NA SIO MAPENZI NA TEAM MAANA HARTA AKIENDA AZAM ATAKANA SIMBA NA YANGA NA KUSIFIA AZAM.
 
Aisee huyu jamaa anapitia wakati mgumu sanaa
Wakati mgumu ni kwa nyie, lakini yeeye account yake inasoma ana wakati mgumu upi?mbona ktk maisha ni mambo ya kawaida tu, ni wanasiasa wangapi walitukana sana walipokuwa leo wako wapi?sembuse taaluma?
 
Leo nimegundua kuwa Haji ni aina ile ya watu wabishi, wasiokubali kushindwa.

Ukimuwekea fedha mezani, atakuwa tayari kufanya chochote ili mradi azipate.

Watu wa Simba naona kama vile ndio mtanufaika sana kupata mambo ya ndani ya Yanga.
 
Siku akienda Azam atasema hivyohivyo
Ndio maana nimeshauri club yetu ya yanga iwe makini na huyu mtu. Wasimwamini sana na kuanza kumshirikisha kwenye vikao vya ndani vya klabu kwa sababu kwa hulka yake siku akitoka yanga ataropoka tu maana ndio asili yake na asili ni kama ngozi huwa haibadiliki
 
Tulieni hivyo hivyo dawa iendelee kuwaingia vizuri nyie makolo na msisahau kunywa maji mengi
 
Back
Top Bottom