"Tutaelewana tu." Dr. Shika.
Vyombo vya ulinzi na usalama hazihusiki na mambo ya kisiasa, kitendo cha kuamini au kulazimisha vikosi vya ulinzi na usalama kushiriki kwenye siasa za nchi yetu itakuwa ni jambo la hatari sana kwa hatma ya siasa za Tanzania za leo, kesho na keshokutwa.
Mpaka sasa inaaminiwa na watu wengi mtandaoni kuwa ni nguvu ya JWTZ ndio iliyopelekea tangazo la kifo cha Magufuli kutolewa kwa umma na ndani ya masaa 48 mama Samia Suluhu kuapishwa kuwa rais wa Tanzania. Kama jambo hilo litakuwa na chembe chembe zozote za ukweli, basi tujue moja tu, nchi yetu haiko salama na Magufuli atakuwa ametuachia urithi mbaya na mbovu kupindukia.
Wasipo maliza tofauti zao ndani kwa ndani, tutegemea majaribio kadhaa ya mapinduzi ndani ya kipindi cha miezi sita mpaka mwaka. Sitaki kabisa kuamini hili, na Mungu aepushilie mbali.