Connect Dot: Nani anataka kumtisha Rais Samia na umaarufu wa Hayati Magufuli?

Connect Dot: Nani anataka kumtisha Rais Samia na umaarufu wa Hayati Magufuli?

Ukiangalia kwa jicho la 3, ni kama wanampotezea, tumalize mazishi tuondoke Chato, turudi mjini tuone je, media zitakuwa na habari gani??

Habari kuu itakuwa uchawi na mvuragano ndani ya chama wa kutafuta makamu na nani apewe kijiti cha uenyekiti. Kuna nafasi za Katibu Mkuu na Mwenezi. Mara chanjo za changamoto ya upumuaji. Chato itakuwa bye!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Wajinga sisi tunajiingiza kwenye makundi na ushabiki tusiojua nyuma ya pazia wanapanga nini kwaajili ya Taifa hili. Kuna Cartels now zinapigana kushika mpini .... miongoni mwao ni wazalendo ambao ukitoa uzalendo wao lakini pia wanajilinda na Cartels ambazo waliziumiza kipindi wakipoka wezi mali zilizoibiwa.

Tuombee vyombo vyetu vya ulinzi na usalama wazalendo waliomo wapitishe salama Taifa kwenye hili, not by compromising ila ustawi wa Tanzania.
una akili sana wewe kama unaweza kufikiria haya wakati huu vijana wameshikiwa akili na kigogo wa twitter.
 
W
Nchi yetu haiishiwi mambo na mengi ni yakutengeneza, jaribu kukonnect dots kwa mambo yafuatayo;

1. Ni Wiki ya pili sasa lakini hakuna chombo cha habari chochote kinachotaka tumjue vizur Rais Samia, na si kwa bahati mbaya, baada tu ya kuapa malori ya kujaza watu kwenda msibani yaliongezeka na coverage zikaongezeka sana, yani hadi waombolezaji waliozimia huku mikono ikiwa imeshikilia viroba vya vitoweo.
2. Kwamba msiba unafuatiliwa na watu karibu bilioni 4, sio kauli ya bahati mbaya, message ni kwamba huyu mtu ni mashuhuri sana na italazimika uenzi metendo yake(Offcorse nawateule wake) la sivyo wananchi wanyonge na dunia haitakuelewa.
3. Nyani wanafurahi kufa kwa Bwana shamba bila kujua kesho watakula wapi; hoja hapa wala sio wapinzani, ni kundi lisilofaidika na cheo kipindi Mzee akiwa hai, ndio limepigwa dongo, kwamba hata kama mnafurahi lakini hata hicho kidogo mlikipata kwa ubavu wake.
4. Waraka mrefu wa mema ya JK(Unaozunguka mitandaoni), unaonesha kwamba tunataka kuanza upya, kujenga nchi kwa usawa, ila pia unajibu vitisho vya team iliyokuwa inasifia mambo bila takwimu lakini pia kujibu mapigo kwamba nani atasaidia kujenga miradi mingine
5. Mimi ni Raisi lakini mwenye maumbile ya mwanamke, ni kujibu vitisho kwa ujumla wake, lakini pia kuonesha kwamba akiamua anaweza kufanya hata kuzidi mtangulizi wake.

Turudi kwenye makundi ya CCM;

Kundi lililofaidi lakini lenye wasiwasi
Wamo kina Kabudi, Pole pole, Bashiru, Majaliwa na team tano tena 2020; hasa walioshinda bila kupingwa na kura za kwenye mabegi kama kule Kawe... hali yao ni ngumu kuliko maelezo.
Pia wamo waliomnanga JK vibaya mno akiwemo Madelu.

Kundi la waliotengwa licha ya uwezo wao na utendaji wao;
Wamo kina Muhongo, Januar, Nape na Kina Kimei.

Kundi la kuunga Juhudi mkono ;

Kina Covid 19, Katambi, Waitara , Silinde, Mollel na wengine, hawa hawajui nini mustakabali mama akitulia kwenye madaraka hivyo dawa ni kujiunga na kundi la kina Majaliwa.

Swali la msingi hapa; nani anataka kumtisha Rais Samia, au wanatumia umaarufu wa Hayati kutaka kumtisha asifanye lolote mambo yaende business as usual?
Waunga juhudi hali yao mbaya Sana.Na za chini ya kapeti ktk kikao cha kwanza cha kamati kuu ya CCM mama aliambiwa hilo. Kwamba walioipigania na wanaoipigania CCM wanatupwa halafu watu kuja wanapewa vyeo wao wanabaki.

Je,kauli ya Mwita Waitara kusema alihamia CCM kwasababu aliridhika na utendaji wa CCM Ni mwanzo wa watu kuanza kuweweseka na hawaijui kesho yao.
 
Hizo ni fikra na ni maoni yako, Tanzania kuna uhuru mkubwa sana wa kujieleza na ni haki ya kila mtanzania kutoa maoni! Hongera kwa kuitumia haki yako ipasavyo.
[emoji848]
Jiulize kwa mfano, mijadala ya TBC Aridhio, hasa comments na inputs za watangazaji, je, hayo ndiyo maoni ya Taasisi au ya kwao binafsi? Kwa sababu, kuna wakati unasikia comment au swali (directional!) la mtangazaji mpaka utabaki unashangaa. Is TBC mouth piece ya serikali au uwanja wa watangazaji kujimwaga? Je kuna mhariri anapitia maswali au comment za watangazaji, kabla hazijawa hewani live?
 
Asipoondoa Genge la Magu Samia atabaki skeleton tu

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Ewala, well said my friend!!!!

Kuna kundi fulani hivi ambalo ni la hovyo sana lilikuwa chini ya Rais wetu marehemu, walikuwa wakijiona kwamba wao ni wao na hiki kikundi kilikuwa kinamharibiwa hata Mh. Rais.

Kweli kabisa, ili Mama Samia aongoze vizuri lazima hili kundi litokomezwe kabisa, otherwise itakuwa ni vigumu sana kwa Mama Samia kusimama.

Halafu inatakiwa pia watu waelewe kuwa Magufuli alikuwa binadamu kama wengine, alikuwa na mapungufu kibao ambayo si ajabu aliwaathiri badhi ya watu kwenye chama, Serikalini n.k pamoja na kuwa kuna mengi mazuri pia aliyafanya.

Kwahiyo ukizingatia kuwa group dynamics zipo, hata nae mama Samia atafuata njia yake sio lazima afuate kila kitu cha Magufuli.

Kwahiyo hebu tumpe uhuru Samia, na watu kwenye chama acheni kumtisha Mama Samia, acheni kuibomoa CCM jamani.
 
Jiulize kwa mfano, mijadala ya TBC Aridhio, hasa comments na inputs za watangazaji, je, hayo ndiyo maoni ya Taasisi au ya kwao binafsi? Kwa sababu, kuna wakati unasikia comment au swali (directional!) la mtangazaji mpaka utabaki unashangaa. Is TBC mouth piece ya serikali au uwanja wa watangazaji kujimwaga? Je kuna mhariri anapitia maswali au comment za watangazaji, kabla hazijawa hewani live?
Hata jamaa yule wa Star Tv bure kabisaaa, analysis zake ni zeero😓😓😓😓
 
Wewe ndo unataka kumtisha au unataka kucheza na akili zetu. Wamtishie nini na kwanini? Acha hizo tumalize msiba
Kuna watu huwa hata mkisoma hamuwezi kuelewa chochote. Hata wewe Ni mmojawapo.

Hujui kinachoendelea kutokana na uwepo wa Rais mpya. Uko ktk mazoea yale ya kibongo bongo, uvivu wa kufikiri, uvivu wa kutafuta habari, kuupuza.
 
Akishazikwa Tu end of story...

Alikuwepo Nyerere hapa akiitwa Mlima Kilimanjaro na wengine vichuguu
Lakini alisahaulika haraka Sana ..

Bottom line .. waliokuwa wanamheshimu Samia toka zamani ndo watakaofaidika
Na waliompigania...
Wengine wasubiri mkeka walio bet
Hii inaitwa utakula ulikopeleka mboga daadeki
 
Hauna akili, kwa hiyo Bashe hizo hela kaenda kumuonga mama Samia ili achague makamu wa rais?

nyumbu ni lini mtapata akili!?
Duuuh,hujui unachoongea.hujui system ya CCM inafanyaje kazi kumpata makamu wa Rais.

Katika hili siyo kwamba huna akili bali ni mbumbumbu mzungu wa reli. Kwa upumbavu wako wewe unadhani mama samia ataenda Kamati Kuu na kusema namtaka fulani basi wanapitisha tu.

Umetokea kijiji gani cha wajinga? Kaa tu kimya haya mambo huyajui. Tambua tu kila kundi Lina mtu wake na linataka apitishwe na kamati kuu awe makamu.

Ndiyo unaambiwa cartels ziko kazini. Ngoja niachane na wewe. Haya huwa ninajadili na watu wanalelewa.
 
Uchambuzi murua kabisa na umeitendea haki elimu yako. Wenye akili walikuwa wakijiuliza mbwembwe zote hizi tunataka kuthibitisha nini na kwa faida ya nani? Yes, lets say anakubalika kama media na "incumbents" wanavyoiaminisha dunia. Je hali hiyo itawezesha rufaa kwa mpendwa wetu arejee? Definitely nop! Kumbe nini? Kumuaminisha "amira" kwamba timu hii ndiyo iliyoleta kombe nyumbani hivyo kocha mpya aendelee kutumia kikosi kilekile. Nope! Nop! This is a trap. Plz get out of this trap.
 
Hapa naona kuna mawili kwenye hizo cartels zinazopigana kushika mpini.

Kuna vita ya ndani ya makundi ya CCM, na vita nje ya CCM lakini inayohusisha makundi ya wana CCM ambayo yanaweza kupata uungwaji mkono wa vyombo vya usalama.

Jambo moja nalodhani litakuwa gumu ni hivi, inawezekana vipi kundi linaloungwa mkono na vyombo vya usalama kushinda mahala ambapo nguvu ya uungwaji mkono wa mtu husika haipo ndani ya chama?

Nionavyo, regardless ya uungwaji mkono wa vyombo vya usalama kama tunavyoaminishwa (sijui kama ni kweli), binafsi bado naiona nguvu ya kura ndani ya cham mwisho wa siku ndio itaamua mshindi. Unless otherwise, huyu nae aingie na majina yake mfukoni, ila sio kutegemea nguvu ya vyombo vya usalama kwasababu haitahusika kwenye vikao vya maamuzi ya chama ( wajumbe kuhongwa, ukabila, etc).

Kuvitegemea vyombo vya ulinzi na usalama kwenye mambo yanayohusu maamuzi ndani ya chama kwangu naona ni sawa na kupotea njia.

Kwa hiyo vyombo vya Usalama vipo vipo tu havina say yeyote na vinapokea kama dodoki maamuzi yeyote ya chama? Kama ni hivyo basi Taifa hili litakuwa ni kama genge la wahuni.
 
Back
Top Bottom