Connect Dot: Nani anataka kumtisha Rais Samia na umaarufu wa Hayati Magufuli?

Eti naskia kuna kundi la wana CCM hawakutaka Mama aongoze nchi na wakawa wanataa kupindua katiba ila JWTZ likaingilia kati na haikutaka kuwepo ujinga!

Nimeskia tu vibarazani, sijui kama watu walikuwa wameshiba tu hawana stori ama vp
Saizi tutasikia ramli nyingi sana, kila MTU now ni mchambuzi mkuu
 
Wivu tulionao baadhi ya watanzania hadi kwa mtu ambae ashatangulia mbele za haki ni wa kushangaza sana.

Raisi msaafu wa Ghana Jerry Rawlings alifariki Nov 12 2020 na akazikwa Jan 27 2021, miezi miwili baadae huyu wiki tu maneno meeengi...waacheni wafanye wanavyotaka na marehem wao, nyie subirini wenu mumzike harakahara.
 
Mtoa uzi unamawazo hafifu sana tena sana. Hakuna aliye lazimishwa kwenda kuomboleza. Tumejipeleka wenyewe.
 
"Tutaelewana tu." Dr. Shika.
Vyombo vya ulinzi na usalama hazihusiki na mambo ya kisiasa, kitendo cha kuamini au kulazimisha vikosi vya ulinzi na usalama kushiriki kwenye siasa za nchi yetu itakuwa ni jambo la hatari sana kwa hatma ya siasa za Tanzania za leo, kesho na keshokutwa.

Mpaka sasa inaaminiwa na watu wengi mtandaoni kuwa ni nguvu ya JWTZ ndio iliyopelekea tangazo la kifo cha Magufuli kutolewa kwa umma na ndani ya masaa 48 mama Samia Suluhu kuapishwa kuwa rais wa Tanzania. Kama jambo hilo litakuwa na chembe chembe zozote za ukweli, basi tujue moja tu, nchi yetu haiko salama na Magufuli atakuwa ametuachia urithi mbaya na mbovu kupindukia.

Wasipo maliza tofauti zao ndani kwa ndani, tutegemea majaribio kadhaa ya mapinduzi ndani ya kipindi cha miezi sita mpaka mwaka. Sitaki kabisa kuamini hili, na Mungu aepushilie mbali.
 
Sidhani kama mtoa mada umefanya research yako

huu msiba umeleta shock kwa kila mtu tanzania na watanzania bado wanatafakali mustakabal wa taifa, wana matumain na mh mama, na hii kasi ya maendeleo ilitimizwa na hawa hawa waliopo na waliokata moto au kuleta ndivyo sivyo mzee aliwaacha kwan kasi yao ilikua ndogo sasa kwa mfano unaona nini kitamshinda anayefuatia?

mashule kongwe kukarabatiwa,
vituo vya afya, barabara kila kona mpaka kwa mtogole nimekuta lami hakyanan

miradi ya maji.
kila aina ya mradi .....
sio kwamba mzee ndio alikua anashika kono bao au spana ila alikua anafuatilia the same same Mama will do.

hizi zingine ni Lamli chonganishi tu na mambo ya Facebook.
 
Kwa mwandiko huu utakuwa unatokea nchi pendwa ya facebook.
 
Asante sana kwa kuwa straight bila kutikisa masikio.

Hapo nawaonea huruma wale waliokimbia njaa upinzani na kwenda kwenye kivuli cha mkrismass ili wapumue kufunguliwa kesi hovyo, na kufuata mtelemko wa kujipatia mkate wa kila siku.
 

Acheni uongo jamani swala la mama Samia kuwa Rais liko ndani ya katiba sio chaguo la CCM mtadanganywa mpaka lini?
 
Nasikia kitendo cha Madelu cha kuapishwa pale chatou kilimpatia jeuri na kuanza kuwadharau wasaidizi wa aliye mchagua.
 
Umepotea sana ndugu yangu,
Kwa taarifa yako ni kuwa humu jamvini wapo hata hao mawaziri ambao wapo kwenye system.

Hivyo wanazungumzia kitu halisi wanao kijua.
 
Alikuwa anatembezwa katika miji ya Ghana katika hicho kipindi?
 
Kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…