Conor McGregor kuzichapa na Dustin Poirier usiku wa leo

screpa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2015
Posts
10,857
Reaction score
15,866
UFC 257 inawakutanisha tena Conor McGregor na Dustin Poirier kwa mara ya pili baada ya pambano lao la kwanza lililofanyika mwaka 2014 (UFC178) Conor kufanikiwa kuibuka na ushindi wa TKO Round ya kwanza.

Hata hivyo baada ya miaka mingi kupita Dustin ameonekana akiwa bora sana na kufanikiwa kuwapiga wakali kama Gaethje na Holloway na kumfanya kwenda juu kwenye Ranking (No2) kwenye uzito wa Lightweight, huku Conor akiwa No4. Lakini ikumbukwe pia hawa wote wawili wamepoteza mapambano yao dhidi ya mrusi Khabib Nurmagomedov ambaye mwaka jana mwishoni alitangaza kustaafu baada kumpiga Justin Gaethje, Khabib alikuwa na mazungumzo hivi karibuni na Rais wa UFC Dana White ya kumshawishi kubadili mawazo yake ya kustaafu.

Hatahivyo Khabib hakukubali moja kwa moja alisema atarudi ulingoni tena endapo atashawishiwa na performance ya wawili hawa. Hali hiyo inafanya pambano hili kuwa na mvuto maradufu huku likitarajiwa kuwa na mauzo makubwa ya ppv, je ni nani ataibuka mshindi? Majibu tutayapata usiku wa leo....

View attachment 1684056
ufc_20210123_103759_0.jpg
 
Conor Mr. mind games

Nakumbuka game yake na Khabib alisema atajipaka mafuta ya nguruwe ili Khabib asimshike... Akamkaribisha Khabib pombe aliyakuwa anajua khabib hatumii kilevi... Akamuita jamaa gaidi na kumfanyia Kila aina ya vituko ili tu kumtoa mchezoni

Siku ya game Baada ya Khabib kushinda sijui kilitokea Nini jamaa akamrukia mtu nje ya uringo
 
Hizi ni mbinu za kuongeza mashamsham kwenye pambano na kuongeza ppv. Ni mbinu ambazo kwa nyie wa nje huwa hamwelewi mnadhani ni kweli kumbe ni performance tu
 
Tatizo huyu jamaa kaingiza biashara chafu UFC,ananunua mechi toka alivyonunuliwa na Mayweather hizi mechi ananunua ndo mana anashinda tu hata apigwe vipi.
 
Hawa jamaa ni maadui kweli hata nje ya ulingo
 
Conor Mr. mind games

Nakumbuka game yake na Khabib alisema atajipaka mafuta ya nguruwe ili Khabib asimshike... Akamkaribisha Khabib pombe aliyakuwa anajua khabib hatumii kilevi... Akamuita jamaa gaidi na kumfanyia Kila aina ya vituko ili tu kumtoa mchezoni

Siku ya game Baada ya Khabib kushinda sijui kilitokea Nini jamaa akamrukia mtu nje ya uringo
Aliruka kwenda kumchapa chawa wa Conor 'Dillon Danis'
 
Tatizo huyu jamaa kaingiza biashara chafu UFC,ananunua mechi toka alivyonunuliwa na Mayweather hizi mechi ananunua ndo mana anashinda tu hata apigwe vipi.
Itakuwa hufuatilii UFC. Hebu niambie tangu kapigana na Mayweather kacheza mechi ngapi na zipi alizonunua kama kweli unafatilia
 
Hamna kitu kama hicho. Msidanganyike na performance kama hizo
Uaga kuna ugomvi wa kupangwa, ila hawa jamaa ni kweli hawaivi hadi leo hii, Khabib anamchukia sana Conor kwakuwa alifikia hatua ya kukashifu dini yake.
 
Bora kapigwa huyu jamaa, ana makelele mengi sana, well done Dustin
 
Conor Mr. mind games

Nakumbuka game yake na Khabib alisema atajipaka mafuta ya nguruwe ili Khabib asimshike... Akamkaribisha Khabib pombe aliyakuwa anajua khabib hatumii kilevi... Akamuita jamaa gaidi na kumfanyia Kila aina ya vituko ili tu kumtoa mchezoni

Siku ya game Baada ya Khabib kushinda sijui kilitokea Nini jamaa akamrukia mtu nje ya uringo

Mcgregory ni Mwehu, kwakuwa ni mzungu tu ndio maana vyombo vya habari vya Wazungu vipo kimya. Kosa angalikuwa ni Muafrika !!😒
 
Back
Top Bottom