"Constituency" Yako Ndiyo Siri Kuu ya Mafanikio ya Shirika Lako

"Constituency" Yako Ndiyo Siri Kuu ya Mafanikio ya Shirika Lako

Joined
Jun 21, 2021
Posts
16
Reaction score
14
1787846855602.png

Shirika lolote lisilo la kiserikali (NGO au Nonprofit), kufanikiwa katika utafutaji wa rasilimali fedha (fundraising) mara nyingi hutokana na kuomba fedha kwa watu sahihi. Kimsingi, fundraising yenye tija inahitaji uelewa wa kina na wa kimkakati wa "constituency" yako au kundi la watu wenye nia, uwezo, au maslahi halisi na kazi au maono ya shirika lako.

Kama alivyowahi kusisitiza mtaalamu wa masuala ya “fundraising” Hank Rosso; utambuzi wa “constituency” ndiyo moyo halisi wa fundraising. kufahamu ukweli huu ni hatua ya kwanza kuelekea kujenga msingi imara na madhubuti wa utafutaji wa rasilimali fedha kwa shirika.

"Constituency" ni Nini?
Kwa lugha rahisi, constituency ni kundi la wadau au watu wenye maslahi na shirika lako. Hii inajumuisha watu wanaoshirikiana nawe hivi sasa, wale waliowahi kushirikiana nawe huko nyuma, na wadau watarajiwa wanaoweza kuunga mkono maono ya shirika hapo baadaye.

Zifuatazo ni aina za “constituency”
  • Wadau wenye ushiriki wa dhati dhidi ya wale wasio na ushiriki wa dhati: Kundi hili linajumuisha wafadhili wanaochangia shirika mara kwa mara dhidi ya wale ambao hawajachangia muda mrefu.
  • Wenye Maslahi dhidi ya Wasio na Maslahi nashirika: Kundi hili linajumuisha wadau ambao mara nyingi husoma “newsletters” na machapisho mbalimbali ya shirika dhidi ya wale wasiosoma habari juu ya shirika.
  • Waliokaribu dhidi ya Walio mbali: Kundi hili linajumuisha wajumbe wa bodi na wafanyakazi wa shirika dhidi ya jamii inayoijua shirika kwa jina tu.

Wadau wa Asili “Natural Constituency”
Baadhi ya mashirika yana bahati ya kuwa na wadau wa asili ambao hutambuliwa kwa urahisi. Mfano wa Taasisi hizo ni kama zifuatazo;
  • Taasisi za Elimu: Wadau wa Taasisi hizi hujuisha wanafunzi/wanachuo wa sasa na wale waliopita (alumni), wazazi na ndugu wa wanafunzi/wanachuo.
  • Sekta ya Afya na Hospitali: Wadau wa Taasisi hizi hujumuisha Wagonjwa waliopata matibabu na kupona pia familia za wagonjwa hao.
  • Makundi ya Sanaa na Utamaduni: Wadau wa Taasisi hizi hujumuisha wateja wa kudumu, wanachama, na wahudhuriaji wa maonyesho ya sanaa.

Hata hivyo, kama shirika lako halina wadau wa asili kama mashirika niliyoainisha hapo juu, fahamu kwamba una nafasi ya kutengeneza “constituency” yako. Kwa msingi huo shirika lako linaweza kutengeneza “constituency” kupitia makundi yafuatayo;
  • Wafaidika wa huduma za shirika (Beneficiaries): Kundi hili linajumuisha wale wanaonufaika na huduma za shirika.
  • Watoa Huduma wa shirika (Service Providers): Kundi hili linajumuisha wafanyakazi na wale wanaojitolea kwa ajili ya utekelezaji wa miradi na programu mbalimbali za shirika.
  • Uongozi (Leadership): Kundi hili linajumuisha wajumbe wa bodi na viongozi mbalimbali wanaosimamia shirika.
  • Watetezi wa Shirika (Advocates): Hili ni kundi la watu wanaoamini misingi na utume wa shirika. Kwa imani waliyonayo kwa shirika wamejipa jukumu la kueneza misingi na utume wa shirika kwa makundi mengine.
  • Wafadhili (Advocates & Donors): Hili ni kundi la watu,taasisi na kampuni ambazo zinaunga mkono jitihada za shirika kwa kutoa rasilimali fedha,utaalamu n.k.

Hatua za Kufuata Ili Kutengeneza “Constituency” ya Shirika Lako
Ili kuhakikisha wadau wasio na mchango na shirika wanakuwa na mchango kwa shirika, Hank Rosso anashauri kufuatwa hatua nne zifuatazo;
  1. Kutambua (Identify): Bainisha ni akina nani wanaguswa au kuwa na hamasa na maono ya shirika lako.
  2. Kuarifu (Inform): Waelimishe mara kwa mara kuhusu kazi za shirika, changamoto ambazo shirika linakabiliana nazo, na matokeo ya programu za shirika.
  3. Kushirikisha (Involve): Tengeneza fursa za wao kushiriki kwenye programu za shirika kama kujitolea, wakaribishe kwenye hafla zinazoandaliwa na shirika n.k.
  4. Kuza Uhusiano wa Kihisia (Bond): Imarisha uhusiano wao wa kihisia na maono ya shirika ili waone shirika ni sehemu ya maisha yao.
Mara nyingi watu huchangia mashirika kwa sababu ya watu (people give to people) na kwa sababu zingine maalumu. Mashirika hayapaswi kuwachukulia wadau/wafadhili kama "pochi za fedha," bali kama wamiliki wa maono ya shirika. Kwa kufanya hivi, shirika litaweza kufanya uwekezaji mkubwa kwa maana mdau anae jitolea leo baadae atakuja kuwa mfadhili wa shirika na mtetezi wa shirika.

HEINZ MANAGEMENT CONSULTING
Strategic Management | Resources Mobilization for NGOs | Training
📍 Msimbazi St, Near Padre Pio Shrine
P. O Box 11219, Dar es Salaam
✉️ Email: [email protected]
📞 Mobile: +255 719 518 367/+255 725 518 376
 
Back
Top Bottom