Constructive ideas zinahitajika hapa!!!!!!!!

Constructive ideas zinahitajika hapa!!!!!!!!

juma sal

Senior Member
Joined
Dec 18, 2011
Posts
156
Reaction score
88
Habari zenu wana-jf wababa,wamama,wakaka,wadada, rika langu na wengineo pia
Hili ni suala la ukweli hivyo basi uliyesoma hii thread naomba unipe mawazo yako ili nifanye maamuzi ya mbolea na yenye tija kwangu....na hii thread sio sehemu ya utani na masihara.
mm ni kijana mwenye umri kati ya miaka 23-30 pia ni mwanafunzi wa shahada ya kwanza, ktk pitapita zangu nimekutana na binti ambae ana kila kitu ninachokipenda awenacho mwanamke ambae siku moja atakua mke wangu...kwa dhati kabisa huyu binti nampenda...ila kabla sijamtamkia lilomoyoni mwangu nikam-google ili nitafute taarifa zake hasahasa back ground yake ya elimu(form 4 & 6) na hata account yake ya facebook( si unajua tena siku hizi watu hujianika facebook?)......hapo ktk elimu ndipo nilipopata taarifa ambayo imeninistua kidogo!!...mm na huyo binti tuko mwaka sawa chuoni ktk vyuo tofauti.... huyo binti japo anaumbile dogo kulinganisha nami lakini yeye mwaka mmoja baada ya yeye kumaliza form four mm ndo nilikua naanza form one!!!
Kwa mahesabu ya harakaharaka atakua amenizidi umri kati ya miaka 3-5 hivi.....swali langu je kama nitaammua kumfanya mke wangu na akiujua umri wangu ni mdogo kwake ataniheshimu kweli?....je ni busara kumuoa mwanamke aliekuzidi umri kama huu?....hivi atani-treat sawa kama mume au atanichukulia kama dogo?......naomba unishauri ktk hili, ahsante!!
 
mmh....ndugu yangu hapa kuna mawili....akijua umri wako....either atakukataa au kukukubali....lakini kwa asilimia 70 anaweza kukukataa....kwa sababu....wanawake wengi hatupendi wanaume tuliowazidi.....inakaa kama mama sukari.....
 
..Age is nothing but rather a Number... Ndio maana siku hizi watu huwa hawataji umri zao katika BirthDay Party's. STUKA
 
To be honest umri saa nyingine si hoja bali
ni mtu ame mature kiasi gani ..

Hapa tutakupa maoni yetu tu ..
Na maoni yangu ni kwamba be honesty with her muulize hayo maswali yeye muhusika.

All the best 🙂
 
Tafuta mwingine huyo mkubwa kwako,kukuheshimu ni ndoto na kujifariji tu.
 
Ki ukweli asilimia kubwa ya wanawake hatupendi tuwe na umri mkubwa zaidi ya wapenzi wetu.. At least mwanaume akimzidi mwanamke miaka mitatu na kuendelea hapo poa.. Ila wapo baadhi kwao sio ishu..Usimfiche, mwambie umri wako aujue ili afanye maamuzi mapema..
 
Wengi wa Watanzania wanaandika detail za uongo katika accaunt zao za FB inawezekana kiumri ni mkubwa lakini daima umri ni kama nambaza kuhesabia.
 
Ulichokiona FB wala usichukulie kuwa ndiyo uhalisia wake maana inawezekana siyo sahihi. Iwapo utagundua kuwa kweli uamuzi ni wako lakini nisingekushauri kuendelea nae.
 
kiukweli wanawake huwa tunajali miaka sana hasa mwanume akiwa mdogo kwako.ila pia mwanamke anawahi sana kukua na pia anatanuka akil mapema akianza kuona mbali na kukushaur utaona nakupanda kichwani sasa kukubali yote au kuongea nae uone atasemaje.
 
Mh, chunguza vizuri ujue umri wa huyo dada na kama amekuzidi umri sikushauri kuwa nae, na naamini hata yeye akigundua kua kakuzidi umri hatokuwa tayari kwa hilo
 
yaani ingekuwa ni mm siwezi kuwa na mwanaume niliyemzidi even 1year sembuse huyo jamani 2 be honest kwa mwanamke ni % ndogo sana anayeweza kukubali kuwa na mwanaume mdogo kiumri
 
Mmmh, atakubemenda bure, mwanamme akiwa mkubwa sawa lakini mwanamke lol
Hakuna 'security' hivi
 
Do you know the actual meaning ya kupenda kwa dhati?
Unamgoogle vipi mtu unayempenda kwa dhati?(kwa sababu ni mtu ambaye at least una a lot of info juu yake).
We utakuwa umemtamani kwa dhati au umempenda kwa dhis!
 
Back
Top Bottom