Control number kulipiwa hii imekaaje?

Nchi Kavu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2010
Posts
4,290
Reaction score
2,468
Unapochukua control number toka mamlaka au taasisi mbalimbali za kiserikali kwa lengo la kulipia huduma fulani, mara nyingi huwa tunaishia kwa mawakala kwa malipo. Sasa hawa nawakala (wa benki mbalimbali) hutoza kuanzia TZS 500 hadi 1000. Hii ni sawa?

Mamlaka husika tunaomba majibu. Hoja zao ni kuwa hawapati faida yoyote kupitia hizo namba, hivyo wanajiongeza. Ukisema hulipi na hutaki kukatwa wala hawana muda nawe.
 
Tunakimbiza
 
Inashangaza kweli aisee,
 
Deposit kwa wakala wa banks si ni bure!?

Jaribu wakala tofauti tofauti. Kwani bank ni mbali mkuu?
 
Boss nchi hii ni ya biashara huria. Ile commission anayopata wakala kwa miamala hiyo ni ndogo sh 100 sasa wakala anajiongeza ili naye apate chochote. Huo utaratibu sio sahihi lakini biashara lazima iwe na faida ndio maana halazimishi hutaki kumpa chochote anakuacha
 
Huko nako wanakatwa😂😂😂😂tena Tigo nadhani kiwango cha chini ni 1200
Kwa hiyo Wakala anaona unakwepa tozo hivyo anajiongeza, unakwepa 1200 hutaki kulipa 500?.

Lipeni tu acheni nongwa bana, kama TIGO likampuni likubwa linatoza yeye akuhudumie bure?.
 
Malipo ya serikali yote ni bure, ndio maana wao uchaji nje ya mfumo iliwapate chochote.
 
Vipi ikitokea umechukua Control Number then usifanye malipo husika mpaka Control number ika expire apo kuna kuwa na kosa kisheria na sheria inasemaje juu hili, msaada jamani kuna jamaa wale wa mawakala wa vipimo kanipeleka hadi polisi kisa sijalipia Control number niliyochukua
 
Malipo ya serikali yote ni bure, ndio maana wao uchaji nje ya mfumo iliwapate chochote.

Acha uongo

Weka pesa kwenye simu yako leo alaf ukalipie control number ya Serikali uone kama hawalati ada yao.

Mfano ukituma laki 2 wanakata 4K.

Tusitoe ushahidi wa uongo JF ni mtandao wenye heshima zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…