Mkuu ukweli mchungu ni kwamba wengi zaidi bado wanamuenzi, kama upo Tanzania jiulize maswali haya:
- Hapo mtaani kwenu ni watu wangapi wanavaa barakoa ?
- Hapo mtaani ni watu wangapi wanapeana social distance ?
- Kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri ni watu wangapi wanavaa barakoa ? Hayo mabasi yana social distance au yamejaza nyomi kama kawaida.
- Kwenye viwanja vya mpira kuna social distancing ?
- Mara ya mwisho kusikia kampeni ya kuelimisha watu kuhusu corona umeisikia mtaani kwenu lini ?
- Watoto wa shule wanapewa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu ?
- Watu wakienda bar na club wanachukua tahadhari zozote ?
- Katika rafiki au ndugu zako 10 ni wangapi wapo tayari kupokea chanjo ya corona ?
- Lini serikali imetoa takwimu rasmi zinazoeleweka kuhusu maambukizi ya ugonjwa huu , zaidi ya kusomewa tu taarifa haraka haraka ambazo tuliambiwa tuna wagonjwa 100, wapo mkoa gani hatujui ? Taarifa mbona hazijafika WHO ?
Serikali ya sasa inachofanya ni kuiaminisha dunia kwamba tupo serious kwenye haya mapambano ili tupate mikopo na tusitengwe ila kiuhalisia ni kama tunaendelea vile vile, wananchi ndio kabisa wanaenzi yale yale ya mwendazake, sana sana utakuta raia wa kigeni ama wale wenye kipato cha kati na kwenda juu ndio wanavaa barakoa na kujitahidi kunawa mikono na kufuata ushauri mwingine wa wataalam wakiwa kwenye shopping malls ama migahawa mikubwa.
Sikubaliani na msimamo aliouchukua Magufuli dhidi ya corona lakini huenda ndio msimamo uliokubalika na wananchi wengi zaidi, watanzania wengi tunapenda shortcut !