#COVID19 Corona: Bila Barakoa huingii stendi ya Magufuli

#COVID19 Corona: Bila Barakoa huingii stendi ya Magufuli

Kuanzia Jumatatu bila kuvaa barakoa stendi Magufuli hakuingiliki tena.

Hata hivyo inashangaza kwanini kuwataka wenye mabasi kuwa na sanitizers kwa ajili ya abiria.

Kama ilivyo kwa barakoa, afya ya mtu ni wajibu wake mwenyewe. Hizi za kutwishana majukumu ya wengine ndiyo chanzo cha kupalilia jamii isiyokuwa na uwajibikaji kwenye mambo yake yenyewe.

Hatua zaidi kudhihibiti misongamano isiyo kuwa na tahadhari itapendeza zaidi.

Chanzo: ITV Habari.
Nitasherehekea siku ukipata Corona!
 
Mkuu ukweli mchungu ni kwamba wengi zaidi bado wanamuenzi, kama upo Tanzania jiulize maswali haya:
  • Hapo mtaani kwenu ni watu wangapi wanavaa barakoa ?
  • Hapo mtaani ni watu wangapi wanapeana social distance ?
  • Kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri ni watu wangapi wanavaa barakoa ? Hayo mabasi yana social distance au yamejaza nyomi kama kawaida.
  • Kwenye viwanja vya mpira kuna social distancing ?
  • Mara ya mwisho kusikia kampeni ya kuelimisha watu kuhusu corona umeisikia mtaani kwenu lini ?
  • Watoto wa shule wanapewa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu ?
  • Watu wakienda bar na club wanachukua tahadhari zozote ?
  • Katika rafiki au ndugu zako 10 ni wangapi wapo tayari kupokea chanjo ya corona ?
  • Lini serikali imetoa takwimu rasmi zinazoeleweka kuhusu maambukizi ya ugonjwa huu , zaidi ya kusomewa tu taarifa haraka haraka ambazo tuliambiwa tuna wagonjwa 100, wapo mkoa gani hatujui ? Taarifa mbona hazijafika WHO ?
Serikali ya sasa inachofanya ni kuiaminisha dunia kwamba tupo serious kwenye haya mapambano ili tupate mikopo na tusitengwe ila kiuhalisia ni kama tunaendelea vile vile, wananchi ndio kabisa wanaenzi yale yale ya mwendazake, sana sana utakuta raia wa kigeni ama wale wenye kipato cha kati na kwenda juu ndio wanavaa barakoa na kujitahidi kunawa mikono na kufuata ushauri mwingine wa wataalam wakiwa kwenye shopping malls ama migahawa mikubwa.

Sikubaliani na msimamo aliouchukua Magufuli dhidi ya corona lakini huenda ndio msimamo uliokubalika na wananchi wengi zaidi, watanzania wengi tunapenda shortcut !
Mkuu, pokea like 1000!
Jana nimesema hivi hivi. Katika mapampano dhidi ya corona, wananchi walio wengi wanamuishi JPM!
 
Waweke Takwimu hizi takwimu za kusema " mia na ushee" si takwimu
 
Ila Tanzania kuna ujinga mwingi. Elimu bado haijasaidia kabisa watu. Kujikinga tu ugonjwa fulani ni jambo linahitaji mjadala kabisa. Mbona Ukimwi Kipindupindu Malaria nk matangazo ya tahadhari yapo miaka mingi mbona hampigi kelele?
Yaleyale ya mwenda zake unajifukiza halafu unatoka hapo na mipua na midomo wazi unaenda kuhemea na kukoholea wenzio.
Guys hii ni tahadhari tu. Na ni jukumu la serikali kutoa tahadhari hizo. Kesho mtakuja humu humu mara ooh serikali iingilie kati.
Umejiweka lock down na familia yako
 
Mkuu ukweli mchungu ni kwamba wengi zaidi bado wanamuenzi, kama upo Tanzania jiulize maswali haya:
  • Hapo mtaani kwenu ni watu wangapi wanavaa barakoa ?
  • Hapo mtaani ni watu wangapi wanapeana social distance ?
  • Kwenye mabasi na vyombo vingine vya usafiri ni watu wangapi wanavaa barakoa ? Hayo mabasi yana social distance au yamejaza nyomi kama kawaida.
  • Kwenye viwanja vya mpira kuna social distancing ?
  • Mara ya mwisho kusikia kampeni ya kuelimisha watu kuhusu corona umeisikia mtaani kwenu lini ?
  • Watoto wa shule wanapewa elimu ya kujikinga na ugonjwa huu ?
  • Watu wakienda bar na club wanachukua tahadhari zozote ?
  • Katika rafiki au ndugu zako 10 ni wangapi wapo tayari kupokea chanjo ya corona ?
  • Lini serikali imetoa takwimu rasmi zinazoeleweka kuhusu maambukizi ya ugonjwa huu , zaidi ya kusomewa tu taarifa haraka haraka ambazo tuliambiwa tuna wagonjwa 100, wapo mkoa gani hatujui ? Taarifa mbona hazijafika WHO ?
Serikali ya sasa inachofanya ni kuiaminisha dunia kwamba tupo serious kwenye haya mapambano ili tupate mikopo na tusitengwe ila kiuhalisia ni kama tunaendelea vile vile, wananchi ndio kabisa wanaenzi yale yale ya mwendazake, sana sana utakuta raia wa kigeni ama wale wenye kipato cha kati na kwenda juu ndio wanavaa barakoa na kujitahidi kunawa mikono na kufuata ushauri mwingine wa wataalam wakiwa kwenye shopping malls ama migahawa mikubwa.

Sikubaliani na msimamo aliouchukua Magufuli dhidi ya corona lakini huenda ndio msimamo uliokubalika na wananchi wengi zaidi, watanzania wengi tunapenda shortcut !
Social distance kwenye daladala za kwenda mbagala inawezekena
 
Too late what do you mean? What should have been early?

Kuwataka watu kuchukua tahadhari ni kuwatisha?

Haya si madhara halisi ya kutokutangaza sababu za vifo vya watu kwa kuficha ukweli?
Kuvaa barakoa sasa hivi ndio unaona suluhisho?
 
Social distance kwenye daladala za kwenda mbagala inawezekena
Social distance imeshindikana JKNIA ndio ianze kufanyika kwenye daladala ? Precision inajaza watu kama mapapai kwenye basi kutoka boarding gate kwenda kupanda ndege...huko KIA kwenye shuttle ndio usiseme...sasa hivi hii vita kovidi tupo tunafanya maonyesho ya sanaa ili kutengeneza "brand" nzuri.

Kama kovidi ingekuwa inaua kama inavyoua kwa wenzetu yangekuwa ni mauaji ya halaiki, inapiga na kutuumiza lakini si kwa viwango vya watu wa nchi za Ulaya, Asia, Amerika ya Kaskazini na Kusini !
 
Too late. Wasianze kutisha raia
Mijinga ni mingi mno. Tatizo kubwa la ujinga ni mtu kutokujua kuwa hajui. Hapo ndipo shughuli pevu ilipo.
Popote ulipo na wenzio mnaobisha juu ya ukivi 19, naomba muende ile wadi ya wanaotibiwa huo ugonjwa hosp. ya mwananyamala mlale huko bila barakao baada ya siky 14 mtupe mrejesho. Hapo tutawaamini.
 
Hizi ni kama zile takwimu za kutolewa kwenye mifuko ya koti kwenye vikaratasi vidogo[emoji1787][emoji2223][emoji205]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahaaaa. Zile zile tu
 
Back
Top Bottom