#COVID19 Corona: Chanjo hadi Desemba

#COVID19 Corona: Chanjo hadi Desemba

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Hii habari inavunja moyo. Desemba?! Tutafika kweli huko? Mbona Zenji kwao imeshatua?

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Profesa Abel Makubi alipohojiwa na kituo cha runinga cha Azam juzi, alisema kundi la kwanza kupata chanjo hiyo ni watoa huduma za afya.

Chanjo hizo, alisema zitaanza kuwasili nchini miezi mitatu kutoka sasa “lakini zitakazotumiwa na makundi mengine zitawasili Desemba.”

Hata hivyo pongezi kwenu:

"Profesa Makubi alisema kutokana na mlipuko wa tatu wa virusi hivyo, Serikali itahakikisha makundi yaliyo hatarini, wakiwamo watumishi wa afya wanachanjwa mapema. Alisema wapo watu ambao ni lazima kupata chanjo hiyo, wakiwamo wasafiri na wanaohudhuria mikutano."

Pana mtu alituchelewesha sana hapa wallahi!
 
Nakazia: "Alisema wapo watu ambao ni lazima kupata chanjo hiyo, wakiwamo wasafiri na wanaohudhuria mikutano."
 
Ukifurahi chanzo na pia jaribu kusoma mkataba wa SERIKALI na WANANCHI wake, amejitoa ataki LAWAMA.

Kazi iendelee
IMG-20210716-WA0020.jpg
 
Kidogo? Mbona Zanzibar chanjo imefika?

Ilikuwa muhimu kujua vigogo serikalini waliokwisha chanjwa. Usije kuta hapa mwenye shibe hajui kama kuna wenye njaa.
Wao wana ile ya Madagascar wanapiga taratiiiibu.......
 
Ukifurahi chanzo na pia jaribu kusoma mkataba wa SERIKALI na WANANCHI wake, amejitoa ataki LAWAMA.

Kazi iendelee View attachment 1855940

Wana nini hawa zaidi ya kutaka kutukamua tu?

Hawa ndiyo wa nyungu mikaratusi na matango pori.

We hold them responsible for all covid-19 deaths prior to the arrival of the vaccines. I hope that is fair enough.
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom