Corona: Hongereni UDSM mmefanya lilo bora

Corona: Hongereni UDSM mmefanya lilo bora

Wewe hujui kuwa si lazima inayosemekana ni dawa itibu hayo anayejiita mzinduzi anasema inatibu?

Kwani ile ya Madagascar haikuzinduliwa? Kwani yaliyosemekana inatibu hayakusemwa? Mbona baada ya kuifuata kwa mbwembwe walioileta waliufyata kama hawakuwahi hata kuisikia?

Vipi mzee mzima babu wa loliondo? Kwani hakuwa na dawa na orodha ya alivyokuwa akitibu?

Kamwulize jiwe na wenzao walioonekana wakifakamia vikombe vya jero jero kama maswahiba yao yaliyowafikisha huko kama yalitoweka, kwisha au hata kupata nafuu.

Nani asiyejua kuwa aliyesema za kuambiwa changanya na za kwako aliona mbali sana?
Hujaelewa .
Mnaosema korona haipo ile dawa nibya nini?
 
Hujaelewa .
Mnaosema korona haipo ile dawa nibya nini?

Ni kweli mkuu nilikuwa sijakusoma sawa sawa ninaparejea pale.

Unajua tuna mipuuzi ambayo ni renowned. Mara moja moja hutokea ukayafananisha na waungwana.

Si unajua hata kwa yenyewe, "usoni iko kama watu?"
 
Hivi mnaotaka Serikali iseme kuna CORONA mnaotaka iweje?baadhi wanataka Serikali ikiri na kuchukua hatua kali km lockdown na tuletewe misaada/kukopeshwa chanjo.Hatua ya Serikali kutokukir ni bora zaid.KAMA mtu anataka Karantin ajiweke mwenyewe.
Hapana ndugu, tunataka serikali itoe tamko kuwa nchi inakabiliwa na janga la corona na iwatake wananchi kuchukua tahadhari moja mbili tatu. Si lazima iwe lock down kwani huko kwa wenzetu wenye nazo walishindwa.

Watu wetu wengi ni wajinga - samahani ujinga si tusi, wanahitaji kueleweshwa na mwenye jukumu hilo ni serikali.

Ni mbaya kuendelea kuwaambia watanzania kuwa hospitali zina wagonjwa wenye changamoto ya kupumua ila sio corona. Serikali iseme kuna korona na kuwa korona ni hatari, watu wataielewa na kuanza kuchukua hatua.

Leo hii ni ngumu kumwambia mtu huku mtaani kuwa chukua hatua za tahadhari dhidi ya korona akakuelewa kwa kuwa serikali inasema hakuna korona.
 
Kinjeketile Ngwale aliwapiga fiksi watu juu ya risasi kuwa maji.
Huyu wa sasa kuhusu corona.
Hili taifa ni la ovyo toka zamani.
 
Wanasitahiri pongezi. Ila No. 5 mwishoni inaonyesha uoga. Wanataka kuwafurahisha watawala. Hata hivyo ni mwelekeo chanya. Tuendelee kujikinga na Corona.
 
Back
Top Bottom