Corona imekuja kuumbua uongo wa dini

Kuwa mwana wa Mungu,kunahitaji maelezo,kwa kuwa Yesu alizaliwa Na Maria,Mwanadamu, Lakini Mungu alipulizia Pumzi yake ili apate Mimba yule Mariam. Sasa tunasemaje kuhusu Adam ,Babu yetu yeye hakuwa na baba wala mama ,si yeye angelistahiki zaidi kuwa mwana kamili wa Mungu?
Eva yeye kaumbwa bila ya Mama ,hata yeye angelistahiki kuitwa mwana wa mungu.
Kuwa Mwana wa mungu hapa umsikilize yesu mwenyewe ,amejiitaje?
Mbona yeye alijiita 'MWANA WA ADAM''?

ama kuhusu kule Horini hakuwezi kuwa na Mtende?.
Qur-an haijakataa ,kuzaliwa yesu bila ya baba,ila imekuongezea information ambayo kwenye biblia haikuwemo.Huo mtende ulitajwa hapa kwa malengo mahususi,aliutikisa na kumletea tende kama chakula baada ya kujifungua.
Hatukuona kwenye biblia habari ya kunywa maziwa eti kwa vile kajifungukia Horini(zizi la ngombe) labda hii nayo ingelifanana
 
Napenda kumalizia kwa kusema kuwa Mungu yupo,na
Alituma wajumbe wake wengi tuu ili kuwatambulisha wanadamu.
Huu ulikuwa ndio mpango aliojiwekea yeye mwenyewe.
Manabii na mitume walikuja wengi sana duniani.
Lakini waliokuwa maarufu na wa mwisho wao ni Muhammad (saw), akifutiwa na Yesu (Issamwana wa Mariam),Mussa, na wote hao Babu yao ni Ibrahim( baba wa manabii wengiwa nyumba ya israil na Waarabu.)
Siku ya Kiama ipo
Na binadamu wote tutawekwa kitimoto kuhukumiwa kwa mujibu wa matendo yetu.
Hivi vitabu tulivyonavyo leo vikuu vya dinivinatupa mafunzo yanayo fanana sana.
Usizini,Uwa
Usiibe,Fanya kazi towa sadaka na zakka,
Kuwa Muadilifu na mwema,
Usiiuwe bila ya haki.
Usilewe,na usiseme uongo.
Usimshirikishe Mungu na iungu mingine.
Usifanye ushirikina.
nk....
 
Mkuu najua unatumia akilizako kutafuta fact katika imani za watu.

Lakini to be honest kila binadamu mwenye akili timamu kunakitu anacho kiamini kwenye maishayake ambacho hajakiona.
Ni vichaa na mataahiratu ndio unaweza kusema hawaamini chochote mana akilizao hazifanyikazi vizuri.

Leo ukienda kulala angalia saayako wakati unaingia kitandani alafu ukiamka angalia saatena alafu jiulize hayo masaa yaliyopita wakati umelala ulikuwa hujui chochote kinacho endelea popote, jiulize tena nini kilikuwa kina endelea kwenye maisha yako katika mudahuo.
Ukikosa jibu ndio ujue kuna vitu invisible vinaendelea kwenye maisha yako ambayo wewe huvijui na ndio MUNGU.

Hoja kwamba MUNGU hayupo ama hatupendi kwa sababu kwanini anaacha majanga yana ikumba duniani na kusababisha vifo sio sawa.

MUNGU ameumba watu hapa duniani kaziyao ni kumtumikia kumuabudu na kutendeana mema na sio kuishi milele hapa.

Hapa ni sehemu ya kupita na MUNGU hajali umekufa kwa njia gani, anajali umetenda jambogani la kumpendeza hapa duniani ili uweze kuishi milele mbinguni.

Binadamu kama ametenda mema ataishi milele baada ya kufa.

Majangayote yanayo tokea na kutoa uhai wa binadamu haina mana kwamba MUNGU hatupendi ama hayupo, MUNGU yupo na anaona kilakinachoendelea kwa binadamu.

Anaweza kuepusha na anaweza kuacha kwa sababu zake mwenyewe.

Matatizo mbalimbali yanayo mkuta binadamu haya manishi kwamba MUNGU hatupendi ama hayupo.

Binadamu mbali na matatizo yanayo mkuta amefanikiwa sana katika maisha yake kwa mambo mbalimbali aliyojaliwa uwezo wa kuyafanya na MUNGU, sitayataja nimengi na kila mtu mwenye akili anajua.

Mbali na majanga binadamu amefanikiwa kuishi kwa raha na anasanyingi zisizo hesabika.

Kumbuka hata wewe unawachapa watoto wako na haina mana kwamba hauwapendi.

Bina damu kupata tabu na kufa sio tatizo kwa MUNGU.

MUNGU haumii tunapo kufa miiliyetu, anaumia tukifa rohozetu.

Kitabu cha mwanzo 3 - 23 kuna sehemu kinasema baada ya Adam kuhasi maagizo ya MUNGU, kwa kula tunda la mti wa ujuzi wa mema na mabaya, MUNGU akaamuru aondolewe katika bustani iliasile tunda katika mti wa uzima alafu akaishi milele hapa duniani.

Hapo utaelewa kwamba MUNGU anajali maisha ya milele mbinguni hapa duniani jambo la mana kwa MUNGU ni kumpenda na kufuata maagizoyake, kifo kipotu hata pasipokuwa na majanga kama HIV , Covid-19, Ebola nk.

MUNGU yupo, anatupenda wakati wote.
Lakini pia hutujalia neema na anatoa adhabupia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kwanza kabisa ukiikubali biblia kua ni kitabu cha kweli hupaswi kutoa dosari ambazo ziko ndani yake

Kutoa dosari katika biblia kwa kuilinganisha na kuran kunaonesha kua hukubaliani na biblia, bali unaangalia maneno gani ambayo kwenye biblia yana match na maneno ya kuran

Mkristo anaweza kusema kwa kutumia akili yake anakubaliana kua biblia ni kitabu cha kweli kilicholetwa na mungu, nawewe ukisema kitabu hicho cha kuran ni cha kweli kutoka kwa mungu halafu wote mkakubaliana kua mungu ni mmoja, hiyo ni "contradiction"

Mungu wa biblia ambaye kawasetia pepo ya kuimba na kuabudu milele na mungu wa kuran ambaye kawasetia pepo ya mabikra 72 wanaume. Mungu hao hawawezi kua mmoja

Mpaka hapo tunaona kua akili ya mtu kukubaliana na jambo fulani sio kipimo thabiti kujua ukweli wa hilo jambo ambalo yeye kalikubali

It's Scars
 

"Kiti cha enzi"

Huyo mungu anakaa kwenye hicho kiti inamaana ana makalio kama sisi?

Habari hii umeipatia wapi?

It's Scars
 
UNATAKIWA KULINGANISHA NA KUBAINI HITILAFU, MAFUNDISHO YA MSINGI
Kimsingi vitabu hivi vyote vinazubgumzia Mungu mmoja,lakini mapokezi na mikono ya watu imereport tofauti
Ndo maana Qur-a akajaribu kusahihisha pale palipokuwa na hitilafu,
huu ni ushahidi kuwa Chanzo ni kimoja,
 
"Kiti cha enzi"

Huyo mungu anakaa kwenye hicho kiti inamaana ana makalio kama sisi?

Habari hii umeipatia wapi?

It's Scars
Jiongeze kujisomea, Najuwa wewe akili yakoiko kwenye makalio tuu,unafikiria kujisaidia ,lakini hayo ni Muhali Kwa Mungu,wala hahitaji hayo.
Kile kiti ni Sovereign tuu, kuonesha ukuu kwa viumbe kama alivyotuumbia sisi kuwa wafalme wetu huwa na viti vya vya kiutawala,Hii ni methali tuu,Lakini Mungu hafananishwi na kitu chochote ukijuacho kuwa ni kitu,lakini yupo na anona na kusikia
 
Mkristo anaweza kusema kwa kutumia akili yake anakubaliana kua biblia ni kitabu cha kweli kilicholetwa na mungu, nawewe ukisema kitabu hicho cha kuran ni cha kweli kutoka kwa mungu halafu wote mkakubaliana kua mungu ni mmoja, hiyo ni "contradiction"
Sasa inaonesha unaanza Kuamini Uwepo wa Mungu, lakini unaelekea kwenye Ukiristo,
Ok ,hatua si ndogo,
Pia mimi nakualika kujisomea Qur-an pia ili akili yako ijuwe pande zote mbili naiwez kuwa huru,
ukikwama ,tunaweza kushauriana katika hilo.
Imani si kiti cha urahisi rahisi
Mungu ni Imani ya Hakika yenye Fcts za kutosha.
 

Mwanaharakati nisiye na dini, nawakunja waumini kila mkao utadhani john sin.../

Nawapagawisha mi ndo wenu teacher, kwa vina adimu natoa funzo zaidi ya hao ma-preacher.../

Leteni sadaka masta nihubiri juu ya kinasa, yule pasta mliyemtolea yuko kuzifanyia anasa.../

Fikra za muafrika zimepotoshwa kwa juzuu, wajanja tusha sanuka wamebaki mazuzu.../



It's Scars
 
Tatizo lako unaandika maneno mengi sana alafu haujibu maswali yangu.
Hizo habari za Adam na Hawa Koran ilizipata wapi kama si kwenye Biblia?

ama kuhusu kule Horini hakuwezi kuwa na Mtende?.
Hakuwezi na mimi nimeshafika Bethlehem alipozaliwa Yesu tumeelezwa yote.
Hiyo haitoshi si wote tunaweza kufika Israel, Biblia haijaandika alizaliwa chini ya mtende.

Qur-an haijakataa ,kuzaliwa yesu bila ya baba,ila imekuongezea information ambayo kwenye biblia haikuwemo.
Kama haikuwemo wewe umeitoa wapi? Yani Koran iisemee Biblia like seriously?

Huo mtende ulitajwa hapa kwa malengo mahususi,aliutikisa na kumletea tende kama chakula baada ya kujifungua.
Uwiii nasekaga!
Biblia inasema Kristo alipozaliwa ilipnekana nyota ya jaa ambayo iliwaongoza mama jusi wa mashariki mpaka horini na walimpelekea mtoto Yesu zawadi.
Ndio maana kipindi cha Christmas huwa unaona kitu kinaitwa Boxing day.
Hizo story unatoa wapi wewe?

Hatukuona kwenye biblia habari ya kunywa maziwa eti kwa vile kajifungukia Horini(zizi la ngombe) labda hii nayo ingelifanana
Biblia inazungumza habari za kupelekewa zawadi tu na mama jusi haisemi alikula tende wala kuzaliwa chini ya mtende.

Naomba uniambie Muhammad alijuaje kama Biblia imepotoshwa, alijuaje kama Yesu alizaliwa chini ya mtende, alimjuaje mama yake na kujua manabii wakale wote waliopita walifanya nini na kwa ajili gani?
 
Hii ni misingi yako tu hakuna Mkristo mwenye hii misingi.
Msingi wa Ukristo ulio mkuu ni UPENDO na msingi wa pili ni kufuata mafundisho ya Kristo OVER!


Hii verse uliyoiweka hapa unaiamini?
 
I don't believe them do you got anything else?
 
Nikienda kanisan nikasikia maubiri ya padri huwa nacheka kimoyomoyo na kusema hapa niwe na kuja ilimradi tuu nisitengwe na wanajamii.
 
Hiyo paragraph ya mwisho sio kweli, mwenyezi Mungu mnambebesha misalaba ambayo sio. Hii haina tofauti kama unavyowaona wananchi kwa kilakitu kumlaumu Rais wa nchi.
 
HOW COVID-19 KILLS--I'm a Surgeon--And Why We Can't Save You


Source : Duc C. Vuong MD

N.B
Gonjwa la Covid-19 lipo hivyo tuzingatie maelekezo tunayopewa na Wizara ya Afya jinsi ya kujikinga na corona kwa kufuata hatua hizi rahisi : epuka misongamano, kukumbatiana, kusogeleana , epuka kuwa abiria wa bodaboda, nawa mikono mara kwa mara kwa maji yanayotiririka n.k
 
Nenda na chain hii nani alimza mzazi wako nk nk nk nk mpaka ukomo wake

Sent using Jamii Forums mobile app
Chain hiyo ukiifata bila kuipindisha itakuletea swali kua hata mungu naye atahitaji chanzo

Mzazi wa mungu ni nani? Baba na mama wa mungu nao watahitaji chanzo

Mpaka hapo bado kuna mungu tena?
 
Hii ni misingi yako tu hakuna Mkristo mwenye hii misingi.
Msingi wa Ukristo ulio mkuu ni UPENDO na msingi wa pili ni kufuata mafundisho ya Kristo OVER!



Hii verse uliyoiweka hapa unaiamini?
Sikiliza ,Uzi huu ulikuwa ni wa Mtu asiyeamini dini ,wala Mungu,
Nadhani wewe unapokuja na hoja za kulinganisha Uislamu na Ukiristo,itabidi tuanzishe uzi wingine.
Lakini,kwa ufupi,Miminaamini kuwa Muungu wa Yesu ndiye Muungu wa Muhammad ,na ndiye Muumba wa kila kitu.
Habari ya kuamini aya aukutoiamini,ni suala jingine,kwani nisingeliicote kama siiamini na kuikubali.
Yesu hapa anatufunza kuwa yeye mwenyewe anaomba kwa Mungu,hivyo nasisi tufuate nyayo zake.
Yohana 17:
24 Baba, shauku yangu ni kwamba, hawa watu ulionipa wawepo mahali nilipo ili waweze kuona utukufu wangu; utukufu ambao umenipa kwa kuwa ulinipenda hata kabla ulimwengu haujaumbwa. 25 Baba Mtakatifu, ijapokuwa ulimwengu haukufahamu wewe, mimi ninakufahamu, na hawa wanajua ya kuwa umenituma. 26 Nimekutambulisha wewe kwao, na nitaendelea kulitambulisha jina lako kwao ili upendo ulio nao kwangu uwe upendo wao pia; nami niwe ndani yao.”
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…