Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Angalia tena video ya jana

Hakuna mpambe nyuma yake

Mkutano umefanyika ndani ya nyumba lakini kajipa distance ya kutosha na wakuu wa vyombo vya ulinzi na sidhani ata kama alienda kuwapa mikono baada ya kuongea nao

Hao wakuu wenyewe wamepeana big gap kwenye meza zao

Sasa kama wanaamini Corona sio tatizo kwanini wajihami ivyo.

Abiria chunga mzigo wako
 
Hizi mindset za kuwaza upinzani ni sawa na corona kweli tuna safari ndefu.
Ninyi wanasiasa pande zote ni tatizo kuliko hata hiyo corona yenyewe, kuna wakati nawaza labda mna mbingu yenu. Nyakati zote ninyi kwa kila jambo mnawazia ustawi Wa itikadi zenu ambazo hata hazieleweki hasa mnalenga nini zaidi ya kuboresha maslahi yenu kwa migongo ya wananchi wenu. Issue hii haihitaji hizo porojo zenu hata kidogo lakini hamshtuki asilani.
 
Mada kama hii yako ni ngumu mno kuiamini, na wala haiingii kabisa akilini.
Kukiwa na ukweli wowte juu ya haya uliyoandika hapa, basi hakuna serikali iliyowekwa madarakani na wananchi. Badala yake, kutakuwa na kitu kingine kabisa ambacho sina jina la kukipa.

Kuleta mada kama hii, halafu pasiwepo na aina yoyote ya ushahidi unaoipa mada uzito, angalau hata wa kimazingira tu, ni kulifedhehesha hili jamvi la JF.

Hii ni hatari sana kama kuna aina yoyote ya ukweli kwenye mada yako.
inawezekana haupo Dar wewe. na kama upo Dar basi Chanika huko!
 
Mkuu, wewe umeshuhudia watu wakizikwa kwenye hayo makaburi au ni hisia tu? Watu wangapi? How ndugu zao wamemlalamikia nani? Kwamba milio ya ambulance ni ushahidi watu 'wengi' wanakufa?

Ni kweli Corona ni tatizo, lakini hatutaishinda kwa kutishana na kujazana hofu. Tutimize wajobu wetu kuishauri Serikali juu ya hatua za kuchukua kwenye mapambano haya huku kila mmoja wetu akichukua tahadhari. Uongo na vitisho kwa wananchi havina tija, vina madhara makubwa zaidi.
Mkuu hivi ndugu wa dk Ulimboka, Lissu na wengine walilalamika wapi? Mie sikumbuki eti
 
Mkuu siyo kwamba immunity haikioni bali immunity at that age inauwezo mkubwa wa kupambana na vinelea vya magonjwa ukilinhanisha na hao walioenda umri.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu nilihisi hivyo hivyo kwamba kwakua watoto wadogo bado immunity yao inaendelea kutambua vimelea basi ni rahisi kwa immunity yao kudetect hivi virusi hata kabla havijaingia kwenye seli. Ila sijaprove hicho ninachohisi.

Sasa tumefeli wapi kujifunza juu ya hili? Kwamba watu wa umri huo dunia nzima immunity yao works the same? Na tunatofautiana, rangi, lishe, makazi n.k
 
Hali ni mbaya, tujitahidi kunawa mikono mara kwa mara na kuvaa barakoa.
 
..................Jamaa yangu Mohammed Fereji na ghorofa zake tatu pale Ilala na Kariakoo amezikwa kama kibudu jumapili jioni,nahisi upungufu wa vipimo vinafanya serikali kushindwa kutoa taarifa sahihi na kwa wakati so wanaamua kila anaekufa mazingira ya ghafla ni Corona kumbe wengine wanakuwa na maradhi mengine kabisa.

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
huyo jamaa yako ni nani mbali na jina, naomba kujua
 
Kwa lugha nyingine ulikiwa waambiwa hiyo virus haina tiba hivyo jaribu kutumia njia mbadalabkadiri uwezavyo ili mradi tu uendelee kuishi...

Kwenye suala la uhai hauhitaji hadi uambiwe na mtu/Rais ni jinsi gani unapaswa kufanya ili uendelee kuwa hai, jilinde na uwalinde wanao kuzunguka kadiri uwezavyo...
Mimi bado nina mshangao tu kuwa Rais amesema tujifukize sijui kawaza nini mheshimiwa
 
Hahaha...

Sasa sehemu kama hiyo inaweza geuka jehanamu, akiupata mmoja tu huko au mtu akiupeleka tu huko...balaa litaanzia hapo
Kuna jamaa yangu kaichukua familia yake yote ameipelekea Mafia kisiwani

Kanipigia anasema sehemu pekee salama kwa sasa ni huko

Nami nimemuahidi hata kwa kuogelea nitakwenda na wapendwa wangu
 
Hahaha...

Sasa sehemu kama hiyo inaweza geuka jehanamu, akiupata mmoja tu huko au mtu akiupeleka tu huko...balaa litaanzia hapo
Huko kisiwani jamaa kakodi nyumba nzima iko nje kabisa ya mji maisha yako chini sana amefanya manunuzi ya chakula cha mwezi na nusu hadi miwili hakuna cha daladala ni mwendo baiskeli tu
 
"Dar es Salaam lazima kuwe na wagonjwa wengi na vifo vingi kutokana statistically kuna Population kubwa".Hii kauli ni ya Mamlaka

Ukweli huogopesha lakini bora usemwe,Corona maeneo ya Dar es Salaam inamaliza watu, Hakuna mwandishi au gazeti ambalo linaweza kuhoji familia hizi zinazolia kila siku kwa kutowaona wapendwa wao wanaozikwa kimya kimya na Mamlaka

Kauli za kupeana Morali kuwa watu wachape kazi waongeze pato la Taifa Dar es Salaam litamsaidia nani? Hizi familia ambazo ndugu zao wanazikwa kwa kuugua corona zina mateso makali sana.

Watu maarufu na wenye ushawishi kwenye mamlaka na jamii ndio hao wanazikwa na watu wasiozidi ishirini au kumi, Je wewe kabwela ambae hutambuliki na mamlaka omba yasikukute

Uchunguzi ufanyike nini kinachoendelea maeneo ya makaburi ya huko Bahari Beach eneo la kondo,Buza na Mbweni

Uchunguzi ufanyike ongezeko la kelele za ambulance kwa wingi maeneo ya Dar es salaam kutoka hospital kuelekea maeneo hayo ni wangapi wanazikwa kwa janga hili

Tunakubaliana vita inahitaji umorali na nguvu lakini hili ni gonjwa sio vita linahitaji tiba tahadhari na ukweli

Leo hii kuna malalamiko makubwa watu wakifuatilia ndugu zao hospitali waliolazwa wanajibiwa alishafariki na kuzikwa na mamlaka kimya kimya,

Mamlaka imeamuru wizara ya afya ijibu kuwa sio kila mgonjwa hufa kwa corona ni kweli.Je kwanini wanazikwa na mamlaka bila hata ndugu kuhusishwa bali hujibiwa ndugu yenu alishazikwa amefariki

Wizara ya afya ni bora mkaongea ukweli ili watu wachukue tahadhari kuliko sasa mnapojaribu kuuma na kupuliza,

Paul Makonda alikuwa anapuliza na kufariji watu wachape kazi lakini visa vya watu kupukutika na corona sasa amebadili kauli na kuamua kuwa mkweli kuwa Dar corona inamaliza watu

Mamlaka kila siku inakuja na kauli kinzani kama corona sio ishu kwanini mnafunga shule Tanzania nzima, Ruhusuni baadhi ya mikoa elimu iendelee isipokuwa Dar na Zanzibar

Wanakijiji wasiojielewa na baadhi ya wapiga pambio wao hawachuji kauli za mamlaka, Hii itapelekea watu kuwa na morali na kupukutika zaidi
CIA wanajua ukweli unaofichwa na viongozi wetu ndio maana wakaamua kuondoa wamarekani wote juzi
 
Kuna jamaa yangu kaichukua familia yake yote ameipelekea Mafia kisiwani

Kanipigia anasema sehemu pekee salama kwa sasa ni huko

Nami nimemuahidi hata kwa kuogelea nitakwenda na wapendwa wangu
Hilo ndio linalotakiwa sasa, siyo kila siku mnatupigia kelele humu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Godzilla umeanza vizuri ila ulipomalizia hapo sijui upo eneo gani. Mfano Dar ambulance zimekua nyingi mno tena landcruiser mpya mpya ila haithibitishi kuwa zinabeba wagonjwa wa corona lakini zipo nyingi na zinazunguka mno. Pili uwepo wa magari ya HUDUMA ZA MAZIKO za jiji zikizunguka zunguka jijini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla ya corona hapakuwa na ambulance hapo dar?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tembeleeni usiku wa manane sehemu zilizotajwa kama Buza makaburini mkajionee
Bahari beach eneo la kondo Buza na Mbweni acheni kusifia mapambio ya mwami wa kihutu anaetupeleka kuzimu

Watu wanaokufa ni wengi sana aisee anakoongelea mfano Makaburi ya Kondo kila siku usiku wanazika zaidi ya watu wanne ......jana kuna mtu ndugu yao kazikwa pale Wachimbaji wakawaambia washazika zaidi ya 30 hadi jana ....sasa acha hayo makaburi mengine yakiwamo ya Mloganzila ...watu wanaotangazwa ni wale ambao ni public figure.
Lakini pia kuna kashfa ya watu wanaokufa kwa CONVID19 na ndugu zao wanafanya ujanja ujanja wanaachiwa wakazike wenyewe ......kuna ex IGP kapewa mke wake akazike na wengine wengine
 
Back
Top Bottom