Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Tetesi: Corona inapukutisha watu Dar. Kuna wanaolalamika ndugu zao kuzikwa kinguvu na Mamlaka Dar huko Bahari Beach, Buza na Mbweni

Mada kama hii yako ni ngumu mno kuiamini, na wala haiingii kabisa akilini.
Kukiwa na ukweli wowte juu ya haya uliyoandika hapa, basi hakuna serikali iliyowekwa madarakani na wananchi. Badala yake, kutakuwa na kitu kingine kabisa ambacho sina jina la kukipa.

Kuleta mada kama hii, halafu pasiwepo na aina yoyote ya ushahidi unaoipa mada uzito, angalau hata wa kimazingira tu, ni kulifedhehesha hili jamvi la JF.

Hii ni hatari sana kama kuna aina yoyote ya ukweli kwenye mada yako.

Huu ni Ukweli kabisa ,nnamjua mmoja alichimbiwa na Serikali.Alikuwa anafanya Biashara Jengo nililo Kodi na mimi pia.Siku 4 wanaifanyia Maiti uchunguzi na Ngugu hawakupewa Mwili.
 
Kama Mwalimu angelikuwepo leo mambo yasingelikuwa hivi

Kwanza anageanza na kaulimbiu:"Korona si lelemama" Mipaka lazima tufunge Mipaka"
Korona ni nduli"

Lakini kwa oyo nyanda tumekula malawi
 
Kwa Sasa naona hivi vyeo vya kuongea kwa niaba ya wengine vinatumika vibaya Sana !


God save us
 
Kama Mwalimu angelikuwepo leo mambo yasingelikuwa hivi

Kwanza anageanza na kaulimbiu:"Korona si lelemama" Mipaka lazima tufunge Mipaka"
Korona ni nduli"

Lakini kwa oyo nyanda tumekula malawi
Ooh! Nimekuelewa. Malawi hakunaga dhahabu, kuna mashiti tu aka schists.
 
Hii ni taarifa ya ovyo na ujinga kabisa, ebu tuondolee upuuzi wako.

Nani anae lalamika? huko unapopata pataja kuna uongozi wake kama kweli hii habari ya ukweli tutajie jina la Mtaa wanaozikwa watu.

Huko pia kuna raia wanaojitambua na kujua baya na zuri TUTAJIE MAJINA YA WATU WALIOKUFA NA KUZIKWA KIMYA KIMYA!! acha kabisa story zako za kijweni kuleta humu JF.

Tutajie nani ambae ndugu yake amezikwa kimya kimya, pia wanatoka mtaa gani? nani mjumbe wao wa washina?

Kwa jinsi ninavyo wajua mimi watanzania, kwa post habari picha na kurusha kwenye mitandao hizo picha zingezagaa kote tena kwa kasi ya 5G.

Ajali ya barabarani au mtu kafumaniwa na mke wa mtu raia wanarusha picha za kumwaga sembuse kifo cha corona ambayo ndiyo habari ya dunia!!!

Watanzania wenzangu CORANA IPO, TENA INAUA tuchukue taadhali.
Watu wabishi kweli yani. Alichoandika mtoa mada na niliyoshuhudia kuna ukweli 90%.
Sio kilakitu mbishe. Kama mtu hauamini basi unachill tuu. Watakaoconsider hiyo habari then watafikirisha akili zao kujua nn kinachoendelea kuhusiana na huu ugonjwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
inawezekana haupo Dar wewe. na kama upo Dar basi Chanika huko!
Mkuu M-mbabe, wewe ni kati ya watu nisiopenda kamwe kuwawekea mashaka katika wanayoyaandika, kwa sababu historia yako hapa jamvini inaeleweka na ni ya heshima ya kutosha.
Naomba nami unielewe kidogo ninacholiandika hapa.

Watu "wanapukutika", maana yake wengi tu kuliko kawaida wanakufa na serikali haitaki ijulikane kuwa watu hao wamekufa kwa ugonjwa wa COVID-19. Wanaficha ili takwimu zao zionekane sio za kutisha!

Nauelewa ulaghai mwingi sana unaofanywa na serikali hii kwa sababu zisizokuwa na msingi wowote, lakini kama wamefikia kwenye hatua hii, nadhani hawa watu sio binaadam tena.

Sasa swali ni moja. Tutaweza kupata ushahidi wa hawa watu kufariki na taarifa za kufariki kwao zifichwe? Hili ndilo swali ambalo ningependa tulitafutie ufumbuzi wa haraka.
Vinginevyo, sote hatuko salama chini ya serikali hii.
 
Rais anasema corona ugonjwa wa kawaida tuendelee kuchapa kazi. YEYE MWENYEWEKWA NINI AMEJIFICHA CHATO? KWA NINI ASIRUDI IKULU TUMUONE AKIENDELEA NA KAZI NA VIKAO KAMA KAWAIDA.
Ndugu zangu serikali inachotaka ni sisi tufanye kazi na ivune kodi zetu, suala la afya sio la msingi ndio maana inasema Dar haiwezi kuwa locked down kwa sababu itatoa revenues nyingi.
Chukua taadhari wewe na familia yako husidhani serikali itajali kuhusu maisha yako binafsi
 
Huu ni Ukweli kabisa ,nnamjua mmoja alichimbiwa na Serikali.Alikuwa anafanya Biashara Jengo nililo Kodi na mimi pia.Siku 4 wanaifanyia Maiti uchunguzi na Ngugu hawakupewa Mwili.
Hakuna anayekataa haya uliyoandika hapa. Inajulikana kuna watu waliofariki kwa ugonjwa huu na kuzikwa na serikali.
Je, huyo mwenyenyumba wako serikali haikumweka kwenye hesabu ya watu waliofariki tunaotangaziwa? Hapa ndipo penye utata.

Je, wapo watu waliofariki kwa ugonjwa huu na serikali haitaki wajulikane kuwa sababu ya vifo hivyo ni COVID-19?
 
Amana inatema Mochwari imejaa mpaka hakukaliki Wagonjwa na wazima wameamua kuondoka
Ni hivi Hospitali zinaanza kucollapse
Haya maCCM yamezoea mauaji Mkuu, hayana utu kabisa. Watu wanapoteza ndugu zao kila uchwao, yenyewe yamekalia kuficha ficha tu.
 
Wewe Ndiyo ulie leta hii habari then huna source yoyote ya kutuaminisha bora ungesema kuna ndugu zako kama watatu wamezika kwa style hiyo.

Mimi nafikiria ungekuja hata na baadhi ya picha au clip kwa siku tofauti ambulance zinapo enda kuzika maeneo ya makaburi si umesema unayajua.
Pamoja na kwamba mleta UZI hajaleta ushahidi but hata yale maneno ya BAshite na yenyewe huyaamini? Mbona yapo youtube kwamba watu Dar wanapukutika? Na akatahadharisha wa mikoni wasije Dar, huyo ni gavana wa Dar remember so anajua kila kinacho endelea jimboni kwake
 
Mkuu wewe amini siku ukishuhudia ndio utajua jinsi huu ugonjwa ulivyo hatari jikinge Sana. Watu wanakufa Sana serekali ikishachukua ndio Bai Bai.

Kuna mda nilimfikiria Magufuli nikakosa jibu kwanini kuwe uficho kiasi hiki,

Kuna wawili mme alikufa akachukuliwa kesho yake mke nae kachukuliwa Kama hawana korona siwangewapa ndugu wazike. Na wangesema watu wangejihami maana Hawa watu wanaishi na watu.

nakwambia siku ukishuhudia ndio utaelewa kwanini mleta mada analalamika.
Unajua mkuu 'Chuma cha Mjerumani', sikukatalii kamwe hayo unayosema, kwa sababu sina njia ya kukataa kuwa hayatokei.
Kinachonistua tu ni hicho cha serikali, kama kweli inafanyika hivyo.

Kama haya yaliyoandikwa kwenye mada yanafanyika, tena yakifanywa na serikali na kwa maksudi kabisa serikali hiyo ikificha watu wasijue kuwa yanafanyika..., hilo ndilo linalonitatiza sana mie.
 
Back
Top Bottom