Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Corona: Mizozo ya mipakani, wa kulaumiwa ni Tanzania

Inshu ya mipakani inaonesha kuna hujuma nyingi nafikiri pande zote mbili zimegeuka makubaliano

Nimesikia kiongozi wa madereva malori anasema mfano: mpaka wa rwanda na Tanzania gari zenye usajili wa rwanda au dereva wenye hati ya kusafiri wanaruhusiwa kupita mpakani japokuwa wengine wako na siku 30 hapo
 
Kwa kutokujikita kwenye mada mjinga mbona utakuwa ni wewe mkuu. Kwa kutokujikita kwenye mada iliyoko hapa hapa wewe mbona ndiyo mwenye kusubiri kusimuliwa. Umeshindwa kusoma na kujikita kwenye mada iliyipo hapa hapa, mfutilia habari utakuwa wewe?

Mbona mu watu wa kujidhalilisha namna hiyo?

View attachment 1470136

Haya mbona yameongelewa sana humu? Wewe huoni kama kuna tija yoyote?

Mkuu kama huoni si ubakie tu huko Twitter, Facebook au Instagram? Huko kutakufaa zaidi.

Mkuu akili ndogo kama yako huku itachemsha tu.
Kiswahili chako hichi kinaonyesha wewe Ni imposter..hatuwezi kuwa na mtz mjinga Kama wewe.
 
Sijaona ramli wala lawama popote. Si katika bandiko hili wala jingine lolote.

Kama hukuelewa, bandiko hili liko wazi:

View attachment 1470139

Jikite kwenye mada na unayoandika jiridhishe kuwa hujapotea njia.
Mimi nakujua mabandiko yako yale yale,umepiga ramli kuhusu maambukizi ya corona ,mara utake takwimu ,sasa hivi umeahamia kwenye lawama.
 
Inshu ya mipakani inaonesha kuna hujuma nyingi nafikiri pande zote mbili zimegeuka makubaliano

Nimesikia kiongozi wa madereva malori anasema mfano: mpaka wa rwanda na Tanzania gari zenye usajili wa rwanda au dereva wenye hati ya kusafiri wanaruhusiwa kupita mpakani japokuwa wengine wako na siku 30 hapo

Mkuu tatizo kubwa ni kuwa hatuna itifaki ya pamoja na hii tusipoangalia tutapoteza muda mwingi kutafuta mchawi kwingine ambako hatutamwona.

Rwanda raia wake anaingia nchini kwake kama ambavyo raia mwingine yeyote anaingia. Atapimwa Corona na quarantine ya siku 14 inamhusu.

Sisi hatutaki kupimwa Corona huko, wala hatutaki quarantine ituhusu.

Sasa hapo tukamtafute mchawi wapi wakati yuko hapa hapa?
 
Hivi corona ikiisha mleta uzi utaandika nini?Almost daily ni bandika bandua nyuzi za corona tu ukijificha kwenye kichaka cha uzalendo.Unalipwa kiasi gani kwa kila uzi ?

Mkuu corona ikiisha nitafanya sherehe kubwa ukipenda nitakupa ukaribisho ili ikiwezekana tuweze kumshukuru Mungu kwa kuwa manusura toka mikononi mwa watu waliokuwa wamepanga kututoa kafara pasipokuwa na uhalali wowote.

Binafsi ninakushukuru kwa kutambua kuwa sina cha kuandika kuhusu siasa, CCM, CHADEMA, NCCR, ACT, CUF, nk; wala kuhusiana na ulaji *matunda kimasihara*.

Binafsi Nina taabu kubwa sana na Corona. Corona siyo siasa, siyo vita vya uchumi wala siyo hujuma. Hili ni suala la survival. "A matter of life and death."

Hata hivyo nisiache kukumbusha mkuu kujikita kwenye mada. Tuwe na itifaki ya pamoja au kila mtu apime wageni wake au tuwe na maabara ya pamoja. Kama yote hayo hayawezekani tufunge tu mipaka kila mtu ajiju.

Tafadhali fahamu, mimi silipwi kama wewe na Sina haja pia ya kulipwa.
 
Siyo mtz huyu..angalia kiswahili chake kwenye comments zake.

Hoja mufilisi kabisa. Ungekuwa mtanzania mwenye chembe ndogo tu za uzalendo usingediriki kuandika wazo fyongo kama hilo.

Kwa mawazo yako unadhani wewe ni mtanzania kuliko wengine. Hayo sasa si ni yale ya simulizi za manyani kutokuona rear gate!

"Ama kweli akili ni nywele."
 
Kwa kilichotokea Marekani kwa watu kukusanyika kiasi kile kwa ajili ya maandamano,basi tutegemee janga kuwa kubwa zaidi,kama hoja iko hapo,
 
Mimi nakujua mabandiko yako yale yale,umepiga ramli kuhusu maambukizi ya corona ,mara utake takwimu ,sasa hivi umeahamia kwenye lawama.

IMG_20200606_160341_788.jpg
 
Inaonekana wewe si mfuatiliaji wa mambo
Mgogoro wa mpakani wa kenya na uganda,chanzo ni Tanzania??!!!
Mgogoro wa mpakani wa kenya na somalia,chanzo ni Tanzania???
Mgogoro wa mpakani wa kenya na tanzania,chanzo ni Tanzania

Halafu jiulize hapo kwa nini huyo kenya anagombana na majirani zake wote katika mipaka yake??!
 
Inaonekana wewe si mfuatiliaji wa mambo
Mgogoro wa mpakani wa kenya na uganda,chanzo ni Tanzania??!!!
Mgogoro wa mpakani wa kenya na somalia,chanzo ni Tanzania???
Mgogoro wa mpakani wa kenya na tanzania,chanzo ni Tanzania

Halafu jiulize hapo kwa nini huyo kenya anagombana na majirani zake wote katika mipaka yake??!

Options zote ziko mezani:

1. Kila mtu apime wageni wake
2. Tuwe na maabara moja ya pamoja mipakani.
3. Tufunge mipaka.

Ipi tunachagua?

Kelele za kila leo hazina tija!
 
Kiswahili chako hichi kinaonyesha wewe Ni imposter..hatuwezi kuwa na mtz mjinga Kama wewe.

Umeshindwa kusoma uzalendo uliotukuka kwenye uzi. Badala ya kujadili hoja umerukia matusi uchwara.

Kwa hakika imposter ni wewe na katika Tanzania hii, hatuwezi kuwa na mtanzania mmoja mjinga namna hii kuliko wewe.

Ama kweli kwa "nyani kuona kun*ule" ni shughuli pevu.
 
Yaani humu kuna vivulana vingi sana. Hivi wewe baba wa nyumba unasolve matatizo ya nyumba yako kwa kufuata maamuzi ya jirani yako? Wewe utakuwa mtu wa ajabu sana. Kuwa na maamuzi yako kama baba. Na hiyo ndiyo misimamo ya wanaume halisi.
Baba wa nyumbani ukija kwangu unafuata sheria za kwangu,kama kwangu ni lazima kuvua viatu basi lazima uvue,kama hutaki kuvua basi rudi ulikotoka,hata kama nikijaga kwako huwa unaniambia nisivue viatu mlangoni,kila nyumba ina sheria na taratibu zake,Kenya wamesema mkitaka kuingia kwao lazima mpimwe korona,nyie mnasema eti "mbona sisi hatuwapimagi"? Kwa hiyo msipooga kwenu na jirani mnampiga marufuku kuoga? Acheni ufala.
 
Kutaja visa vingi ndiyo ongezeko la pesa kutoka huko, ambazo zinagawiwa kuendana na idadi ya wagonjwa.. Yaani ukitaja na si kuthibitika moja kwa moja kwa visa hivyo, hivyo za kuambiwa changanya na zako
 
Hoja mufilisi kabisa. Ungekuwa mtanzania mwenye chembe ndogo tu za uzalendo usingediriki kuandika wazo fyongo kama hilo.

Kwa mawazo yako unadhani wewe ni mtanzania kuliko wengine. Hayo sasa si ni yale ya simulizi za manyani kutokuona rear gate!

"Ama kweli akili ni nywele."
Imposter
 
Options zote ziko mezani:

1. Kila mtu apime wageni wake
2. Tuwe na maabara moja ya pamoja mipakani.
3. Tufunge mipaka.

Ipi tunachagua?

Kelele za kila leo hazina tija!
Kila serikali ina mikakati yake kupambana na corona,serikali ya magufuli imetilia mashaka vipimo hivyo kutovitumia ktk upimaji ,serikali ya tz imechukulia corona kama suala la ki-usalama,tofauti na nchi zote za africa mashariki,msimamo wa serikali ya tz tangu corona inaingia ni kutofunga mipaka..kwa hiyo ishu ni simple serikali ya kenya ifunge mpaka wake kwamba hakuna chochote kutoka tz kitakachoingia kenya jadi corona iishe

Halafu kitu usichokijua, tanzania haiwezi kuwa na maabara moja kutokana na kwamba hadi sasa hakuna jirani yeyote anayeaminika na tz,kutokana na kwamba sisi tumechukulia corona kama security issue tofauti na wenzetu wamechukulia corona kama public healthy issue..ndo maana unakuta raisi juzi kawaambia watu wajitengenezee wwnyewe barakoa hata kama ni za sidiria,na si za kupewa msaada,ukitoa msaada wa barakoa zenye corona ni kosa la jinai
 
Waambie Kenya kwamba makubaliano yalikuwa kila mtu apimwe nchi yao na mipakani waoneshe vyeti tu. Sasa kwa kuwa wamevunja makubaliano inabidi wao wenyewe warudi upya mezani kuomba suluhu. Na round hii wametupa tena nafasi ya kuongeza trms zetu zaidi maana tuko upande wa ushindi as always kama mwanzo.

Kwa kuvunja makubaliano ya wali tunashukuru sana maana mpaka ufunguliwe tena upya itabidi tuongeze terms nyingine tena mpya na wafate matakwa yetu. Tutazidi kuongoza na wao watafa na watatii tu. Ukigeu geu huko huko kwao.

Mkuu usijichanganye mimi siyo Kabudi. Jikite kwenye mada kutambua yafuatayo:

1. Kuna matatizo mipakani na si Kenya tu bali hata Uganda na Rwanda.
2. Matatizo haya mzizi wake wa fitina uko kwenye kutokuwapo kwa itifaki ya pamoja.
3. Kwa kutokuwa na itifaki ya pamoja hatimaye sasa imekuwa ni sisi dhidi ya wengine. Tuna maslahi tofauti.
4. Kwa kutambua matatizo yatokanayo na uwepo wa maslahi tofauti hapo juu, ili kuondoa mzizi huu wa fitina uzi unapendekeza yafuatayo:

A. Kila mtu apime wageni wake kabla ya kuwaruhusu kuingia kwake.
B. Tiwe na maabara za pamoja mipakani.
C. Kama si A au B hapo juu inayokuwa ni muafaka kwa wote, basi mipaka ifungwe.

Haya ni mawazo huru kwenye uzi huru toka kwa mwananchi huru aipendaye nchi yake vilivyo.

Kwamba kuna makubaliano yoyote fyongo yalikuwapo? Waulize ACACIA au Barrick Gold.

Kuyapiga teke makubaliano yoyote yasiyokuwa na tija au maslahi, hilo mbona kwa mtu yeyote nadhani ni wajibu.

Haliwezi kusubiria ruksa kutokea popote.

Ni vyema kujikita kwenye mada.
 
Back
Top Bottom