Ndekrepha
JF-Expert Member
- Jun 4, 2020
- 1,506
- 2,664
Mkuu usijichanganye mimi siyo Kabudi. Jikite kwenye mada kutambua yafuatayo:
1. Kuna matatizo mipakani na si Kenya tu bali hata Uganda na Rwanda.
2. Matatizo haya mzizi wake wa fitina uko kwenye kutokuwapo kwa itifaki ya pamoja.
3. Kwa kutokuwa na itifaki ya pamoja hatimaye sasa imekuwa ni sisi dhidi ya wengine. Tuna maslahi tofauti.
4. Kwa kutambua matatizo yatokanayo na uwepo wa maslahi tofauti hapo juu, ili kuondoa mzizi huu wa fitina uzi unapendekeza yafuatayo:
A. Kila mtu apime wageni wake kabla ya kuwaruhusu kuingia kwake.
B. Tiwe na maabara za pamoja mipakani.
C. Kama si A au B hapo juu inayokuwa ni muafaka kwa wote, basi mipaka ifungwe.
Haya ni mawazo huru kwenye uzi huru toka kwa mwananchi huru aipendaye nchi yake vilivyo.
Kwamba kuna makubaliano yoyote fyongo yalikuwapo? Waulize ACACIA au Barrick Gold.
Kuyapiga teke makubaliano yoyote yasiyokuwa na tija au maslahi, hilo mbona kwa mtu yeyote nadhani ni wajibu.
Haliwezi kusubiria ruksa kutokea popote.
Ni vyema kujikita kwenye mada.
Ishu sio nyepesi hivyo mkuu. Haswa ukiwa una deal na ndumilakuwili.
Nadhani kwa situation hiyo kwa sasa option C ni muhimu zaidi. Ili somo lieleweke zaidi.