#COVID19 Corona ni Mtihani, Jee Ummy Mwalimu Amepasi Mtihani?. Mnaonaje Ampokee Majaaliwa as PM, na Majaliwa Ampokee Magufuli?.

Paskali nilichogundua hapo kwenye uzi wako ni wataalam wa afya karibia wote wameliwa vichwa, pili kuna kipindi hali ilikuwa mbaya hadi kufikiria viwanja vya sabasaba kugeuzwa hospitali kwa muda.
Tutafika tu
 
Kuhusu Covid19, JPM amewatumbukiza Watanzania kwenye Kanuni ya "Survival for the Fittest". Ukwel ni kwamba Mimi na wewe hatuna uhakika wa Ku- Survive kwenye Kanuni hii.
 
Paskali unataka kusemaje kwamba wataalamu wanaondolewa anaachwa layman ambae ni mwanamke na kwao Tanga ( wanajua kunyenyekea )... Aina hii ya uandishi ndio inakuachaga njia panda tunashindwa kukupa sehemu utulie mana hatukusomisomi
 
Hao waliong'olewa ndio wataalam na walitaka kufuata miongozo sahihi ya WHO, siyo mambo ya kujifukiza na kufuata mitishamba ya Madagascar. Tutapata jibu mwezi wa sita na wa saba nani alikuwa sahihi katia ya aliyetumbua na waliyotumbuliwa. Tuna hii clip tuitazame tena wakati huo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu
Upande uliochagua lazima ukuvue nguo tu, leo umeandika mambo kimhemko mpaka unataka Magufuli ampite majaliwa
Then unakaa unaomba na kulialia kila siku kwa nini hupewi teuzi?
Majibu ndio haya sasa
 
Huyu Pascal Nadhani Hajitambui, Maana logically Hauwezi Kumsifia Waziri ( Politician) ukawaacha Wasaidizi wake ambao Kimsingi ni Professional. Ukweli ni Kwamba Pascal na Anaowasifia wote Wamelichukulia Janga la Corona Kisiasa na wanafurahi Majibu Mepesi yanapotolewa bila takwimu. Watu wamezikimbia Hospital full stop...
 
Pascal Mayalla bhana........... mie sijawahi elewa nyuzi zako kabsa........na una njaa kweli kama jina la mzee wako, but usihofu ntakuona tu siku moja, kaudisiiii katakutosha .
 
Nimekupata mkuu, utawala huu ukitaka upate sifa mbele ya Magufuri weka taaluma yako pembeni, jitoe ufahamu na kila unapozungumza basi mwisho wa sentensi yako lazima umtaje Magufuri tena kwa kumsifia .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu soma tena huu uzi kuna ujumbe mwingine utaupata tofaut na ulivyowaza

Sent using Jamii Forums mobile app
 

What do you mean " ampokee" ?
Hakuna kupokezana , hapa kila mtu apitie tanuru la moto.
Mtu atangaze nia na apimwe na umma anaotaka kuwatumikia.
 
Kuhusu Covid19, JPM amewatumbukiza Watanzania kwenye Kanuni ya "Survival for the Fittest". Ukwel ni kwamba Mimi na wewe hatuna uhakika wa Ku- Survive kwenye Kanuni hii.
Struggle for existence and survival of the fittest!!
Tafsiri nyingine ni "pambana kivyako vyako...ukiugua sawa...ukifa sawa...ukiishi sawa.."
 
Paskali nilichogundua hapo kwenye uzi wako ni wataalam wa afya karibia wote wameliwa vichwa, pili kuna kipindi hali ilikuwa mbaya hadi kufikiria viwanja vya sabasaba kugeuzwa hospitali kwa muda.
Tutafika tu
Tumejuaje kuwa hiyo hali mbaya imebadilika???
Mbona hatupewi majibu ya kitaalamu...??
 
Hicho kipengele cha "NITSEMA KWELI DAIMA FITINA KWANGU MWIKO" CCM walishakiondoa hicho kipengere.
Sasa hivi fitina na uongo ndio nyumbani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri hajafanya lolote lile, Wameachia watu wafe bila sababu. Magufuli ni denier wa ugonjwa na Ummy anaendelea kufuata maagizo yake. Naibu waziri amefukuzwa baada ya kuongea ukweli kuwa "KUJIFUKIZA HAKUSAIDI BALI NI HATARI KWA AFYA" wakati Magufuli anaaminisha watu kuwa kujifukiza ndiyo TIBA kitu ambacho siyo kweli. Ummy hana msimamo ameachia wagonjwa wafe hivyo hafai kabisa kwa nafasi yoyote hata ya UDIWANI
 
Yule Mkurugenzi Mkuu wa MSD aliyetolewa siyo Medical Doctor bali ni mtaalamu wa Sociology. Sijui ukibadili hapo kama mada yako itaendelea kuwa na tija
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…