#COVID19 Corona ni sawa na UKIMWI kwa wazungu, msitutishe!

#COVID19 Corona ni sawa na UKIMWI kwa wazungu, msitutishe!

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
324
Reaction score
649
Kumezuka katabia ka watu kutishia wananchi Kuwa Corona ipo Tanzania utadhani wao wanaumwa Corona au ndugu zao wamekufa kwa CORONA. Watu wamebeba mabango Kuwa serikali inawaficha wagonjwa wa corona. Ukiwauliza wewe unaumwa? Ndugu yako anaumwa hiyo corona? Rafiki yako amekufa kwa corona? Wanabaki kusema watu wanakufa huko kwa Corona.

Niwaambie na kuwashauri Watanzania wenzagu Corona ipo Duniani kama ilivyo Malaria, UKIMWI n.k. Je Wazungu kule kwao Malaria ipo kama ili huku kwetu? Wazungu wanakufa UKIMWI kama tunavyofa Afrika? Kwani kipindi kile watu wanakufa Ebora huko Congo, Uganda n.k Tanzania au USA walikufa?

Hivi Kama Tanzania watu wanakufa kwa UKIMWI na Wazungu hawafi kwa UKIMWI ni dhambi kwa nchi nyingine watu kufa kwa Corona na Tanzania tukabaki salama? Huko kwenu kuna maiti zinaokotwa barabarani Kama walivyotutabilia? Tuache barbaric thinking. Badala ya kumshukuru Mungu Kuwa pamoja na watu huko Duniani kufa kwa corona Mungu umetuepusha na wingu hili tunabaki tunainung'unikia serikali kuwa inaficha utadhani wewe unaumwa na umefichwa! Hapana.

Mungu aliamua kutuachia UKIMWI na ametuepusha na Corona, shida nini? Watanzania tumerogwa na Nani? Inawezekana Tanzania corona ipo, lakini imedhibitiwa na aina ya vyakula tunavyo kula au aina ya maisha tunayoishi. Sasa kwa nini tulazishe tufe kama wanavyokufa wao? Nao Wazungu Mungu amewaepusha na UKIMWI na Malaria.
 
Usitulazimishe tuamini unavyoamini kila mmoja na achague wa kumuamini kama ni mwanasiasa sawa au la Kama ni wataalamu sawa.
Mimi nawaamini wataalamu.
 
Afisa Mtendaji kata,
ya covid 19 yapo nje ya uwezo wako achana nayo.
Endeleza pambio ndio unachoweza.
 
Watanzania tutumie akili katika kufikiri!

Kwanza tumshukuru Mungu kwa hali tuliyonayo hapa Nchini kwetu kuhusu haya maradhi ya COVID 19.Ukweli ni kwamba hata kama maradhi haya yapo hapa Nchini kwetu lakini yapo kwa kiwango kidogo ambacho si kama Wenzetu wauza chanjo na vibaraka wao humu ndani wanavyotaka iwe!

Kwa kweli tunamshukuru sana Mungu na pia Rais wetu Mhe. Dr.JPM kutoyumbishwa katika vita hii.

Cha msingi tuchukue taadhari muda wote kwani Tanzania si kisiwa!
 
Mbona nyuzi za corona zimekuwa nyingi sana humu?
 
Usitulazimishe kuwa Wapumbavu kama ulivyo wewe, tunao marafiki na ndugu waliokufa kwa dalili zote za Corona na vipimo tunanyimwa majibu na kuambiwa nyie eleweni amekufa kwa Pneumonia.

Kama kwenu hakuna wenye akili usilazimishe kila ukoo kuwa wa Mazuzu na Walamba viatu kama ukoo wenu.
 
Halafu unajiona msoomii..! Kwa vineno vya kibarbaric ulivyokariri. Nani kakudanganya Wazungu hawafi kwa Ukimwi? Wasipokufa wengi si kwa sababu ni Wazungu bali ni kwa sababu wameelewa jinsi ya kufanya mapenzi salama.

Ni mzungu gani utalala naye pekupeku bila kupima ukikutana naye siku ya kwanza? Lakini nyie mnalala kwanza na mwanamke mliyekutana naye kwenye basi halafu ndo unatoka kwenda kupima kama umeupata.
 
Halafu unajiona msoomii! Kwa vineno vya kibarbaric ulivyokariri. Nani kakudanganya Wazungu hawafi kwa Ukimwi? Wasipokufa wengi si kwa sababu ni Wazungu bali ni kwa sababu wameelewa jinsi ya kufanya mapenzi salama. Ni mzungu gani utalala naye pekupeku bila kupima ukikutana naye siku ya kwanza? Lakini nyie mnalala kwanza na mwanamke mliyekutana naye kwenye basi halafu ndo unatoka kwenda kupima kama umeupata.
Sasa wewe zuzu kama wao wanajikinga kwa UKIMWI KWA nini iwe shida kwetu tuliofanikiwa kujikinga kwa corona?
 
Usitulazimishe kuwa Wapumbavu kama ulivyo wewe, tunao marafiki na ndugu waliokufa kwa dalili zote za Corona na vipimo tunanyimwa majibu na kuambiwa nyie eleweni amekufa kwa Pneumonia.
Kama kwenu hakuna wenye akili usilazimishe kila ukoo kuwa wa Mazuzu na Walamba viatu kama ukoo wenu.
Kama upo kwa nini wewe hujafa? Kichwa nazi kweli.
 
Watanzania tutumie akili katika kufikiri!
Kwanza tumshukuru Mungu kwa hali tuliyonayo hapa Nchini kwetu kuhusu haya maradhi ya COVID 19.Ukweli ni kwamba hata kama maradhi haya yapo hapa Nchini kwetu lakini yapo kwa kiwango kidogo ambacho si kama Wenzetu wauza chanjo na vibaraka wao humu ndani wanavyotaka iwe!
Kwa kweli tunamshukuru sana Mungu na pia Rais wetu Mhe. Dr.JPM kutoyumbishwa katika vita hii.
Cha msingi tuchukue taadhari muda wote kwani Tanzania si kisiwa!
Kiwango kidogo wewe unakipima je? Au ni kwa kuota ndoto tu za mchana?
 
Usitulazimishe kuwa Wapumbavu kama ulivyo wewe, tunao marafiki na ndugu waliokufa kwa dalili zote za Corona na vipimo tunanyimwa majibu na kuambiwa nyie eleweni amekufa kwa Pneumonia.

Kama kwenu hakuna wenye akili usilazimishe kila ukoo kuwa wa Mazuzu na Walamba viatu kama ukoo wenu.
Acha kubeba kasumba pneumia nayo si ugojwa? Si inaua? Sasa kwanini ufikirie korona tu futa kasumba hiyo yapo magojwa mengi ya mfumu wa hewa yanayo uwa mamilioni duniani kote tangu enzi sasa epuka kasumba ya kudhani kila anaekufa kwa magojwa yanoyo husiana na kupumua ni corona.
 
Ni hivi unaweza ukapata corona na usiwe na dalili/usiugue (asymptomatic)

Unaweza ukapata corona na ukaugua na kupona.

Alieugua na ambae hana dalili anaweza kusambaza huo ugonjwa ndo maana tunaambiwa wote tuvae barakoa ili kuzuia huo ugonjwa usisambae. Yaani, assume una corona, jilinde, na ulinde wengine.

Watu wengi waliougua wanapona, lakini wengi, hasa walio na matatizo ya kiafya na watu wazee wako na risk kubwa ya kutopona huu ugonjwa.

Sisi tunaoishi karibu na wazazi tuchukue tahadhari. Usitukane watu wanaochukua tahadhari sababu huu ugonjwa haujapitia familia yako.

This is far from over.
 
Huwezi kufananisha hayo magonjwa.

Ebola (si EBORA) - Wazungu waliugua lakini waliougua ni wale waliokuwa na direct contact na wagonjwa wa ebola. Wao walipogundua wana huo ugonjwa wengi walitibiwa kwenye nchi zao. Waafrika hawana pa kukimbia, wanafia kwao. Huo ugonjwa kusambaa ni ngumu sababu wagonjwa wanatengwa mbali sana na watu ili ugonjwa usisambae. Hata mazishi wakifanya kuna usimamizi mkali sana sababu maiti inaweza kuambukiza huo ugonjwa. Unaua haraka sana, by the time una dalili huna nguvu hata za kusema ufunge safari uende mji mwingine, unafia hospitali au nyumbani.

UKIMWI - Husambaa kupitia kubalidilishana body fluids (blood transfusion, mama kwa mtoto, ngono zembe). Nchi zilizoendelea wanafundishwa jinsi ya kujikinga na zinaa na wana uwezo wa kununua kinga. Ni utamaduni wao kuzingatia utafiti unasemaje.
UKIMWI umeenea Afrika sababu watu hawatumii kinga, aidha sababu hawana uwezo wa kuzinunua, kuzipata, au hawaamini kwamba kuna kitu kinaitwa UKIMWI (nakutana na post kila siku humu ndani mtu anaandika UKIMWI haupo).

Corona ni ugonjwa unaosambaa kupitia hewa. Haichagui wewe ni Mwafrika au mzungu.

Ndio, kesi huenda ziko chini zaidi hapa Tanzania, hasa kwenye maeneo yasiyokua na mkusanyiko wa watu (vijijini), lakini ugonjwa upo.

Jihadhari.
 
Back
Top Bottom