Mabibi na mabwana moja kwa moja kwenye mada. Itifaki yote imezingatiwa.
Serikali ni chombo cha wananchi chenye dhamana ya kuwaongoza wananchi wake. Katika dhamana hiyo serikali haiwezi kuukwepa wajibu wake wa kutoa taarifa zilizo sahihi katika jambo lolote lile kwa wananchi wake.
Ni vivyo hivyo hata kwa taarifa kuhusiana na ugonjwa huu ambao hata una athari za moja kwa moja kwenye maisha yetu ya kila siku ukiwamo uhai wetu sisi wananchi kama mtu mmoja mmoja.
Ni ukweli uliowazi kuwa katika nchi takribani 195 zilizopo duniani, ni Tanzania pekee ndiyo iliyozikataa itifaki za msingi za WHO zinazoiongoza dunia kwenye kupambana na ugonjwa huu:
1. WHO inatambua ugonjwa huu kuwa ni janga la kimataifa. Kuwa ugonjwa huu ni hatari, unauwa, hauna dawa wala chanjo ya kujikinga nao.
2. WHO inatambua kuwa ugonjwa huu ungalipo na kuwa kama hatua stahiki za kuudhibiti hazipo, basi utaendelea kusambaa na hali kuwa hata mbaya zaidi.
Hata hivyo WHO inatambua ugonjwa huu kuwa utakuwapo kwa muda mrefu na kama jitihada sahihi za kuudhibiti zikiwapo, basi tunaweza kuendelea na maisha salama hata kama ugonjwa ungalipo hadi pale tiba au chanjo vitakapogunduliwa.
Matokeo yake yametufanya sisi kama nchi tusiwe na mshirika wala rafiki. Hakuna tunayemwamini si nchi wala mtu.
Wote wasiokubaliana na sisi wamekuwa kwetu ni mabeberu au wanatumika nao.
Nukuu iliyopo hapa chini ni ya member wa JF anayeonekana kuwa na taarifa zaidi kuhusu misimamo tata hii ya serikali yetu:
Kila mtu ni mbaya isipokuwa sisi?
Imekuwa sisi dhidi yao? Sisi dhidi ya dunia? Tumekuwa kina Rambo? Yaani "us against the world?"
Kwa nini kila mtu atuchukie sisi tu duniani humu? Kwa lipi la mno?
Member niliyemnukuu kaandika mengi likiwemo la kuwa Tanzania imechukua utaratibu wa kujenga "herd immunity" katika kupambana na huu ugonjwa.
Je, ni kweli Serikali yetu imechukua utaratibu huo wa kujenga "herd immunity" na imefanya hivyo kinyemela?
Kwa hakika wao kama wenye dhamana tu, hawawezi kukwepa. Ufafanuzi unahitajika.