CORONA: Nimempenda sana huyu Mkenya amechoma Sindano ya moto kwa wanasiasa (viongozi) wa Africa katika hii Video

CORONA: Nimempenda sana huyu Mkenya amechoma Sindano ya moto kwa wanasiasa (viongozi) wa Africa katika hii Video

Ndio wale wale, yeye ni kiongozi sio Mkenya wa kawaida, hana jipya huyo. Ni kama haya maneno yatamkwe na Makonda. Maneno matamu ya kisiasa tu, sema ana point nzuri.
Jamaa alikuwa mtata sana enzi zile akiwa msemaji wa serikali. BTW vipi ile project yake ya Machawood?...
 
Mkuu anaitwa nani huyu?
Ni governor machakos county Kenya. Ni Kati ya hawa anaowasema matajiri lakini katokea familia ya kimaskini. Alipata ufadhiri wa Masomo toka kwa mfadhiri wa kikanisa marekani chuo kikuu huko huko marekani.
 
Jamaa alikuwa mtata sana enzi zile akiwa msemaji wa serikali. BTW vipi ile project yake ya Machawood?...

Kipindi hicho akiwa msemaji alikua anaachia pumba kama za Bashiru au Pole Pole.
Machawood iliangukia pua.
Hakujua vipau mbele vya kaunti.
 
View attachment 1391437

Japo kaizungumzia Kenya,ila ni ujumbe mzuri kwa Viongozi wote wa Afrika
Hiki ndicho mpiganaji Magufuli anachopambania na anakifanya tz kwa vitendo! Wakenya karibu kwenye club…sisi tumeshatambua kipindi tangu Magu ashike usukani…safari apolo zimepungua na tunatengeneza appolo zetu hapahapa tz!
 
Nadhani huyu ni alfred mutua aliwahi kuwa msemaji wa serikali ya kenya
 
Yuko sahihi kabisa hajakosea, hapa wote tutakuwa sawa hakuna cha tajiri wala masikini, hakuna cha minister wala mkulima wote tutakufia hapa hapa.
 
Hiki ndicho mpiganaji Magufuli anachopambania na anakifanya tz kwa vitendo! Wakenya karibu kwenye club…sisi tumeshatambua kipindi tangu Magu ashike usukani…safari apolo zimepungua na tunatengeneza appolo zetu hapahapa tz!

Kuna sehemu nilisoma kwamba spika wenu anatibiwa mafua kule India, ilikuaje.
 
Kuna sehemu nilisoma kwamba spika wenu anatibiwa mafua kule India, ilikuaje.
Hiyo ilikuwa kabla Magu hajashika hatamu! Kipindi hicho hata nyumba ndogo zilikuwa zikitaka tu kwenda shopping Dubai walisingizia wanakwenda kwa ajili ya checkups india na arabuni! Kipindi hicho madaktari na hospitali zetu hazikuonekana kuwa na hadhi ya hata kufanya check-ups kwa vigogo hao!
 
That guy is probably one of the best performing governors in Kenya. What he has done for healthcare in his county is rivaled only by his neighbouring governor.
 
Hiyo ilikuwa kabla Magu hajashika hatamu! Kipindi hicho hata nyumba ndogo zilikuwa zikitaka tu kwenda shopping Dubai walisingizia wanakwenda kwa ajili ya checkups india na arabuni! Kipindi hicho madaktari na hospitali zetu hazikuonekana kuwa na hadhi ya hata kufanya check-ups kwa vigogo hao!

Tatizo mnapenda kutumia nguvu nyingi kusifia mpaka mnajisahau na kuanza kuongea uwongo, hapa nasoma taarifa za huyo Spika Ndugai alivyotumia mamilioni ya hela za walipa kodi kule India tena ilikua mwaka juzi tu kwenye hii awamu ya tano halafu bila aibu unadanganya eti ilikua enz za Kikwete.
Kule alikwenda mpaka na wasaidiz wake wote wakalipiwa kila kitu.

Fuata huu uzi hapa Gharama za matibabu ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, nchini India kwa kipindi cha miezi mitano kufuru!

Kwa uchambuzi wa ripoti ya CAG, Bw. Job Ndugai alikaa India kwa miezi mitano, sawa na siku 150. Kwa siku moja alilipwa posho ya dola 500 sawa na Sh. 1,160,100.00, na hivyo kwa miezi mitano alilipwa dola 75,000 sawa na Sh. 174,015,000.00.

Akiwa India alikuwa na wasaidizi wawili – maana alihamishia ofisi yake huko huko hotelini. Kwa gharama ya dola 450 sawa na Sh. 1,044,090.00 kila moja kwa siku, walilipwa dola 900 sawa na Sh. 2,088,180.00 kwa siku. Kwa siku 150 walizokaa India, walilipwa dola 135,000 sawa na Sh. 292,950,000.

Kwa ujumla, matibabu ya Ndugai kwa miezi mitano huko India yalitumia posho za sh. 466,965,000. na hapo bado gharama za hospitali huko India, na tiketi za ndege kwa watu wote hao, na bado gharama alizokuwa anatumia mkewe.

Takwimu hizi zilikuwa ni kwa mujibu wa ukaguzi wa CAG katika Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika hospitali za India.

Wakati huo huo tusisahau kuwa Bw. Job Ndugai aliendelea kupata mshahara wake na posho zake kama Spika wa Bunge ambazo idadi yake naomba kama kuna watu humu wanazijua watusaidie kuzitoa.

Hakuna anayejua kwa uhakika Bw. Job Ndugai alikuwa anaumwa ugonjwa gani uliosababisha hadi ofisi yake ihamishiwe 5-star hotel nchini India ambako alichukua VIP suite nzima. Mpaka sasa gharama za matibabu yake ni siri kama ulivyo ugonjwa wake.

UPDATE:

Soma pia

Kipindi hicho akiwa msemaji alikua anaachia pumba kama za Bashiru au Pole Pole.
Machawood iliangukia pua.
Hakujua vipau mbele vya kaunti.
Duh! Nakumbuka alipopata tu ugavana wa Machakos kuna msaidizi wake mmoja alinifuata (by the time I was a Secretary General of Tanzania Film Federation) ili kuwe na ushirikiano kati ya Federation yetu na Machawood, nikakabidhiwa kwa msaidizi wake anayeshughulikia Machawood anayeitwa Muniaf...
 
Tatizo mnapenda kutumia nguvu nyingi kusifia mpaka mnajisahau na kuanza kuongea uwongo, hapa nasoma taarifa za huyo Spika Ndugai alivyotumia mamilioni ya hela za walipa kodi kule India tena ilikua mwaka juzi tu kwenye hii awamu ya tano halafu bila aibu unadanganya eti ilikua enz za Kikwete.
Kule alikwenda mpaka na wasaidiz wake wote wakalipiwa kila kitu.
Hii issue ya Ndugai na matumizi ya ovyo ndiyo iliyochangia kuondolewa madarakani CAG...
 
View attachment 1391437

Japo kaizungumzia Kenya,ila ni ujumbe mzuri kwa Viongozi wote wa Afrika

Nimuunga mkono, na amesema vizuri.
Ingekuwa huku Tanzania, ungesikia huyo si mzalendo na ni kibaraka wa mabeberu. Na hapo utasikia jeshi la polisi ninamtafuta kwa makusa ya jinai.

Hii CORONA korona unatibiwa nchini kwako.
 
Back
Top Bottom