Unachokiandika ni kipi ndugu?
Kuna namna mbili; kuna asili ya lugha na chimbuko lake. Asili ni jinsi jambo lilivyoanza. Ukisema chimbuko maana yake ni mahali kitu kilipoanzia ama jambo lilipoanzia.
Unachomaanisha wewe ni chimbuko la Kiswahili (ijapokuwa umeandika asili). Kiswahili kimetokana na neno la kiarabu Sahil, ni neno la kiarabu na moja ya maana yake ni pwani. Kumbuka tuna lugha zetu za kibantu na nyinginezo. Ustaarabu katika miji na nchi zetu ulianzia ukanda wa pwani kwa sababu ni ukanda ambao ulikuwa na muingiliano na mataifa ya bara Asia kwa muda mrefu hususan waarabu. Hii lugha ilikuwa inatumika kibiashara ya kimataifa kwenye pwani ya Afrika Mashariki.
Tanzania kuna pwani na ipo Afrika Mashariki. Kenya kuna pwani na ipo Afrika Mashariki. Somalia kuna pwani na ipo Afrika ya Mashariki. Kwa hiyo kanda za pwani hizo zote zilikuwa zikizungumza Kiswahili. Sisi kwa watu wa bara kimeenezwa tu hususani kipindi cha Nyerere. Waulize wazee wetu, Kiswahili kilifanywa ni lazima kuzungumzwa kipindi hicho watu wananzungumza lugha ya makabila ya kwao tu.
Sisi ni jitihada ya kukitumia na kukienzi tukairasimisha rasmi. Lakini mmiliki wa hii mali ya lugha ya Kiswahili ni watu wa ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki.