#COVID19 Corona: Vifo vinazuilika tusijitabirie kwenye nadharia za kijinga

#COVID19 Corona: Vifo vinazuilika tusijitabirie kwenye nadharia za kijinga

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana ujinga si tusi bali ni hali halisi ya kuwa na uelewa mdogo au kutokuwa na uelewa kabisa kuhusu jambo fulani.

Hayupo binadamu mmoja asiyekuwa na ujinga katika mambo yote.

Kwamba kila mtu atakufa? Hilo ni dhahiri. Lakini halina maana kuwa tujifie tu hata kama ni kwa kujisalamisha wenyewe kwenye kifo.

Kwamba tuna Janga na watu wanakufa kwa uzembe wetu? Asivishwe Mungu lawama zisizomhusu kwenye hilo.

Chanjo za Corona zipo, zinapatikana bure na ni wajibu wa Serikali kuona kuwa tunaozihitaji tunazipata.

Pana hatua za kuwahami watu kuhusiana na Corona. Ni wajibu wa serikali kuhakikisha kuwa inawajibika kuwahami watu wake kwenye mambo yanayohitaji uwepo wake.

Kwamba serikali imeonyesha nia ya kuukataa wajibu wake? Hili litakuwa suala jingine sasa. Kwani ipo madarakani kwa ajili ya nini basi?

Kuwaitisha serikali kutelekeza wajibu wake ni wajibu wetu sisi kama wananchi.

Serikali haina mamlaka ya kuikataa miito yetu labda kama haituwakilishi sisi.

Ninawasilisha.
 
Bahati nzuri na wakubwa wanaondoka vizuri sna

Bado kuna mbuyu, amini nawaambia hayupo mwenye dhati yake ati kuwa yuko bega kwa bega na huyo mwamba.

Ukitikiswa huo utashangaa, kumbe hata kina kasimu mapili wanapelekeshwa na njaa kiasi hiki cha kujitoa ufahamu na hata kuonja sumu kwa ulimi?

Wako wapi kina balozi? Walikuwa na nafasi yote ya kumkatalia wamejikaza kisabuni hadi yamewakuta.

Eeh mola wetu ukazisikie Dua zetu.
 
Kama serikali ni wawakilishi wetu tunayo haki ya kuwataka kubadili mwelekeo.

Hatuwezi kulazimishana kukielekea kifo.

Ni muda sasa wakatuelewa.
Sasa unataka kufanyaje? Au unataka kuvaa barakoa au kunawa mikono? Kwani unataka wakueleweje? Au unaamua kujifungia nyumbani mwako!

Nafikiri hivyo ukivifanya tutakuelewa. Lakini ukiishia kulalama na ilihali unajua cha kufanya, tutakushangaa na kuku ogopa. Kama wewe ni kiongozi wa kanisa, funga kanisa na misa zote tumia on line.
 
Tatizo lako ni kuwa ume comment fasta fasta bila shaka hata kabla ya kusoma na hata kuelewa lolote.

Ndiyo maana umeuliza maswali lukuki ambayo yote hayahusiani na yako nje ya mada.

Ungekuwa umesoma ungekuwa umeona hayo.

IMG_20210304_175230_693.jpg

Ni vizuri kujiridhisha kuwa umo kwenye mada. Vinginevyo ni kuonyesha kiwango cha umbumbu wako tu jombi.

Ama kweli pana tofauti kubwa baina ya kusoma na kuelimika.

Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Wewe mchawi chanjo siyo bure zinauzwa!

Umeusikia uwepo wa COVAX?

Au ungali na matunguli mikononi? Kwenye wachawi wala marehemu wewe si ndiyo mama lao?

Hata kama zinauzwa maisha mnanunua wapi washirikina wakubwa nyie?
 
Umeusikia uwepo wa COVAX?

Au ungali na matunguli mikononi? Kwenye wachawi wewe si ndiyo mama lao?

Hata kama zinauzwa maisha mnanunua wapi washirikina wakubwa nyie?
Uchawi wako unakufanya upinge kila JPM anachofanya au kusema
 
Msiwe kama wajinga hizo chanjo zimeponesha taifa lipi? Hatuwezi kupokea chanjo bila wataaalamu wetu kuikagua kama inafaa am la
 
Msiwe kama wajinga hizo chanjo zimeponesha taifa lipi? hatuwezi kupokea chanjo bila wataaalamu wetu kuikagua kama inafaa am la

Mjinga usiwe wewe jombi.

Una habari wataalamu wetu wenyewe wangependa mno kupata hiyo chanjo?

Acheni siasa uchwara wakati watu wanakufa na kuwapo kwa chanjo tu kungewafanya wanaokufa kuishi.

Mna roho za namna gani nyie ambao hata chanjo zilizo bure mnataka kupotosha kuwa zinauzwa?

Unasema au unaota?
 
Kama serikali ni wawakilishi wetu tunayo haki ya kuwataka kubadili mwelekeo
Walipita kwa wizi wa kura kwenye mabegi meusi na kwa nguvu ya dola. Ndiyo maana wananchi wanaonekana kama takataka mbele ya serikali ya dikteta.
 
Walipita kwa wizi wa kura kwenye mabegi meusi na kwa nguvu ya dola. Ndiyo maana wananchi wanaonekana kama takataka mbele ya serikali ya dikteta.

Mkuu una hoja nzito.

Kwa hali hii pana haja ya kuwa na plan B. Ikibidi basi hata option zero.

Ni heri kufa huku tukipambana kuweza kuishi kuliko kukisabiria kifo cha kuletewa kijinga jinga namna hii.
 
Unamkosoa nani Rais wetu mtaalamu na nguli wa kemia na mwanasayansi.wew umekosa uzalendo wew ni kuwadi na kibaraka wa mabeberu hatukaki ujinga wenu.
 
Unamkosoa nani Rais wetu mtaalamu na nguli wa kemia na mwanasayansi.wew umekosa uzalendo wew ni kuwadi na kibaraka wa mabeberu hatukaki ujinga wenu

Kwani nani anautaka ujinga wenu mamburula nyie?

Mwanasayansi mkemia nguli unayempamba pamba ndiye huyu hapa anayetusakizia kufa?

IMG_20210218_174254_207.jpg

Au huyo ni mjomba wake tu?
 
Mjinga usiwe wewe jombi.

Una habari wataalamu wetu wenyewe wangependa mno kupata hiyo chanjo?

Acheni siasa uchwara wakati watu wanakufa na kuwapo kwa chanjo tu kungewafanya wanaokufa kuishi.

Mna roho za namna gani nyie ambao hata chanjo zilizo bure mnataka kupotosha kuwa zinauzwa?

Unasema au unaota?
Hujakatazwa kufuata chanjo, nenda katumie
 
Back
Top Bottom