KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,187
- 17,167
Gonjwa la COVID 19 limewatia hofu watu wengi duniani kote, na wenye uwezo watalichukua kama changamoto na kulifanyia kazi.
Ninay hakika Coronavirus atapata m-arobaini wake mda si mwingi. Atakuwa gonjwa la kawaida tu kama magonjwa mengine, kama ataamua kubaki katika jamii. Bado kuna uwezekano pia kwamba anaweza kusambaratika na kupotea kabisa kama yule SAR mwenzake aliyemtangulia.
Sasa nimekaa na kuwaza kidogo. Sijatumia mda mwingi kulifikiri hili; lakini nikiweka mawazo juu ya huyu corona kwa wiki nzima, na kupata fursa ya kugonga vichwa na mawazo na wataalam katika maeneo ya magonjwa haya, ninayo hakika kwamba tunaweza kutoka na njia mbali mbali za kumpiga huyu corona, hata katika mazingira yetu haya yenye ufinyu wa raslimali.
Sisi hapa hatunao uwezo wa kumwangalia corona kwa ukaribu wake ili tuweze kumshambulia. Kwa mfano, katika mazingira yetu haya hapa Tanzania hatuwezi tukasema tutafute njia za kumkata miguu yake ile ili asiingie kwenye cell za binaadam, hata kama tunajua anapenda sana kudandia kwenye 'protein' inayoitwa ACE2 (Angiotensin convering enzyme) inayopatikana kwenye cell zilizomo puani na sehemu nyingine mwilini.
Utafiti wa aina hiyo utahitaji vifaa tusivyokuwa navyo.
Je fursa yetu inapatikana wapi?
1. Hivi hatuwezi kumpunguza nguvu wakati anapoingia puani, kwa mfano. Ndio tutavaa barakoa, je tukiweza hata kupata dawa ya kupaka puani ikiwa na vitu kama pombe inayomwathiri corona, hilo halitasaidia? Huu ni utafiti rahisi kufanyika katika mazingira yoyote.
Kuna watu watakaokumbuka "Vicks Vapour Rub"..., eeh bwanah, haiwezekani kumpunguza nguvu? Fanya utafiti, utajua jibu.
Kila siku watu wanajipaka vipodozi, losheni/krimu, n.k., kwenye ngozi. Kuna kazi gani ngumu ya kutengeneza vipodozi hivyo vikiwa na aina fulani ya 'sanitizer' anayoweza mtu kujipaka mikononi na kukaa kwa muda mrefu ikipambana na huyu korona kwa siku. Njia pekee ya kujua ni kufanya utafiti, tena utafiti rahisi sana.
2. Fursa zipo. ACE2 inapatikana kwa wingi ndani ya mapafu ya binaadam, ndio sababu hiyo ndio sehemu yake ya mwanzo kabisa kuishambulia. Na kwa sababu anafanya uharibifu mkubwa kwenye mapafu, ndio maana wagonjwa wengi wanaokufa, maafa hutokea kwenye kushindwa kupata hewa, na ndio maana ya hizo 'ventilator' ambazo wengi tulikuwa hatuzijui, sasa hivi ni kama wimbo.
Ventilators ni mashine za kizamani sana, sio teknologia mpya hata kidogo. Mainjinia wetu hapo chuo kikuu hawawezi kuifumua 'ventilator' moja au kadhaa wakagezea tu (Reverse engineering) na kuzitengeneza nyingi tu za kutosha hata bila ya kuwepo coronavirus?
Kwa nini tusitumie fursa hii ya corona kuondoa mahitaji ya kuagiza ventilator tena?
Hali ni hiyo hiyo kwenye figo, nako imekwishathibitika kwamba corona anapapenda sana, kwa sababu ACE2 ipo kwa wingi huko pia, na matokeo yake ni kuharibu figo na kuwasababishia wagonjwa matatizo hayo.
Tunao wagonjwa wa figo, tena siku hizi wameongezeka sana sijui sababu ni nini (kabla ya corona). Hizi mashine za 'kidney dialysis' nazo tunaagiza toka nje. Kwa nini sasa hii fursa ya corona asitufumbue akili ili tutengeneze za kwetu
Nilisema nikikaa wiki nzima na kuweka mawazo yangu juu ya huyu corona..., tunaweza kumpiga vizuri sana kama tulivyompiga Nduli.
Hebu tugonge vichwa, pengine wataalam na wenye uwezo na raslimali nao watajitokeza kutuunga mkono.
Wanasayansi wetu wakati mwingine tunajidharau sisi wenyewe.