CORONAVIRUS: Naongeza miluzi ya tahadhari lockdown iharakishwe

CORONAVIRUS: Naongeza miluzi ya tahadhari lockdown iharakishwe

Titicomb

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2012
Posts
12,823
Reaction score
21,210
COVID-19 inachofanya kule Italia na Spain sio mzaha,

Hali imekuwa mbaya sana kwa hizo nchi kiasi cha maiti kuhifadhiwa makanisani. Pamoja na tamaduni zao kuchangia hali kuwa mbaya lakini kuna uzembe flani ambao hata sisi tunaendelea kuufanya, hutujifunzi kwao.

Vifo sasa vinawafuata vijana, mwanzo vilikuwa dhidi ya wazee lakini kadri siku zinavyo zidi kwenda na ndivyo umri wa wanaokufa kwa huu ugonjwa unashuka.

Hali ya hewa ya joto sio kizuizi kwa huu ugonjwa kuenea. Sema joto nahisi linasaidia kidogo wagonjwa kujisikia nafuu kuliko ukiugua kifua na mafua mahali penye baridi kali.

Italia na Spain zimefikiaje hali mbaya kiasi hiki? Jibu: Walichelewa kuchukua hatua ya kufunga mipaka viwanja vya ndege, train na magari. Kosa kubwa zaidi walichelewa kufunga mitaa au kuzuwia mizunguko ya watu mitaani (lockdown of streets).

Daktari bingwa wa upasuaji aliye badilisha kazi yake na kuwa mhudumu wa kitengo cha wagonjwa mahututi (ICU) cha wagonjwa wa COVID-19 Dr. Emanuela Catenacci anasema.

"Try to stop, try to stop - isolate people, stop contact in everything because otherwise the situation is, like, a tsunami, is a tsunami, when it starts to grow it's really… it explodes,"

"Don't think that it is happening here and [think] it can't happen everywhere else - because it will if you don't do anything to stop it."

Msome hapa Coronavirus: 'Everyone dies alone': Heartbreak at Italian hospital on brink of collapse

Spain inakaribia kuwa nchi ya pili kwa kasi ya maambukizi ya huu ugonjwa na vifo ikikaribia kuipita Iran.
Spain imefikia hapa sababu ya kupuuzia mambo na wenye mamlaka kuwaza pesa (uchumi) kuliko maisha.

Mfano Meya wa jiji la Madrid alikataa kusitisha tukio (Event) moja la kimataifa lilofanyika kwenye mji wake karibuni kwa kuhofia kukosa kipato kupitia watalii walio hudhuria tukio husika.
Alizembea hivi na kutetea kama sisi kwamba zitawekwa sanitizer za kutosha ukumbini, hii yote ni tamaa ya $500 milioni tu za hao watalii.

Gharama za matibabu na maisha ya raia wake wanaougua na kufa kwa hili gonjwa inazidi mara dufu ya hii fedha. Someni hapa sababu za kuenea gonjwa kwa kasi Spain na Italia Why did coronavirus hit hard in Italy and Spain? Some blame a lack of social distancing — and a lot of social kissing.

Tujifunze kitu kimoja muhimu hapa, pesa sio maisha ya watu. Pili joto halizuii kuenea kwa huu ugonjwa maana Italia na Spain hasa hapo Madrid ni jiji lenye joto sio baridi kama China, Korea ya Kusini au nchi zingine zilizokumbwa na hili gonjwa.

Kauli ya dada yangu wa wizara inayo husu haya mambo kwamba "tuombe Mungu kwakweli, maana hatuwezi kudhibiti(control)" ni mzaha mkubwa na utani na maisha ya watu.

Mungu yupo lakini kama hatutumii akili na utashi aliotupatia nawaambia tutaangamia kweli kweli na wala huyo Mungu hatatuokoa na mkono wa COVID-19. Nasema tusimjaribu Mungu kwa kusubiria miujiza.
Ina maana sisi ndio hatuna dhambi sana kuliko walikotutengenezea makusanyo ya vitabu vya Biblia huko Italia kwa warumi?

Are we more Christians than Romans? Ina maana sisi ndio tuna uislam safi kuliko huko Uarabuni na Uajemi ambako mtume (S.A.W) na maswaaba wake walikuwa wanafanya kazi yao ya kuhimarisha dini ya uisalam?

Are we more Islams than Arabs and Persians? We can't be serious!! Let's hope we're more Buddhists than Chinese who have nearly won the war against this pandemic disease. If we are doing nothing to help ourselves out of this tragedy but rather wait for God to save us, then surely we shall be forsaken!

Hivi kwanini hatuzuii nyumba za ibada, hatuzuii raia toka nchi zenye huu ugonjwa hasa za Ulaya na Afrika ya Kusini? Kufanya hivi ndio kujaribu kudhibiti tatizo. Fedha ya utalii itatutokea puani na yote ile tuliyo ingiza miaka 2 iliyopita na ya kipindi hiki cha ugonjwa itaishia kwenye kutibu na kupima, na kuzika watu walikumbwa na COVID-19.

Serikali mtaniwia radhi sina nia ya kutisha watu na kupotosha ndio maana nimeweka na rejea kwa njia ya internet hyperlinks. Najua mnajua lakini someni na hapa, pitieni hizo link. Fungeni mipaka na taasisi za ibada angalau kwa siku 21 (majuma matatu).

Tuombeane uzima, na kutakiana kila la kheri.

UPDATES
==================
Mkuu recommendations ni nini?tufanyeje?
  1. Tufanye lockdown baadhi ya maeneo ya mikusanyiko inayowezekana kuzuiwa kwa muda kama majumba ya ibada.
  2. Tuzuie wageni hasa toka nchi zilizo shambuliwa sana na huu ugonjwa.
  3. Tuache ndege na magari ya mizigo tu na ya huduma muhimu za kibinadamu.
  4. Mikahawa na vilabu vya pombe (restaurants and bars) viwe vya kuchukua huduma na kuondoka na bidhaa.
  5. Majumba ya sinema yafungwe.
  6. Kutolewe muongozo wa shughuli za mazishi na mikusanyiko yake, Mfano liwekwe shariti watu wakae mbali mbali na wanaobeba jeneza wavae golves, mask, na wawe wachache tu, sehemu kubwa jeneza libebwe na magari.
  7. Zizuiwe sherehe za kijamii kama harusi zinazokusanya watu wengi kumbini, au zifanyike viwanja vya nje na watu wakae umbali wa miata 3 au zisitishwe kwa muda.
Unaweza kuongezea, nashauri hii ifanyike angalau majuma matatu tu kwa majaribio, tusisubirie majanga kisha tuje kuwaomba radhi waliotoa tahadhari wakashughulikiwa kama ilivyo tokea China kwa yule Daktari alie toa angalizo kwa umma.

90% ya hao wagonjwa ni imported cases. Yaani wameingia Bongo wakati mzee Corona tayari keshazama ndani. All in all, joto sio sababu kwa kuwa South Africa sasa local transmission zimeshaanza maana kuna wagonjwa kibao ambao hawajasafiri kutoka nje ya Nchi.
Singapore wana wastani wa joto la 27°C lakini kuna kesi za wagonjwa ambao hawana uhusiano na kuutoa nje ya nchi.
Link ya taarifa rasmi ya serikali ya Singaore hii hapa Coronavirus disease 2019: Cases in Singapore
Wazungu wanasema seing is believing.

Singapore na Tanzania hasa Dar es Salaam tunafanana sana hali ya hewa, wastani wa joto hapa kwetu ni 29°C.
 
All in all hadi sasa tz wagonjwa 6...

Tukubali tukatae huu ugonjwa kwa africa its not a big deal sema umekuja kutafuta kick tu za bure.

Ingelikuwa kwel huu ugonjwa unasambaa kwa kasi africa nadhan robo ya watu sasa hivi wangekuwa washapoteza maisha maana si mchezo kabisa unavyoua...
 
Eti serikali inachojitetea ni kwamba wanaopata Corona TZ ni watu wasio na kinga nzuri kwenye miili yao, Utetezi wa kipuuzi kabisa, hivi wazee na watoto wana kinga imara kweli? Corona anaweza kuipata mwenye kinga imara alafu akawaambukiza wasio na kinga imara wakafa yeye aka-survive. So selfish!
 
All in all hadi sasa tz wagonjwa 6...

Tukubali tukatae huu ugonjwa kwa africa its not a big deal sema umekuja kutafuta kick tu za bure.

Ingelikuwa kwel huu ugonjwa unasambaa kwa kasi africa nadhan robo ya watu sasa hivi wangekuwa washapoteza maisha maana si mchezo kabisa unavyoua...
Tatizo hatuna maabara tosha za kupima, huko ambako unaona number ipo ubwa wanapima kila mtu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
All in all hadi sasa tz wagonjwa 6...

Tukubali tukatae huu ugonjwa kwa africa its not a big deal sema umekuja kutafuta kick tu za bure.

Ingelikuwa kwel huu ugonjwa unasambaa kwa kasi africa nadhan robo ya watu sasa hivi wangekuwa washapoteza maisha maana si mchezo kabisa unavyoua...
Unaambiwa hata uchina ilianza hivihivi wengi kupuuzia baada ya wachache kuwa wanaugua siku za mwanzo. Kipindi hicho ndicho wengi hupata maambujizi kabla ya zile dalili kuanza kuonekana.

Zikianza inakuwa kama moto katika nyasi kavu watu wengi kwa wakati mmoja watakuwa wakiugua na namba kupanda kwa kasi.

Muhimu chukua thlahadhari mapema mara zote majuto ni mjukuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
All in all hadi sasa tz wagonjwa 6...

Tukubali tukatae huu ugonjwa kwa africa its not a big deal sema umekuja kutafuta kick tu za bure.

Ingelikuwa kwel huu ugonjwa unasambaa kwa kasi africa nadhan robo ya watu sasa hivi wangekuwa washapoteza maisha maana si mchezo kabisa unavyoua...
Hakika nakuambia (Verily, verily I say onto thee) Africa sio mahali maalum na wala sisi siyo watu maalum.
Kinacho tusaidia hadi sasa ni utamaduni wetu wa kutosalimiana kwa kubusiana (kissing) mashavuni, kukumbatiana (hugging) au kuonesha mahaba kwa wapendanao kwa kubusiana midomo.

Pili ukiachana na mitaa michache kwenye majiji yetu sehemu kubwa watu wanaishi kwenye nyumba zenye nafasi kati ya nyumba moja na nyingine.
Masoko, maduka yetu na sehemu za huduma nyingine ni maeneo ya wazi, wenzetu masoko, maduka, maduka maalum ( supermarkets ) vyote vipo ndani ambako hakuna nafasi na hewa ya kutosha.
Kwao klabu za pombe na bar karibu zote ni za ndani (indoors), hii inachangia sana watu kugombea hewa chache inayozungushwa ndani na mitambo huku tayari ikiwa na virusi.
Tabia yao ya kuogelea kwenye mabwawa (swimming pools), na sauna pamoja ni tatizo.

Bahati nzuri kwetu wanao ugua mpaka sasa ni watu wenye uwezo walio toa ugonjwa ulaya na huku nchini hawaishi uswahilini maeneo yaliyo banana makazi na idadi ya watu.

Kwakweli umaskini wetu na utamaduni wetu tunaonekana hatuja staarabika lakini unatuokoa sana kwenye janga hili.
Tukiendelea kupuuzia na kuamini uzushi kama huu wako tutakuja kujuta kama waispaniola walivyo puuzia wakati Italia wanaanza kutaabika na COVID-19.

Tusipokee raia yeyote hata mtazanzia toka nchi zenye huu ugonjwa hasa nchi za Ulaya, mbona tulikataa kuwarudisha watoto wetu toka China hali ilipokuwa mbaya kule kwao?
 
Sisi bado tunafanya mzaha, kisa hakuna aliekufa mpaka sasa!
Very sad mkuu.
Tukiendelea hivi tutakuja kujuta mbele ya safari lakini haita saidia kurudisha muda nyuma tuweze kurekebisha makosa na kurudisha maisha ya watu watakaopotezwa na hili janga.

Waswahili wanasema majuto ni mjukuu.
 
All in all hadi sasa tz wagonjwa 6...

Tukubali tukatae huu ugonjwa kwa africa its not a big deal sema umekuja kutafuta kick tu za bure.

Ingelikuwa kwel huu ugonjwa unasambaa kwa kasi africa nadhan robo ya watu sasa hivi wangekuwa washapoteza maisha maana si mchezo kabisa unavyoua...
Mkuu,inawezekana hawa virus wakiingia katika mazingira mapya, huchukua muda kujibadilisha ili kukabiliana na mazingirta husika(iwe ni host au mazingira ya nje) na kisha huanza mashambulizi.

Nahisi hivi kwasababu huko kote tunaambiwa ulianza kama mzaha na kuwafanya watu kuupuuza ila baadae unakuwa hatari sana kama tunavyosoma kwenye huu uzi hivyo na sisi tusibweteke kisa hakuna anaekufa bali tuchukue tahadhari zote muhimu.
 
Uganda, kenya, Rwanda na hata Congo wameshachukua hatua serious ila kuna nchi fulani ya Afrika mashariki a.k.a nchi ya asali na maziwa haina serekali![emoji12][emoji12][emoji12]
 
Well said mkuu, ccm wazto Sana kufkr, hawajui korona haichagui mwanasiasa au raia wa kawaida...
Raii yng, augue mwana siasa mmoja Kati ya wale executive aondoke ndo wajue kuwa this z serious tragedy

Sent using Jamii Forums mobile app
Utamu ni kwamba ugonjwa ukishachanganya hata vigogo hakuna kwenda kutibiwa nje![emoji16][emoji16][emoji16]
 
Back
Top Bottom