CORONAVIRUS: Naongeza miluzi ya tahadhari lockdown iharakishwe

Pili joto halizuii kuenea kwa huu ugonjwa maana Italia na Spain hasa hapo Madrid ni jiji lenye joto sio baridi kama China, Korea ya Kusini au nchi zingine zilizokumbwa na hili gonjwa.

Ni kweli. I hope research zinaweza kusaidia. Tehran average centigrade ni nyuzi 17 na Milan ni 20 wakati Addis Ababa ni 19 ila huko wao wamekuwa hit very hard. Joto sio sababu. Watu wanajifariji tu kuwa hiki kirusi hakiwezi kuvumilia joto linalozidi centigrade 24. Dar ni 29-32, Nairobi 26, Entebbe 26
 
Mkuu tuanze na maeneo ya starehe, nyumba za ibada, sherehe za harusi n.k.
Tuzuwie watu toka nchi zilizo athirika na janga hasa za Ulaya.

Tufunge mpaka wetu na nchi jirani zenye COVID-19 turuhusu kusafirisha mizigo tu kati ya nchi zetu.


Yaani mfunge bar kisa corona? Tukanywe wapi sisi😥😥😜😜acheni wehu wenu basi
 
Tunaelekea kwenye mvua kawaida huwa ni low season kwa utalii, vyema tufunge sasa tufungue baada ya mwezi au miezi miwili wakati huo tukiianza high season ya june/july

Few years from now you may wish you should have started today...
 
Cardiovascular disease and diabetes kills more than covid-19

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunaelekea kwenye mvua kawaida huwa ni low season kwa utalii, vyema tufunge sasa tufungue baada ya mwezi au miezi miwili wakati huo tukiianza high season ya june/july

Few years from now you may wish you should have started today...

Nimebarikiwa na signature yako mkuu😊
 
Kwa vile tuna wagonjwa tayari maeneo ya Dar, Arusha , na Zanzibar basi nachukulia madai hayo ya joto zaidi ya nyuzi 24 siyo yenye uzito sana.
Ingawa kitakwimu ni kweli ugonjwa umeshambulia sana maeneo yenye baridi sana.
Uingereza kuna, Urusi na nchi za Scandinavia zina baridi kubwa kuliko baadhi ya maeneo yaliyoshambuliwa sana na ugonjwa kama ya kule Italia.
 
Kwa vile tuna wagonjwa tayari maeneo ya Dar, Arusha , na Zanzibar basi nachukulia madai hayo ya joto zaidi ya nyuzi 24 siyo yenye uzito sana.
90% ya hao wagonjwa ni imported cases. Yaani wameingia Bongo wakati mzee Corona tayari keshazama ndani. All in all, joto sio sababu kwa kuwa South Africa sasa local transmission zimeshaanza maana kuna wagonjwa kibao ambao hawajasafiri kutoka nje ya Nchi.
 
Ni hivi corona iliyopo tz idadi kama ni ndogo hawapungui 200+lakini hawaonekani na wala haionekani kuwa na madhara kivile hivo ww mleta mada usitutie hof acha tuendelee kujitafutia kipato utakapotukuta ni hapo. Ww unalalamika unataka wafunge miji wazuie watu kutembea ili tule nn ss mengine ni kutuogopesha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu tuanze na maeneo ya starehe, nyumba za ibada, sherehe za harusi n.k.
Tuzuwie watu toka nchi zilizo athirika na janga hasa za Ulaya.

Tufunge mpaka wetu na nchi jirani zenye COVID-19 turuhusu kusafirisha mizigo tu kati ya nchi zetu.
Unajua baa na manight clab yameajir watu wangapi ww em tuache jaman tusije kufa kwa stress kabla ya crona

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Rais Magufuli na serikali kwa ujumla. Tunao uhakika kuwa maudhui ya nyuzi hizi yanawafikia.

Mtakuwa na mioyo migumu kuliko ya Farao kama miito hii haiwahusu.

Hadi tufe wangapi ndipo mgutuke?
 

Mawazo duni kabisa. Utakuwa huku soma kilichoandikwa wala kuelewa.
 
Yaani mfunge bar kisa corona? Tukanywe wapi sisi😥😥😜😜acheni wehu wenu basi
Ha ha haaa..
Kwani ukichukua six pack yako, mzinga wa whisk au kreti la bia ukanywea nyumbani haulewi?
Tukizembea utazikosa kabisa hizo kitu, dead people don't drink.
 
Sijamaanisha total lockdown bali baadhi ya huduma au shughuli za mikusanyiko.
Na mipakani kuzuia wageni hasa toka nchi zenye wagonjwa wengi wa COVID-19.
 
Wengi wanalaumu serikali kwann haifungi mipaka, Mara kupiga mikusanyiko ya bar, sokon, na mabasi ya mkoa na daladala.

Swali kwao Kama unajua n hatari hvyo kwann usijikinge wewe kwa kuanza kuepuka mikusanyiko Kama hyo?

Jibu n kuwa wazuie wasizuie huu ugonjwa watanzania wanautafuna kwa ud na uvumba juz kila mtu 80% waliokuwa na viela mfukon walianza kufanya showoff Mara kununua mask, Mara midawa, Mara shopping ya vyakula alafu kesho yake ndo wakwanza kutokunawa mikono, wakwanza kutoa mkono wa kwanza kuhag. N mungu tuu anatulinda Ila watanzania kuishi kwa bajet ya siku tatu tuu n shida Yan hata mtu awe na kilakitu ndan atajitia kiherehere Cha Mara yupo baa, Mara sokon Yan full mzaha
 
Mkuu recommendations ni nini?tufanyeje?
  1. Tufanye lockdown baadi ya maeneo ya mikusanyiko inayowezekana kuzuiwa kwa muda kama majuba ya ibada.
  2. Tuzuie wageni hasa toka nchi zilizo shambuliwa sana na huu ugonjwa.
  3. Tuache ndege na magari ya mizigo tu na ya huduma muhimu za kibinadamu.
  4. Mikahawa na vilabu vya pombe (restaurants and bars) viwe vya kuchukua huduma na kuondoka na bidhaa.
  5. Majumba ya sinema yafungwe.
  6. Kutolewa muongozo wa shughuli za mazishi na mikusanyiko yake, Mfano liwekwe shari watu wakae mbali mbali na wanaobeba jeneza wavae golves, mask, na wawe wachache tu, sehemu kubwa jeneza libebwe na magari.
  7. Zizuiwe sherehe za kijamii kama harusi zinazokusanya watu wengi kumbini, zifanyike viwanja vya nje na watu wakae umbali wa miata 3 au zisitishwe kwa muda.
Unaweza kuongezea, nashauri hii ifanyike angalau majuma matatu tu kwa majaribio, tusisubirie majanga kisha tuje kuwaomba radhi waliotoa tahadhari wakashughulikiwa kama ilivyo tokea China kwa yule Daktari alie toa angalizo kwa umma.
 
Waziri Mkuu Majaliwa linganisha mawazo yako:

Majaliwa awataja wanaoruhusiwa kutoa taarifa kuhusu corona

na maudhui yaliyotolewa kwa unyenyekevu, heshima na taadhima kiasi hiki katika uzi huu.

Tunaamini mamlaka mliyo nayo yanawawajibisha kututendea haki sisi raia wenu.

Pana hatari ya kuja kuanza kulaumiana muda si mrefu kutoka sasa.

Mungu ni mwema janga hili linatukuta wakati tulikuwa na muda wote wa kujifunza toka kwa wenzetu katika kipindi chote kabla ya ugonjwa na hata baada ya ugonjwa kutufikia.

Historia itakuwapo kutuhukumu.

Eeh Mungu wetu utusamehe sisi wakosaji.
 

Kweli serikali hii bado tu haisikii?

Mbona balaa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…