Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe magufuli ameandika:
"Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia."
Inawezekana kashaona dalili za ugonjwa kufika kikomo na anahimiza watu kusali ili ikifika wiki ijayo maambukizi yatakapo pungua, awazodoe wale wanaomkejeli kwamba njia anazotumia za maombi si sahihi.
Katika tweet ya jioni hii, Rais Magufuli ameandika yafuatayo "Ndugu zangu Watanzania, kutokana na ugonjwa wa Corona, nawaomba tutumie siku 3 za kuanzia tarehe 17- 19 Aprili, 2020 {Ijumaa, Jumamosi na Jumapili} KUMUOMBA MWENYEZI MUNGU aliye muweza wa yote atuepushe na janga la ugonjwa huu. Tusali kwa kila mmoja kwa imani yake, atatusikia."