Mimi naomba unifundishe kuhusu sadaka kwa wahitaji(yatima na watumishi wa Mungu - ingawa hawa wanaoitwa watumishi wa Mungu siwaelewi hawa kabisa maana wengi siku hizi wamekua wababaishaji sana)..
Sent using
Jamii Forums mobile app
Ni kweli wengi Ni wababaishaji
Hata katika maandiko Mungu anasema nasi kuhusu Hawa Watumishi wa uongo..
Anasema kwamba tuangalie Kuna wengi watatokea wakitaja Jina lake wakijivisha ngozi ya kondoo Kumbe ndani Ni mbwa mwitu..
Swali:unawajuaje? Unawajua kwa kuwajaribu,si kila roho inatokana na Mungu.. nyingine zatoka kuzimu
Unawajaribuje? Lazima kwanza uwe na uhusiano mzuri na Mungu
Lazima utengeneze na Yesu.
Lazima Roho mtakatifu akae ndani yako,umpe nafasi,umsikilize na ukubali kutenda anayokuelekeza.
Na ili Roho mtakatifu akae ndani yako ni lazima uwe msafi,usome Neno maana Neno ndiyo taa yako.
Lazima uishi maisha matakatifu.. Roho mtakatifu huwa hakai mahali pachafu.
Lazima ukubali kwamba u dhaifu na unahitaji msaada wake sawa na Rum8:26
Unafanikiwaje: Kuna gharama,lazima ukubali kutoa muda wako kwa ajili ya kujifunza Neno,kusali, kufanya mazoezi ya kumkaribisha na kumsikiliza Roho mtakatifu,utulivu wa ndani na nje. Kuna vitu lazima uviache/vikupite ili ujiimarishe kiroho
Wakristo wengi wanashindwa kutambua Watumishi wa kweli ni wapi na waongo ni wapi kwa sababu hawataki kujitesa kwa kusoma Neno,kuomba, kutengeneza na Mungu.
Watu wanapenda vitu vya mkato matokeo yake wengi wanalizwa hovyo.
Mtumishi anayekwambia umpe pesa kwanza ndipo akuombee Huyo si mtumishi wa Mungu, na Kama Ni Wake basi amekengeuka.
Mungu hugawa karama kwa watu wake kadri apendavyo mwenyewe
Anasema mmepewa bure toeni Bure. Anayeponya Ni Mungu na wala si mtumishi.
Watu wasivyopenda kujitesa kusoma maandiko wanajikuta wanapelekwa kokote.
Hawahangaiki kumtafuta Mungu mwenye nguvu ila wanazitafuta tu Nguvu za Mungu.
Neno linasema mtakeni Bwana na Nguvu zake Mtakeni Bwana kwanza.
Sadaka juu ya wahitaji nitakufundisha kesho Mungu akipenda. Nitaomba unitafute sehemu nzuri.. sidhani Kama hapa panafaa sana kwa Mimi kuweza kukufundisha
Barikiwa Sana na karibu.
Sent using
Jamii Forums mobile app