Sasa mradi umedelay for almost a year now, hizo additional cost zipo, zimeangukia wapi kwa serikali au mkandarasi?
Kimsingi nadhani ni ngumu kupata upande wa kubebesha lawama. Ikumbukwe kuwa Yapi hawajawahi kujenga mradi mkubwa kuliko Dar - Makutupora (if I don't mistake). Ukijumlisha hilo na mvua nyingi kupita kiasi na matarajio kuanzia mwaka jana mpaka mwaka huu nadhani hawakuweza ku-cope.
Nadhani ili wasipate hasara pengine hawajataka kufanya panic decision ya kupeleka mradi kwa kasi kubwa kufidia muda uliopotea.
Ikumbukwe pia kuwa hii kampuni ina miradi chungu nzima Ulaya, Asia na Afrika. Simple analysis inatosha kubainisha kuwa huenda kampuni imeyumba/inaenda kwa tahadhari isiyumbe post Covid 19. Mfano: Tukumbuke kilichoipata benki ya Barclays Tz miaka ya 2010. Ilifunga matawi na vituo vingi vya huduma hapa Tz ilhali hasara ilipatikana kwao Uingereza! Najaribu kuwaza tu.
Zaidi ya hapo serikali imekuwa ikisisitiza kuwa haijawahi chelewesha certificate hata moja ya mkandarasi Yapi (34 mpaka sasa kwa mujibu wa PM alipokagua mradi juzi hapo). Hivyo ni ngumu pia kudhani shida iko serikalini.
Kuhusu uagizaji wa treni nadhani serikali imeamua ku-relax kwa kuzingatia kuwa ujenzi wa reli ni dhahili bado. Hivyo huenda hawaoni sababu ya kutumia pesa kulipia ilhali kuna mambo mengine mengi yanayohitaji pesa pia.
All in all (in Baba Levo tone) nashauri tuendelee na Yapi ikiwa tutajiridhisha kuwa wataweza kumudu mradi ujao (assumption ni kuwa DSM itakuwa almost done). Sababu ni kuwa jamaa wamekuwa rafiki sana kwetu hususani kwenye suala la local content.
Kwa mfano. Kwenye HR local content ni 80% lakini tangu mradi uanze ni almost 96%. Huu ndiyo mradi wa kwanza mkubwa tunaona ushiriki mkubwa sana wa local engineers hata kwenye sensitive operations. Naamini technology transfer imekuwa kubwa sana kwenye hii miradi yao miwili.
Tujadili.