Source yake ni huyo mwanaharakati uchwara ambaye ukimpinga kwa fact anakublock [emoji23][emoji23][emoji23]
''Jeshi la ulinzi la wananchi wa Tanzania limesikitishwa mno na taarifa hizo na kwa ujumla ni kwamba hatukutarajia kabisa kwamba jambo hilo lingeweza kuzungumziwa kwasbabu Tanzania haina wanajeshi ambao wamevuka mpaka na kuingia Msumbiji'', alisema bwana Sipe.
''Hadi kufikia sasa tunakalia maeneo yetu ya utendaji ambayo hayahusiani kabisa na operesheni zozote za Msumbiji'', alisema Luteni Sipe.
Kwa jumla ni kwamba utendaji wa jeshi la Tanzania upo katika maeneo yake ya kawaida kabisa katika kutekeleza ulinzi wa mipaka yake na operesheni zake hazihusiani kivyovyote vile na harakati zinazoendelea nchini Msumbiji.