Cost comparison SGR Kenya vs SGR Tanzania

Cost comparison SGR Kenya vs SGR Tanzania

Hapo inapita parallel na iliyopo.. Inaingilia pale Dawasa
Angalia maelezo utaona kuna piers zinajengwa kuelekea Shauri moyo reli ya SGR itapita chini ya hilo Daraja hapo Keko kama MGR!
 



FNGjYBUWQAIEbw8



FNGjYy1X0As_pTA
 

Tril 25/- kujenga SGR Dar-Mwanza-Kigoma

Tril 25/- kujenga SGR Dar-Mwanza-Kigoma

Francisca Emmanuel
09/03/2022
0 Maoni
ZAIDI ya Sh trilioni 25 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kwa vipande vya Dar es Salaam- Kigoma na Dar es Salaam -Mwanza.

Katika ujenzi huo unatumia fedha za ndani pamoja na mikopo mbalimbali kutoka taasisi za fedha, Sh bilioni 600 zimeshatolewa kwa mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha Makutupora hadi Tabora.

Taarifa hiyo ilitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti katika kituo cha Soga mkoani Pwani.

Alisema ujenzi wa reli kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro ulitumia fedha za ndani na mikopo kutoka Denmark na Sweden ambayo ilikuwa na riba ya asilimia tatu. “Mkopo huu ni wa miaka 20 na zaidi na ni mkopo mzuri sana kwani ulitupa fursa ya kufanya majadiliano.

Upembuzi yakinifu kuhusu mradi huu ulifanywa na Serikali ya Awamu ya Nne na serikali nyingine zimeendeleza,” alisema Kadogosa.
Alisema katika mradi huo, hawatategemea mizigo pekee kujiendesha badala yake watashirikisha sekta binafsi kwa ajili ya kuanzisha huduma za kifedha, migahawa na biashara ambazo zitawaongezea mapato.

“Ni lazima reli ijiendeshe kwa kutumia mapato mbalimbali yatakayokusanywa kutoka katika vitega uchumi tulivyoviweka kwenye vituo vyetu vyote vya abiria,” alisema Kadogosa.

Alisema wakikamilisha ujenzi huo kwa kuunganisha maeneo muhimu ya bandari itachukua miaka 15 kupata faida na kwamba wanafanya jitihada mbalimbali kurudisha mzigo mkubwa unaochukuliwa Uganda kuliko nchi zote.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Daniel Sirro alisema serikali imefanya kazi kubwa katika mradi huo wa kilometa 300 na asilimia kubwa (95.3) imekamilika. Alisema reli ni muhimu kwa uchumi na kijamii na ni mradi muhimu kwa maendeleo ya nchi hivyo wanaamini wataishauri vyema serikali katika utendaji kazi.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete alisema Sh trilioni 14.5 zimelipwa kwa mkandarasi na Sh trilioni saba ni za mikataba hivyo wanaamini katika bajeti ijayo itawasaidia kutekeleza miradi kwa wakati ili kutoa huduma bora kwa jamii.

Mwakibete alisema wameagiza mabehewa 44 na vichwa vitatu kwa ajili ya kupeleka mizigo katika Bandari ya Isaka.

Alisema wanatarajia kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa Rwanda, Congo, Burundi na Uganda ili kutumia fursa hiyo.

 
Back
Top Bottom