Kwenye ukweli lazima tuzungumze ukweli.
Mfano hiyo TTCL ilianza kuleta shida 2022 na ndio ishakufa kabisa.
Mwendo kasi ujenzi wa kuelekea Gongo la mboto lile eneo toka mwaka juzi limechimbwa na kuharibiwa ila ujenzi wa kusuasua.
Na hata hii SGR kama hatutatafuta watu makini wa kuiendesha basi inakwenda firisika,maana kama MGR tu route alizozifufua Magufuli zingine zishaanza kufa tena na ufanisi wa MGR umepungua,kama mwaka huu mwanzoni watu wankaa station siku nne treni haijaja kwa ratiba iliyopangwa.
Je hiyo SGR itakuaje aisee.
Bongo sasa hivi ni sawa na BURUNDI in all aspects a truth to be told.
Hiyo ni kuhusu miradi.
Ukija katika maisha ya raia biashara ngumu mzunguko wa pesa mgumu aisee.
Ukijipata ufanye biashara ukiingia katika anga za serikali kuna walafi wanaotaka cha juu laa sivyo biashara zako zitaenda mrama,mimi limenikuta mwaka huu April mtu anadai leseni sehem ambayo kodi/VAT ishakatwa kwa kibali,kisa tu sijammegea pande.
Huduma za kijamii zimerudi kuwa mbovu tena kama 2015 kushuka chini.
Vitu vinapanda panda hovyo tu pasi na kueleweka,gharama za maisha ziko juu bongo,IMAGINE HADI VOCHA IMEPANDA BEI,UKITAKA VOCHA YA 1K UONGEZE 100 TZSH aiseee!!
Tunabishana bure tu ila Tanzania ina hali ngumu kama Burundi tu.