Wapi taarifa za kuaminika, msilete viblog uchwara, nataka taarifa za kuaminika na kukubalika kwamba mlipiga deal ya Wachina chini kwa sababu ilikua ghali. Maana ninachojua ugomvi wenu na Wachina ni kwasababu wao walitaka mfanye single sourcing. Yaani watoe mkopo na wajenge wao, halafu mkandarasi Mchina akapewa kandarasi bila kufuatilia utaratibu.
Lakini hadi sasa sijaona gharama anayotoza Mturuki, hivyo sielewi mnachekacheka nini, maana humo ndani hamjui mahesabu yapi yanayofanywa. Hata wana Lumumba wamejaa humu JF bila taarifa ya kweli, wanatetea bila hata kujua nini wanachotetea.
Sisi reli yetu ipo tayari, umbali wa kilomita 609km, mabehewa, vichwa vya treni, madaraja ya kisasa, vituo vikubwa vilivyojengwa kwa teknolojia ya kisasa... yaani vitu vyote vipo tayari kwa gharama ya $3.8b
Halafu kumbuka yetu pia itaongezwa na kuwa ya umeme.