Mkuu,
ICD ndio hiyo moja hakuna nyingine na ipo ktk kijiji kinaitwa Kwala katika kata ya Kwala, mkoani Pwani.
Ukiwa kwenye Moro highway baada ya daraja la mto Ruvu mbele kidogo kuna mizani ya TANROADS eneo la Kata inayojulikana kama Vigwaza. Hapo ndio barabara mchepuo kuelekea Kwala ICD inapoanza.
Ilipo hio ICD ni karibu na MGR stesheni ya Ruvu na pia ni pembezoni mwa Kwala Marshalling yard ya SGR inayojengwa na Yapi Merkezi.
Geza Ulole" said:
BTW marshalling yard ya Ilala Shaurimoyo inakuwaje? maana hii ICD ya Kwala inamaana itapokea containers moja kwa moja toka Bandarini then stored for few days before being marshalled (SGR and MGR) or trucked for upcountry or regional destinations haulage ili kuondoa mkusanyiko! Je cargo ya TAZARA pia?
Main marshaling yard ya Central line itakuwa ndio hio ambayo Yapi Merkezi wanajenga kwa ajili ya SGR hapo Kwala pembezoni mwa hio ICD.
Hapo la banda la ngozi hapatatumika tena kama yard, treni zitakua zinafanya shunting moja kwa moja toka bandarini hadi Kwala.
Mizigo yote ya container itakuwa haikai bandarini zaidi ya siku 1, itakuwa inabebwa kila saa na treni kuelekea ICD ya Kwala na kuhifadhiwa hapo ikisubiriwa kulipiwa na wenyewe na kupelekwa kwenye destination mbalimbali kwa usafiri wa treni na malarori.
Kuna wafanyabiashara ambao wanazo ICD zao maeneo kadhaa ya Dar, wote wamepewa notice hadi end of June kuhamia Kwala ambapo wamegawiwa maeneo ya kujenga ofisi zao pale.
Kwa hio kwa kifupi kwala ICD area litakua na ICD ya TPA na several ICDs za wafanyabiashara.
Main Marshalling yard ya TAZARA iko Yombo, nadhani kwa TAZARA treni zao zitendelea kwenda bandarini kubeba makonteina.
Simon said:
Wote wawili hata sijawaelewa