Sina details za revenues na matumizi ya TRC ila sidhani TRC wana mapato ya kutosha ya kudeal na tatizo la katikati ya Kilosa na Gulwe.
Kumbuka pale sehemu korofi sio moja na kuna vitu vingi vya kufanya pale. Kuna sehemu za kuhamisha reli, kuna sehemu za kujenga madaraja na kuna sehemu za kujenga mabwawa ya flood control. Gharama ya kuyafanya hayo TRC hawaziwezi hata kiongozi abadilike awe nani.
Sasa shida inakuwa TRC hawapati biashara moja ya sababu ni kutokuwa na uhakika wa huduma, hiyo inasababiisha wanakosa mapato ya maintenance, kukosa maintenace kunafanya huduma kuwa ya mashaka zaidi na hivyo wanakosa wateja zaidi, then wanakosa hela zaidi na cycle inajirudia. Kwa umasikini wa TRC hawana uwezo wa kuhudumia majengo na locomotives kwa ukamilifu kama hata mishahara wanasaidiwa na serikali kuu.
MGR kuwa profitable kunahitaji uwekezaji mkubwa kutoka serikali kuu lakini so far uwekezaji umekuwa wa kusuasua.
Kuna vitu vingine pia vinakuwa against maendeleo ya TRC kama sheria na sera za serikali. Kwa mfano TRC wana maeneo mengi makubwa katikati ya miji. Haya hayahitaji TRC wawe matajiri ila wanaweza kupata private capital wakaendeleza hayo maeneo, ila naamini sheria ilikuwa inawabana. Recently NHC wameweza kuaccess private capital na kupartner na private sector baada ya sheria kubadilishwa ila sijui kama TRC wako covered na hizo sheria mpya.
Then katikati ya Kilosa na Gulwe kulikuwa na mabwawa kadhaa ya flood control yalikuwa chini ya TRC ila serikali iliyahamishia wizara ya maji ambao wana priorities tofauti na wameya-mismanage mpaka yote yamebomoka. Nasikia yanataka kurudishwa TRC ila ni measure ambayo imechelewa sana maana kuyarekebisha sasa ni expensive sana.
Anyway, mambo ni mengi . I just hope SGR will fare better.