Haijapata kutokea the changing guards ya type hii hapa nchini!, yaani ma DGIS 4 wanakuwa hired na fired ndani ya miaka 3! Haijapata kutokea! what is it exactly?
Pigia mstari maneno hayo muhimu uliyoyaandika.
Mamlaka za uteuzi zinafahamu umuhimu wa cheo hicho ?
Je inafaa apigiwe kura ya kuwa na imani naye na chombo gani?
Upandaji cheo chake ndani ya taasisi ulikuwa kupitia utumishi uliotukuka?
Kama ametolewa nje ya taasisi hiyo nyeti je huko alikotoka ataleta uzoefu unaohitajika sana ndani ya TISS
Umri wa mteuliwa nao unangaliwe, je ameteuliwa akiwa amefikia umri wa kustaafu ?
Angalau utumishi katika Polisi na TPDF huangalia wanaochukua ukuu wa majeshi hayo kutoka ndani na wale wa ngazi za juu hivyo hudumu ofisini kwa kipindi kinachotabirika kuweza kuleta mageuzi au kuimarisha taasisi, je kwa mfumo wa TISS hilo halizingatiwi ?
CASE STUDY / 'SHAMBA DARASA'
Uundwaji wa mfumo mpya ndani taasisi nyeti kupitia mkuu wake, mkuu wa majeshi ya ulinzi mstaafu jenerali Mirisho Sarakikya anazungumza :
View: https://m.youtube.com/watch?v=vOfLnZaKHV0
Sandhurst military college 1961 Mirisho Sarakikya, Kashmiri, Alex Nyirenda.....
Askari wa vyeo vya juu jeshi la KRA waliokuwa na nyota ya vitambaa siyo ya vyuma Twalipo, Musuguri
Maofisa vijana wapya Marwa, Mayunga, Kimario, Mwaisongo ...
Kitovu cha maasi kambi ya Kolito Dar es Salaam .... matatizo ya Ngara mwaka 1962, Old Shinyanga Boma, mafunzo Israeli, mkufunzi wa kijeshi Nakuru Kenya, Tabora 1963
January 1964 mutiny maasi ya wanajeshi wa KRA yalitokana na kupunguziwa marupurupu na kudai mishahara iongozwe
1964 Mwalimu Nyerere kwa uchungu sana aomba vikosi vya Uingereza kuja kupokonya silaha kwa waasi mutineers, Mwalimu ikabidi aombe wabaki kwa muda. Nyerere akaomba waingereza wabaki ... baada ya kuwafukuza askari wote walioshiriki maasi hayo. Maofisa hawakyfukuzwa kwa kuwa hawakushiriki.
Mirisho Sarakikya, mwaka 1964 akateuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa mkuu wa majeshi akiwa na umri wa miaka 30 huku akiwa hana jeshi wala askari hata mmoja ....
Ulikuwa mzigo mzito kuunda jeshi upya lakini ndiyo jukumu alilopewa Mirisho Sarakikya ....