Could this be it?....................

...haya sasa! hii nayo ndio nini?

hahaha Mbu yaani nakwambia sie wapendwaji na wapendaji ndo wenye matatizo afu tunasingizia mapenzi.............sasa kama huyu ndoo kafanya nini sasa? Loh inanifanya niamini ule usemi wa kitaani kuwa mwanaume mzuri ni yule aliye-occupied!! Eti wanawake wana tabia ya kupenda mwanaume ambaye tayari ana mwanamke than yule aliye single kabisa......sijui tunaona raha kucompete?! ah
 

FA........hilo ni sahihi kabisa na nadhani ndio maana sisy anashindwa kusema kwa nini alimkatalia hiyo miaka 8 iliyopita. Ingawa nashindwa pia kujua why now atake kukubali? Je penzi huwa linaota kutokana na muda au????
 


Inanikumbusha jamaa mmoja ni rafiki yangu nilikua na kusoma nae. Moja kati ya gia zake kuwaangukia wanawake ilikuwa ni kulia. Yani yeye kulia ni igizo analolipenda na hakukosa alichokitaka kwa kulia na alikiri kuwa anajifanyishaga..

Hivyo basi ukiacha kilio cha jamaa wa hii thread, si vyema kuendeleza uhusiano na mume wa mtu. Mwanajamii1 ungekuwa mtu wa kwanza kumshauri huyo dada yako mpendwa kuwa huyo kaka ana ndoa yake..Hata hivyo bado una nafasi hiyo unless anataka kumuoa dada yako kuwa mke wa pili kama ni wa dini hiyo inayoruhusu.
 

...ah ahha hhaa! hakuna! hata mimi ningelia (uchungu)
huwezi jua jamaa alikuwa amejiandaa kiasi gani siku hiyo (pamoja na kuwa ameoa!)
Mwj1 alishasema jamaa hajawahi pewa nafasi ya u faragha wawili peke yao.

ha ha ha, FA ushawahi kumfanyia mtu nini? ulivyoielezea mnh? ha ha ha!
 

mnh! BJ watu na fani zao...ngoja nianze ku practice hili zoezi siku moja nimtokee mtu! ...LOL
 
Mbu...huku ndani tunayaona/yackia mengi mengi jamani, mie nshakomaa cku hizi.
yaani dada .......acha tu. ndoa ni so complicated na ndio maana siku zote nasema kupenda, uaminifu na respect.....ni vitu ambavyo huwezimsemea mtu. Wewe kama unampenda mtu au u mwaminifu kwake huo ni ukweli unaoujua peke yako na mwenzi wako hawezi katu atauthibitisha na the same kwa mwenzio......so majigambo ya kuwa ....ananipenda kweli... simply because amekununulia gari, amekujengea nyumba au amekulilia haitoshi kukuhakikishia kuwa ni kweli anakupenda.

Natamani wote tujifunze hili.
 
mnh! BJ watu na fani zao...ngoja nianze ku practice hili zoezi siku moja nimtokee mtu! ...LOL
Loh Mbu labda kama utaijaribia kwa wa nje.................sie hapa wote mshatujuza so hatudanganyiki tena!!
 
Reactions: Mbu

unadhani hatujui bac....sema tuna hulka ya kujitoa ufahamu.
 

Kuna ukweli mwingi sana hapo......
 

Mi nina mashaka kama atasikiliza ushauri wako.......labda umuunge mkono.....
 
Acha kabisa hii kitu dada MJI kama mioyo ingekuwa inafunguliwa watu wanasoma yaliyomo watu wengine wangeshauana.


 
Loh Mbu labda kama utaijaribia kwa wa nje.................sie hapa wote mshatujuza so hatudanganyiki tena!!



...mnnnnnnnn?? mwj1 Vibaya hivyo! hujasikia wewe " 'mtoto' akililia wembe mpe?"
 

Nadhani mti wowote utaujua kwa matunda yake..
ni kwa sababu tu wengi wanapokuwa kwenye mapenzi wanakuwa kama vipofu, lakini tabia za watu huwa zinaonekana wazi kabisa.
Pia watu hawataki kutenga muda kujua tabia za mtu anayehisi anampenda.
Nafikiri uaminifu au heshima ni qualities zinazotakiwa kuwa demonstrated kwa nje ili watu wazione, na sio ukae nazo wewe peke yako.
 
Acha kabisa hii kitu dada MJI kama mioyo ingekuwa inafunguliwa watu wanasoma yaliyomo watu wengine wangeshauana.
Chauro hebu tenea mate chini maana kama huwa kuna kubbatani MUNGU alikibofya ili tusiwezeisoma mioyo ya wenzi wetu basi tuombe kisijefyatuka...................yaani ni kweli kabisa kuna wanaolala kitanda kimoja na wenzi wao, wanado na kudo lakini moyoni anajuta na kuombea afe ili awe huru! Jamani chauro hata sijui umewaza nini we binti..............I whish....................
 
Mwanajamii One inawezekana kabisa...hii ya dada kuzaa na mwingine na jamaa kuoa ni ajali tu ya kimapenzi but moyo ya kupenda wacha kabisa,hakuna kushauri hapa ni kukaa nje na kusoma mchezo utaona picha itakavyojibu yenyewe
 
Ni kweli mpendwa ila ninachomaanisha hapa ni kuwa matendo pekee hayadhihirishi upendo au uaminifu...........bali yanakusaidia kukupa tulizo la moyo kwa kuamini kuwa unapendwa na mwenzio ni mwaminifu kwako but ukweli wa hayo unabaki kwa muhusika.

Wapo walioletewa maiti za wenzi wao waliofumaniwa au kufa wakiwa uzinzini na bado wakabisha wakisema hapana alikuwa mwaminifu sana kwangu................
 

Huo ndo ushauri wa maana. Huwezi kumshauri mtu ambaye keshakalishwa chini na kuliliwa akakusikiliza. Labda wewe uwe unaweza kulia zaidi!!

Too late....Hawa jamaa wataamua kama akili zao zitakavyowatuma.
 

Mmh Ikifikia hapo hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…