Van pebles
JF-Expert Member
- Oct 23, 2018
- 2,861
- 5,305
[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]. Tutafanyaje Sasa tutasubiri tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Hamna namna[emoji23][emoji23][emoji23]
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
[emoji4][emoji4][emoji4][emoji4][emoji4]. Tutafanyaje Sasa tutasubiri tu
Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda whatsapp kwenye Group yake.[emoji120] ila picha hakuna
Nenda whatsapp kwenye Group yake.
Picha ya tukio katika situation room ambapo baraza la usalama la us likitazamaDEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?
#6
Nimesema hii kampuni ya Tripple Canopy ambayo Commandos wake siku ile ya April 30 walikuwa wanamlinda Rais Obama inamilikiwa na kampuni mama inayoitwa Constellis Group.
Hawa Constellis Group ni kampuni mama ambayo inamiliki kampuni nyingine kadhaa za masuala ya ulinzi na usalama. Mojawapo ya kampuni hizo nyingine ambazo wanazimiliki inaitwa Academi. Sasa unajua Academi ni akina nani?
Unakumbuka pale mwanzoni nilieleza kuhusu lile tukio la Nisour Square massacre… wale makomando wa kampuni ya BlackWaters Worldwide waliowafyatulia risasi raia wa Iraq mwaka 2007?
Sasa tukio lile lilizua sekeseke la haja kimataifa. Blackwaters wakasakamwa kila mahala.
Ilipofika mwala 2009 wakabadili jina lao kutoka Blackwaters Worldwide na kujiita Xe Services. Baadae mwaka 2011 wakabadili tena jina na kujiita Academi ambalo ndilo jina wanalotumia mpaka sasa.
Kwa hiyo hawa Constellis Group ndio kampuni mama inayomiliki Triple Canopy ambao walipewa jukumu la kumlinda Rais siku ile ya Apeil 30 na pia hao hao Constellis Group ndio wanaomiliki kampuni ya Blackwaters (Academi) ambao huko nyuma niliwaelezea kwa ufupi.
Sasa, kwa nini nimeeleza haya. Kuna kitu adhimu nataka ukione. Vitu viwili actually..
Mosi, 'majority shareholder' yaani mtu mwenye hisa nyingi zaidi kwenye kampuni ya Contellis Group (ambao wanamiliki Triple Canopy na Academi (Blackwaters)) ni kampuni inaitwa Carlyle Group.
Hawa Carlyle Group wenyewe hawajihusishi na masuala ya ulinzi na usalama pekee… hawa wanajihusisha na uwekezaji kwenye kila aina ya biashara unayoijua japo wenyewe wanajieleza kwamba wanafanya masuala ya private equity na altenative asset management na huduma za kifedha.
Jambo la msingi zaidi hapo kuzingatia ni kwamba hawa Carlyle Group kiuhalisia wao ndio wanaomiliki Constellis Group (ambayo ni kampuni mama ya Academi na Triple Canopy) na pia hawa Carlyle Group ndio wanamiliki Booz Allen ambao nilieleza kwamba Wakurugenzi wakuu wote wawili wa Intelijensia ya nchi walitoka huko.
Sinui kama tumeenda sawa hapo… yaani kwa kifupi ni kwamba kampuni binafsi ya kijeshi (Triple Canopy) ambayo ilipewa jukumu la kumlinda Rais siku ya April 30… na kampuni ambayo imetoa Wakurugenzi Wa Intelijensia ya nchi (Booz Allen) zote mzizi wao ni mmoja... Carlyle Group.
Hili jambo la msingi sana kulizingatia. Nimesema nataka kueleza kuhusu masuala yanaitwa "Deep Events".. namna gani yanatokea.
Sasa suala la pili, nimeeleza Triple Canopy wanajihisisha na nini, na nimeeleza Blackwaters wanajihusisha na nini… lakini mpaka muda huu bado sijaeleza Booz Allen wanajihusisha na masuala gani hasa.
Booz Allen ambao Rais Bush alimtoa Mkurugenzi wa Intelijensia toka kwao, na Obama naye mteule wake wa masuala ya Intelijensia ya nchi akamtoa kwao… hawa watu wanafanya nini hasa?
Nianze kueleza kwa swali dogo kabisa.. Naamini mpaka uko humo basi lazima utakuwa unamfahamu shushushu aliyejizolea umaarufu duniani miaka ya hivi karibuni, Edward Snowden. Sivyo?
Hivi huyu shushushu Snowden alikuwa ni nani hasa? Yaani mpaka kipindi kile anaiba zile nyaraka za Idara za Ujasusi za Marekani na kuzivujisha kwa umma, alikuwa ameajiriwa na Idara gani ya Ujasusi?
Jawabu lako ni lipi?
Wafuatiliaji wa mambo watajibu kwamba alikuwa ni afisa wa Idara ya Ujasusi ya NSA.
Na wako wengine watasema CIA..
Vipi nikikwambia kwamba Snowden huyu ambaye kila mtu anamfahamu hakuwa jasusi wa NSA na wala hakuwa jasusi wa CIA.
Ndio alikuwa jasusi, lakini hakuwa mwajiriwa wa idara zote hizo mbili..
Unasemaje?
Ni vigumu mtu kukubali ukimweleza hilo… sababu kwa miaka sita sasa tumekuwa tunasoma habari za kusisimua kuhusu Snowden na mara zote tunafahamishwa kwamba kipindi anatoroka na hatimaye kuvujisha nyaraka, alikuwa ni afisa wa NSA.
Hii ina ukweli nusu… au tuseme ni maelezo ambayo hayajakamilika.
Huko mbeleni nitaeleza kwa undani zaidi.. Edward Snowden ni sahihi kabisa alikuwa ni shushushu.. amewahi kuwa afisa wa CIA lakini kipindi anatoroka na nyaraka nyeti za nchi hakuwa jasusi wa CIA wala NSA.
Yes!
Kipindi Snowden yuko stationed Tokyo Japan kwenye facility za NSA pale Yokota Air Base.. alikuwa pale kama "Contractee" wa kampuni ya Dell ambao walikuwa wanafanya kazi ya kuimarisha mifumo ya Computer ya NSA. Yeye alikuwa pale kama 'Cyberstrategist'.
Mwaka 2013 alipotoroka Marekani, naam alitoroka akitokea kwenye jengo la NSA kule Hawaii… na alikuwa anafanyakazi hapo lakini hakuwa mwajiriwa wao. Snowden alikuwa pale kama Mwajiriwa wa Booz Allen. Ndio, Booz Allen ambao nimekuwa nawaongelea sana kwenye makala hii. Booz Allen walikuwa ni contractors wa NSA na walikuwa na wafanyakazi wao kadhaa kwenye facility za NSA pale Hawaii na mojawapo ya wafanyakazi hao alikuwa ni Edward Snowden.
Inawezekana ni habari mpya nimekupa na inakuacha na maswali mengi zaidi na wasiwasi… tuache hiyo kwa sasa.
Hayo nitaeleza huko mbeleni… turejee kwenye swali… hawa Booz Allen wanafanya nini hasa… na kwa nini mpaka Marais kadhaa wanawachukua mabosi wake na kuwaweka kwenye vitengo nyeti vya serikali kama vile Wakurugenzi wa Intelijensia?
Hapa chini nimeweka picha mbili… picha hizi zimepigwa ndani ya tofauti ya masaa manne tu kati yake.
(Huko whatsApp niliziweka picha hapa.. hapa JF nashindwa kuweka picha hapa katikati ya mada. Nitajitahidi niziweze mwisho wa hii post... I hope zitatokea)
Picha ya kwanza, Rais Obama akiwa kwenye hafla niliyoieleza iliyofanyika April 30 mwaka 2011.
Picha ya pili imepigwa masaa manne baadae akiwa Ikulu kwenye chumba adhimu na cha siro kubwa wanachokiita 'Situation Room'.
Pale mwanzo nilieleza kwamba Rais Obama ilikiwa ni lazima ahudhurie hafla ile ya chakula cha jioni pale hotelini sababu kulikuwa na jambo kubwa zaidi ambalo lilikuwa linaendelea nyuma ya pazia ambapo hafla hii pia ilikuwa inatumika kama 'diversion' kukinga tukio hilo kubwa ambalo lilikuwa linatokea.
Tukio lenyewe ambalo lilikuwa linatokea nyuma ya pazia lilikuwa ni Oparesheni Neptune Spear. Oparesheni ya kuvamia na kumuua Osama Bin Laden huko Pakistan.
Nimeeleza kwa undani wote kuhusu Oparesheni hii katika makala yangu ya "Geranimo".
Hapa nataka utazame picha hii ya pili ya Situation Room kwa makini. Unaona nini?
Bila shaka unamuona Rais Barack Obama, unamuona Makamu wa Rais Joe Biden, Waziri wa Mambo ya Nje Hillary Clinton, hapo mkono wa kulia wa Hillary huyo aliyekaa ni Naibu Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Taifa Bw. Denis McDonough, huyo aliyekaa pembeni ya Obama mwenye sare za jeshi ni Brigedia Jenerali Marshall Webb maarufu kama "Brad" ambaye ni Kamanda Msaidizi wa Kamandi ya Joint Special Operations, huyu aliyekaa mbele ya Hillary ni Robert Gates Waziri wa Ulinzi.
Wale wa nyuma waliosimama pale nyuma ya Obama ni Jemedari Mike Mullen ambaye ni Mwenyekiti wa Joint Chief of Staffs ambaye muda mchache uliopita walikuwa wametoka wote na Obama kwenye ile hafla ya chakula cha jioni.. anayemfuatia ni Tom Donillon ambaye ni msaidizi maalumu wa Rais kwenye mambo ya Ulinzi na Usalama, anayemfuatia ni William Daley ambaye alikuwa ni Katibu Mkuu kiongozi kama alivyo mzee wetu Kijazi hapa nyumbani, huyo nyuma yake ni Tony Blinken ambaye ni mshauri wa masuala ya Usalama kwa Makamu wa Rais Joe Biden, pembeni yake huyo binti mdogo mbichi kabisa ni mwanadada shushushu nguli anaitwa Audrey Tomason ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa masula ya Counterterrorism kwa Baraza la Usalama wa Taifa.
Hapo pembeni yake amesimama jasusi mwingine nguli John Brennan ambaye baadae alikuja kuwa Mkurugenzi wa CIA lakini wakati hii picha inapigwa alikuwa ni mshauri wa Rais wa Masuala ya Usalama wa Ndani ya Nchi na Counterterrorism.
Pembeni yake amesimama James Clapper Mkurugenzi wa Intelijensia ya Taifa ambaye ndiye huyu Obama alimtoa Booz Allen.
Bila shala hiki ndicho unachokiona… kama ni mzoefu watu hawa wote unaweza kuwataja kwa majina toka kichwani.
Hiki ndicho unachokiona, lakini jambo la msingi zaidi katika hii picha ni kile ambacho haukioni…. Yes, itazame picha kwa makini alafu jiulize ni nini haukioni?
Tazama pembeni ya James Clapper (au juu ya Robert Gates)… unaona nini?
Kuna mtu ametokea mkono nusu, amevaa suti nyeusi na tai nyeupe.
Naam, hicho ndicho ambacho haukioni.
Si bahati mbaya mtu huyu kutokea nusu bila sura labda sababu 'frame' ya picha ilikuwa haitoshi kutoa watu wote… hapana, huyo mtu hakuwa anapaswa kuonekana.
Kwa nini nasema hivyo kwa hakika kuwa hakupaswa kuonekana… sababu toka picha hii imewekwa hadharani, kuna waandishi wa habari walioifanyia 'analysis' wakauliza huyu mtu aliyetokea nusu bila sura kuonekana ni nani? Mpaka leo hii unaposoma hapa Whitehouse wamekataa kueleza huyu mtu ni nani na ana cheo gani au alikuwa anafanya nini ndani ya Situation Room.
Sasa, sitaki kusema kwamba nitaeleza huyo mtu ni nani sababu ni Whitehouse pekee wanamfahamu kwa asilimia mia moja huyo mtu ni nani… lakini tunaweza kuunganisha nukta kadhaa na kubashiri huyo mtu ni nani na kwa nini hakutakiwa kuonekana.
Na hapo ndipo kwenye key ya kuelewa hizi 'deep events' ambazo nachambua hapa..
Inaendelea..
Habib "The Bold"
To Infinity and Beyond
Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona Hillary kama anaogopa ?Picha ya tukio katika situation room ambapo baraza la usalama la us likitazamaView attachment 1451353
Sent using Jamii Forums mobile app
Huwez kumpangia km vp lete ww, yaan wabongo shida kweli kila mtu ana ratba zake za kutumia mitandao, nje ya hapa ana majukumu mengne
Asante kwa pichaPicha ya tukio katika situation room ambapo baraza la usalama la us likitazamaView attachment 1451353
Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani huko whatsapp kunalipwa nini? Halafu mbona kama ni siri hivi, yaani ni kama vile mpaka uwe na connection? Si iwekwe wazi tu, wanaotaka waende.Nenda whatsapp kwenye Group yake.
Kwani huko whatsapp kunalipwa nini? Halafu mbona kama ni siri hivi, yaani ni kama vile mpaka uwe na connection? Si iwekwe wazi tu, wanaotaka waende.
Hakuna cha kulipwa zaidi ya ada kila mwezi ukitaka kwenda unamcheck tu mleta mada huwa anaweka namba zake,Kwani huko whatsapp kunalipwa nini? Halafu mbona kama ni siri hivi, yaani ni kama vile mpaka uwe na connection? Si iwekwe wazi tu, wanaotaka waende.