DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?
#11
Naamini Eid yako ilikuwa njema na baraka tele…
Tuendelee.
Mara ya mwisho niliongea kwamba mwaka jana kabla hata ya mlipuko wa ugonjwa huu wa COVID-19 Wizara ya Ulinzi ya Marekani walitoa kazi kwa moja ya Contractors wale anayeitwa Sierra Nevada Corporation kufanya uchunguzi wa mwenendo wa shughuli ambazo zilikuwa zinafanyika pale Wuhan Institute of Virology.
Kampuni ya Sierra Nevada wakatoa jukumu hili kwa moja ya subsidiary yake inayoitwa MACE.
Hii ilikuwa ni mwezi October mwaka jana.
Sasa,
Kwenye uchunguzi huu uliofanywa na MACE uelekeo wa kwanza ambao waliuchukua ilikuwa ni kutazama kitu chaitwa 'Telementry data'. Yaani kwamba kuchunguza taarifa za WIV kwa kutazama transmissions za vifaa pamoja na picha za Satellite za pale Wuhan Institute of Virology.
Katika uchunguzi huu wa MACE ukabainisha masuala kadhaa ambayo yalikuwa ya kutilia shaka na yenye kupaswa kuchunguzwa kwa undani zaidi.
Kwa mfano; MACE waligundua kwamba kuanzia tarehe za mwanzo mwa mwezi October kulianza kuwa na mwenendo ambao haukuwa wa kawaida kwenye kituo cha WIV pamoja na maeneo ambayo yanaizunguka.
Mfano tazama hii picha hapa chini..
Kama ambavyo nimeeleza pale juu kwamba njia kuu ya kwanza amabyo MACE ni kuchambua 'telemetry data'. Kwa maana ya kwamba kupima transmissions za vifaa mahususi vilivyopo eneo la Wuhan Institute of Virology.
Sasa hii picha hapa chini inaonyesha uwepo wa vifaa vya kieletroniki vyenye kufanya kazi mahala hapo. Kwa maana ya mitambo/mashine za maabara, taa, magari, simu za mkononi n.k.