COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

Poleni niliwahi kujiunga huko mwisho wa mwezi ndio anakuwa active kweli kudai michango mkishamchangia anaanza kuwaringia kana kwamba anafanya msaada! Halafu dizain anapenda kubembelezwa
Tuwaombe Mods wampige ban ya maisha,maana amefanya JF ni sehemu ya kutafutia wateja kujiunga na group lake la whatsap.
 
kitu kibaya mtu kukukatisha utamu. Mimi nitakuwa sifuatilii story zako Habibu kwa maana najua hautomalizia km nyingine nyingi za nyuma
 
Wakuu huyu jamaa asituzoee vibaya. Tuangalie namna yakuumaliza wenyewe huu uzi
 
Wakuu, naona nashindwa kuweka picha katikati ya Post kama ambavyo nataka.

So, nitafanya jambo moja.

Nitapost sehemu ya 11 kwa vipande vipande (yaani kila kipande kitakuwa ni post inayojitegemea).

Kwa hiyo naomba baada ya post hii usipost kitu hapo chini maana utavuruga mtiririko.
Mpaka ukiona nimeandika neno "ITAENDELEA.." hapo waweza kuendelea kucomment.

Naanza kupost. Usicomment tafadhali mpaka nimalize.
 
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?





#11




Naamini Eid yako ilikuwa njema na baraka tele…

Tuendelee.


Mara ya mwisho niliongea kwamba mwaka jana kabla hata ya mlipuko wa ugonjwa huu wa COVID-19 Wizara ya Ulinzi ya Marekani walitoa kazi kwa moja ya Contractors wale anayeitwa Sierra Nevada Corporation kufanya uchunguzi wa mwenendo wa shughuli ambazo zilikuwa zinafanyika pale Wuhan Institute of Virology.
Kampuni ya Sierra Nevada wakatoa jukumu hili kwa moja ya subsidiary yake inayoitwa MACE.
Hii ilikuwa ni mwezi October mwaka jana.


Sasa,


Kwenye uchunguzi huu uliofanywa na MACE uelekeo wa kwanza ambao waliuchukua ilikuwa ni kutazama kitu chaitwa 'Telementry data'. Yaani kwamba kuchunguza taarifa za WIV kwa kutazama transmissions za vifaa pamoja na picha za Satellite za pale Wuhan Institute of Virology.

Katika uchunguzi huu wa MACE ukabainisha masuala kadhaa ambayo yalikuwa ya kutilia shaka na yenye kupaswa kuchunguzwa kwa undani zaidi.

Kwa mfano; MACE waligundua kwamba kuanzia tarehe za mwanzo mwa mwezi October kulianza kuwa na mwenendo ambao haukuwa wa kawaida kwenye kituo cha WIV pamoja na maeneo ambayo yanaizunguka.

Mfano tazama hii picha hapa chini..

Kama ambavyo nimeeleza pale juu kwamba njia kuu ya kwanza amabyo MACE ni kuchambua 'telemetry data'. Kwa maana ya kwamba kupima transmissions za vifaa mahususi vilivyopo eneo la Wuhan Institute of Virology.
Sasa hii picha hapa chini inaonyesha uwepo wa vifaa vya kieletroniki vyenye kufanya kazi mahala hapo. Kwa maana ya mitambo/mashine za maabara, taa, magari, simu za mkononi n.k.
20200525_153635.jpeg
 
Ukitazama kipande cha juu cha cha hii picha ina tofauti kubwa na kipande cha pili cha picha.

Kipande cha juu kinaonyesha 'flow' ya kawaida ya vifaa kwenye eneo la WIV. Kipindi hiki ni cha miezi kadhaa kabla ya mwezi wa kumi mwaka jana (kuanzia July 2019).
Flow nzuri kabisa ya vifaa inaonekana kwenye eneo la WIV. Mashine na mitambo ndani ya kituo inawashwa, kuna simu za mikononi (uwepo wa watu), magari yanaingia na kutoka n.k.

Ukutazama kipande cha chini unaona ni giza tupu. Hakuna 'flow' yoyote kama mwanzo ya uwepo wa 'devices' au vifaa kuwashwa na kutumika.
Hiki ni kipindi cha tarehe za mwanzo kabisa za mwezi wa kumi.

Hii inazua swali la msingi zaidi kwamba ni kwa nini hakukuwa na uwepo wowote wa devices kwenye eneo la WIV.?

Ili kujibu swali hili, MACE wakaanza kuchambua picha za satellite za eneo la WIV kwenye kipindi hiki ambacho kinaonyesha hakukuwa na flow yoyote ya vifaa kwenye eneo la Wuhan Institute of Virology.

Swali likawa kwa nini data walizonazo zinawaonyesha kwamba hakukuwa na flow ya devices kwenye eneo la WIV mwanzoni mwa mwezi October.

Picha za satelline (nimeweka hapa chini) zikajibu kwa sehemu kwa nini hakukuwa na uwepo wa Devices maeneo ya WIV mwanzoni mwa mwezi Octoba.

Note: hizi picha ambazo zimeziweka hapa chini zimechukuliwa toka kwenye 'commercial satellites'. Kwa hiyo nembo ambata utaziona ziko tofauti kwa kila picha. Kama waelewa ufasiri wa picha za satellite…
 
Back
Top Bottom