Picha hii inaonyesha flow ya mawasiliano ya simu kati ya Oct 25 mpaka Dec 1 mwaka jana 2019.
Tafasiri ya data hii ni kwamba, katika kipindi hiki inaonekana kuna uwepo wa watu ulirejea kwenye kituo cha WIV.
Utaona kuna mahala kuna dot kama tatu hivi ziko pamoja.
DOD walipofuatilia data za simu kwenye hizi dot wakagundua kwamba… dot moja data zake zinashabihiana na dot moja ambayo ilikuwa inaonekana kipindi cha August mpaka mwanzoni mwa October (eneo la walinzi). Lakini dot nyingine mbili zilizosalia hazishabihiani na data nyingine zozote za simu ambazo wamewahi kuziona kwenye eneo la WIV kwa muda wa mwaka mzima huo wa 2019.
Hii ina maana tatu muhimu sana.
Maana ya kwanza ni dhahiri kwamba hawa walikuwa ni walinzi. Lakini maafisa hawa wa ulinzi walikuwa wamebadilishwa isipokuwa watu wachache tu (mmoja au wawili). Kwamba serikali ilikuwa imepeleka maafisa wapya kulinda eneo la WIV na kuondoa wale walinzi wa awali isipokua afisa mmoja tu au wawili. Tutaongea zaidi kuhusu hii baadae.
Maana ya pili ni kwamba sehemu ya ukaguzi kabla ya watu kuingia ndani ya kituo cha WIV ilikuwa imehamishwa kutoka pale tulipopaona mara ya kwanza (kwenye mstari wa njano) na sasa imeingizwa ndani zaidi. Kuna uwezekano mkubwa walifanya hivi baada ya kuweka kizuizi kile barabarani.
Maana ya tatu ni kwamba, security perimeter ilikuwa imefanywa ndogo zaidi. Kwa nini, sababu pekee yenye mashiko ya wao kupunguza mzingo wa ulinzi ni kwamba 'focus' yao yote walikuwa wameielekeza kwenye jengo lenye maabara ya BSL-4. Lile jengo ambalo nililizungushia duara jana kwenye picha.
Naam, hizi teknikaliti za ulinzi nitaja kuzichambua zaidi kwa undani mbele kidogo.
Sasa hebu elekeza macho kwenye picha hii ya tatu na haswa nataka utazama hii dot moja ambayo imejitenga peke yake pale chini.
Nilisema kwamba eneo hili la WIV lina majengo kadhaa na kwenye majengo hayo yote ni jengo moja tu ambalo ndani yake lina maabara ya BSL-4.
Sasa mahala ambapo dot hii ipo ni hapo kwenye hii maabara ya BSL-4.
Maana yake ni kwamba baada ya eneo hili la kituo cha kisayansi cha WIV kufungwa ghafla kuanzia october kwa sababu ambazo mpaka sasa hatuzijui (of course baadae tutaona ushahidi/viashiria ni sababu zipi) lakini baadae, baada ya watu wote kuwa evecuated kuna mtu mmoja maalumu alipewa access ya hili eneo.
Ni nani huyu? Alikuwa anafanya nini?
Nimeelez kwamba katika hatua hii MACE walikuwa wanadukua 'cellphone data'.
Hivyo wakafanikiwa kuing'amua namba za utambulisho za simu hii.
Ukisoma kwenye ripoti ya MACE ambayo wamei-submitt DOD eneo la namba za utambulisho wa simu hii zimefichwa (reducted) kwa sababu zilizo wazi kabisa, hawawezi kuiweka hadharani.
Lakini hilo sio suala muhimu sana, suala muhimu na la kusisumua mi 'Pattern-of-Life Analysis' ambayo waliifanya ya mtumiaji wa simu hii.
Kuna mambo ya kusisimua hasa na kustaajabisha…
MACE wakafuatilia mwenendo wa 'Device' hii kwa kipindi cha mwaka mzima, na haya ndiyo ambayo walikutana nayo.
Tarehe 26 January mpaka tarehe 25 February mtumiaji wa device hii ilionekana kwamba alikuwa nchini Kenya kwa muda wa mwezi mzima. Naam, Kenya hapa hapa 'nyumbani'.
(Aambapo Tarehe 11 January mtumiaji wa Device hii alisafiri kwenda Dubai na kisha kurejea tena Kenya).
Tarehe 3 March mpaka Tarehe 28 June mtumiaji wa Device hii alikuwa mji mkuu wa nchi ya China, Beijing kwa kipindi cha miezi minne hiyo yote.
Tarehe 28 June mtumiaji wa device hii alikuwa mjini Wuhan, China.
Tarehe 21 mpaka Tarehe 25 August mtumiaji wa Device hii alikuja tena Kenya kabla ya Tarehe 28 kuelekea Dubai.
Baada ya hapo hakukuwahi kuwa a data nyingine yeyote ya Device hii (device hii iliacha kutumika) mpaka ilipokuja kuibuka tena mwishoni mwa october hapo eneo la Wuhan Institute of Virology.
Kuna nini unakiona hapo? Think… kuna jambo la wazi kabisa unaling'amua ukitazama mtiririko wa hizi safari na hatimaye kuja kuibukia WIV kipindi wafanyakazi wote wa hapo wakiwa wameondolowa kwa dharura.