COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

COVID-19 & DEEP STATE: Nini maana ya Uhandisi Jamii unaotokea Duniani!?

Jamani SAA nane ilikuwa ahadi ya kushushiwa kipande cha 15 vip
 
Mkuu nasubiri sehemu ya 15 tangu saa nane mchana, kwema lakini?
 
Bwana safi nilikuwa na kazi kazi imenibana nikawahi hapa nikijua Tatar mapilau yako mezani dah! Nakuta kumenuna hapa nipo Niko bored
 
Da kila nikiunga dots kunatokea hitilafu kwenye viungio dots zinajipangua
 
Kesho jalali akupe kheri upate muda utuwekee chakula ya ubongo Habibu A.Hanga
Screenshot_2020-03-21-15-07-01-1.jpeg
 
Nilishasema kwamba mm n binadamu kama nyinyi pia ninakuwa na majukumu mengine ya kikazi na kifamilia, na kunawakati nakua nje ya mudi au kuumwa pia, Naomba msinichukilie tofauti labda kama nadharau au la ....... Samahanini kwa kuwakwaza lkn nitarejea apa soon.
 
DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?





#15



Nilikuwa napitia kabrasha za miaka ya zamani kidogo… kuna ripoti nikakutana nayo ambavyo ilikuwa na kitu fulani interesting nikaona si vibaya nikiwashirikisha. Ripoti hii imetolewa siku ya kwanza ya mwaka 2000 (January 1, 2000). Ripoti hii imeandaliwa na shirika la Ujasusi la Marekani CIA ikiwa na kichwa cha habari "The Global Infectious Disease Threat and Its Implications for the United States".
Ripoti hii imetolewa na ofisi ya Mkurugenzi wa Intelijensia ya Marekani lakini kimsingi imeandaliwa na shirika la CIA.
Unaweza kuipitia nimeiweka hapo chini lakini nitatoa kwa ufupi 'point' ya msingi sana kwenye taarifa hii niliyoipata baada ya kuisoma.

Suala la kuvutia kuhusu ripoti hii yote ukiisoma ni vile ambavyo CIA wanatabiri kwa muda wa miaka 20 ijayo kutakuwa na mrudio wa mara kwa mara wa kutokea ugonjwa mpya (au uleule ukijirudia kwa namna tofauti) ambao utateteresha hali ya ulinzi na usalama nchini Marekani na Duniani kwa ujumla.

“…new and reemerging infectious diseases will pose a rising global health threat and will complicate U.S. and global security over the next 20 years.”

Miezi miwili baadae Dr. Anthony Fauci (naam, huyu huyu Dr. Fauci ambaye tumekuwa tukimuoma pembeni ya Trump mara zote akiwa anatoa 'update' kuhusu hali ya maambukizi ya Covid-19), huyu Dr. Fauci alichapisha andiko lenye kichwa cha habari "Clinical Infectious Diseases" ambamo kwenye andiko hilo ukilisoma mkazo mkubwa anauweka kwenye kutabiri kutokea tena kwa 'strain' mpya ya virusi vyenye kufanana na kirusi cha H5N1 ambacho kiliteteresha dunia mwaka 1997 na 1998.


Kuna stadi inaitwa 'Pattern Recognition' ambayo chimbuko lake ni kwenye masuala ya statistical data lakini stadi hii iko mpaka kwenye Uhandisi na hata kwenye saikolojia.
Kuna masuala kadhaa ambayo yalitokea mwaka 1997, 1998 na 2003 ambayo kwa msingi yao idara za Intelijensia za Marekani wakaamua hata kuwatuma MACE kufanya huu uchunguzi ambao tumekuwa tunaujadili hapa.

Chanzo cha 'pattern' ya hiki kilichotokea mwaka huu kuhusu Covid-19 CIA waliibashiri miaka 20 iliyopita kwenye ripoti yao ambayo nimewawekea hapo chini pamoja na andiko la Dr. Fauci.
Tutarejea hapo…


Kwanza niwarejeshe kwenye lile swali ambalo sikulitolea jawabu kuhusu ile Device ambayo ilaonekana nchini Kenya, Dubai, Beijing na kisha kupotea na kuja kuibuka tena Wuhan mwaka jana mwezi wa kumi.


Sasa,

Nchi ya China wana programu ya kitaaluma wanaiita "Thousand Talents Program".
Wenyewe wanaipambanua programu hii kama mkakati wa kuchochea bunifu na vumbuzi za kisayansi duniani kwa kutengeneza mazingira wezeshi kwa watafiti wa kisayansi.
Yani tuseme kwa mfano… moja ya watafiti magwiji wa kisayansi ndani ya nchi yetu ambao binafsi ninaowajua ni Profesa Benezet Mutaboya wa chuo kikuu cha Sokoine (SUA) Morogoro ambaye ni kati ya wanasayansi wa daraja la kwanza kabisa kuutambulisha ulimwengu kwenye masuala ya 'Wildlife Forensics'. Nakumbuka mwaka 2014 chapisho lake la "The use of DNA tools in Wildlife Forensics" lilishinda tuzo ya kimataifa ya National Geographic (Buffet Award).


Sasa,

Mtafiti adhimu kama huyu wachina wakimuona wanamchukua chini ya hiyo Progamu yao ya "Thousand Talents".
Unaulizwa profesa unataka nini? Unawandikia proposal unawaeleza unachotaka, utawaambia labda wataka kutengeneza maabara yako binafsi, wataka uwe na uwezo wa kulipa posho wasaidizi wako wa maabara, labda pia wataka kusafiri sehemu tofauti za duniani kufuatilia masuala kadha kuhusu tafiti zako… na kadhalika, na kadhalika.
Bila hiyana, wanakukatia 'kibunda' uweze kufanya hayo unayoyasema.

Kwenye miaka ya hivi karibuni hii "Thousand Talents" imeibuka kuwa moja ya vinara wa kumwaga fedha kwa wanasayansi wa watafiti duniani.View attachment infectiousdiseases_2000.pdf
 
Ndio hivyo kusema kama ambavyo wanajipambanua kwamba wanasaidia kutengeza mazingira wezeshi kwa wavumbuzi na watafiti wa kisayansi. Lakini sharti kuu la kupata fedha zao ni moja tu kwamba unapaswa 'ku-share' nao findings utakazozipata kwenye tafiti zako. Na hata 'paper' yako itachapwa kwa jina lako lakini chini yao wao Thousand Talents.

Programu hii ya Uchina imezoa wanasayansi wengi manguli kutoka kila pembe ya dunia. Tena wengine wengi wanapelekwa china kabisa kuishi huko na kupatiwa kila aina ya uwezeshaji wanaohitaji ili wafanye kazi zao kwenye mazingira rafiki.

Ni jambo zuri na jema kabisa… si ndivyo?

Ndio… katika jicho la kawaida ni jambo jema sana. Lakini kwa nchi ya Marekani wamepiga marufuku wanasayansi ndani ya nchi yao kushiriki au kupokea ufadhili kutoka kwenye hii programu ya "Thousand Talents".!

Kwa nini?

Vyombo vya usalama vya Marekani pamoja na Bunge la Seneti (Kamati ya Seneti ya Intelijensia) wanaamini kwamba Programu hii ni mwamvuli wa kishushu wa nchi ya China kuiba teknolojia za kisayansi toka kila kona ya Dunia na hasa kuiba toka nchi za magharibi. Na ni kwa sababu hiyo Vyombo vya usalama vya Marekani wameweka sharti kwamba kwa watafiti na wanasayansi wake wote kama wakitafutwa na hawa "Thousand Talents" kwamba wanatakukukupa ufadhili basi wapaswa kuripoti kwa vyombo husika vya usalama.


Sasa tuje hapa juzi mwaka huu 2020 mwezi wa pili pale Marekani kulikuwa na jambo la kusisimua sana ambalo linashabihiana na hii Device ninayoisema kwenye sehemu zilizopita.
Suala ambalo eidha kwa makusudi au bahati mbaya (nitaeleza kwenye makala ya Deep State) sijaona likiripotiwa kwa uzito kwenye vyombo vya habari.

Ni kwamba,
Kwa muongo (decade) wa mwaka 2000 mpaka mwaka 2010 ulimwengu ulimtunuku Profesa Charles Lieber kutoka Marekani kama Mkemia bora wa muongo.
Kwenye ulimwengu wa sayansi, Profesa Lieber anahesabika kama ni "kichwa" bora cha kemia tulichonacho kwa wakati wetu huu na kizazi chetu.
Profesa Lieber amebobea kwenye masuala ya 'Nanoscience' pamoja na 'Nanotechnology' na yeye ndiye anayeongoza kwa kufanya gunduzi na kuifanya sekta ya Nanoscience kuwa hivyo ilivyo sasa.
Kwa sasa Profesa Lieber ni Muhadhiri kwenye chuo kikuu cha Harvard nchini Marekani.

Kuna mahala nilisema kwamba unapoona watu kama akina Trump licha ya 'ukichaa' wake anasema kwamba hili suala la Covid-19 lina makandokando mengi nyuma yake unapaswa kukuna kichwa badala ya ku-dismiss kwamba huyu bwana ni kichaa.
Unapoona mashushushu wabobezi kama akina Michael Pompeo wanaonyesha wasiwasi kuhusu uhalisia wa Covid-19 unapaswa kuvuta pumzi na kutafakari.
Unapoona moja ya watu muhimu zaidi wa kizazi chetu kama Elon Musk anang'aka kwamba dunia inapigwa 'mchanga wa macho' kuhusu Covid-19 wapaswa nawe uchukue japo dakika mbili kuwaza na kuwazua.

Nimekumbushia suala hilo sababu kuna jambo kubwa sana pale Marekani lilitokea mwanzoni mwa mwaka huu lakini hakuna chombo cha habari kikubwa walio valia njuga kuliripoti.

Ni kwamba,

Baada ya mlipuko wa maambukizi ya ovid-19 kushika kasi pale Marekani na vifo vikiripotiwa kwa maelfu vyombo vya usalama vya marekani nao wakaongeza kasi wa kuchunguza wasiwasi ambao walikuwa nao siku nyingi kuhusu watu fulani.
Uchunguzi wao huu ukapelekea kukamatwa kwa Wanasayansi watatu wakubwa ndani ya Marekani.
Wa kwanza ni Profesa Zaosong Zheng Mtafiti na Muhadhiri wa chuo kikuu cha Harvard.
Wa pili ni Dr. Yanging Ye Muhadhiri na nguli wa Biomedical Engineering toka chuo kikuu cha Boston.
Na wa tatu ni huyo nguli ambaye nimemueleza pale juu, Peofesa Charles Lieber Mkemia na Mtafiri toka chuo kikuu cha Harvard.

Jambo la kusisimua zaidi ni kwamba kila mmoja ya hawa wanasayansi alikamatwa kwa sababu zake tofauti… lakini kiko kitu kimoja ambacho kinawaunganisha wote hawa watatu.
Wote watatu walikuwa kwa siri kubwa walikuwa wanapokea ufadhili kutoka "Thousand Talents Program" ya China ambayo wanasayasi wa Marekani hawaruhusiwi kupokea ufadhili au hata kushiriki kwa namna yoyote kwenye programu hiyo.
Fahamu kwamba japo wao kupokea kwa siri ufadhili toka "Thousand Talents" ni kosa, lakini hiyo haikuwa sababu kuu au sababu ya awali wao kukamatwa.
Sababu kuu iliyopelekea FBI kuvamia nyumba zao na kuwakata ilikuwa ni kile ambacho walolikuwa wanakifanya maabara na gunduzi za kisayansi ambazo walikuwa wamezituma China.
 
Back
Top Bottom