DEEP STATE, COVID-19: Nini Maana ya Uhandisi Jaamii Unaotokea Duniani?
#15
Nilikuwa napitia kabrasha za miaka ya zamani kidogo… kuna ripoti nikakutana nayo ambavyo ilikuwa na kitu fulani interesting nikaona si vibaya nikiwashirikisha. Ripoti hii imetolewa siku ya kwanza ya mwaka 2000 (January 1, 2000). Ripoti hii imeandaliwa na shirika la Ujasusi la Marekani CIA ikiwa na kichwa cha habari "The Global Infectious Disease Threat and Its Implications for the United States".
Ripoti hii imetolewa na ofisi ya Mkurugenzi wa Intelijensia ya Marekani lakini kimsingi imeandaliwa na shirika la CIA.
Unaweza kuipitia nimeiweka hapo chini lakini nitatoa kwa ufupi 'point' ya msingi sana kwenye taarifa hii niliyoipata baada ya kuisoma.
Suala la kuvutia kuhusu ripoti hii yote ukiisoma ni vile ambavyo CIA wanatabiri kwa muda wa miaka 20 ijayo kutakuwa na mrudio wa mara kwa mara wa kutokea ugonjwa mpya (au uleule ukijirudia kwa namna tofauti) ambao utateteresha hali ya ulinzi na usalama nchini Marekani na Duniani kwa ujumla.
“…new and reemerging infectious diseases will pose a rising global health threat and will complicate U.S. and global security over the next 20 years.”
Miezi miwili baadae Dr. Anthony Fauci (naam, huyu huyu Dr. Fauci ambaye tumekuwa tukimuoma pembeni ya Trump mara zote akiwa anatoa 'update' kuhusu hali ya maambukizi ya Covid-19), huyu Dr. Fauci alichapisha andiko lenye kichwa cha habari "Clinical Infectious Diseases" ambamo kwenye andiko hilo ukilisoma mkazo mkubwa anauweka kwenye kutabiri kutokea tena kwa 'strain' mpya ya virusi vyenye kufanana na kirusi cha H5N1 ambacho kiliteteresha dunia mwaka 1997 na 1998.
Kuna stadi inaitwa 'Pattern Recognition' ambayo chimbuko lake ni kwenye masuala ya statistical data lakini stadi hii iko mpaka kwenye Uhandisi na hata kwenye saikolojia.
Kuna masuala kadhaa ambayo yalitokea mwaka 1997, 1998 na 2003 ambayo kwa msingi yao idara za Intelijensia za Marekani wakaamua hata kuwatuma MACE kufanya huu uchunguzi ambao tumekuwa tunaujadili hapa.
Chanzo cha 'pattern' ya hiki kilichotokea mwaka huu kuhusu Covid-19 CIA waliibashiri miaka 20 iliyopita kwenye ripoti yao ambayo nimewawekea hapo chini pamoja na andiko la Dr. Fauci.
Tutarejea hapo…
Kwanza niwarejeshe kwenye lile swali ambalo sikulitolea jawabu kuhusu ile Device ambayo ilaonekana nchini Kenya, Dubai, Beijing na kisha kupotea na kuja kuibuka tena Wuhan mwaka jana mwezi wa kumi.
Sasa,
Nchi ya China wana programu ya kitaaluma wanaiita "Thousand Talents Program".
Wenyewe wanaipambanua programu hii kama mkakati wa kuchochea bunifu na vumbuzi za kisayansi duniani kwa kutengeneza mazingira wezeshi kwa watafiti wa kisayansi.
Yani tuseme kwa mfano… moja ya watafiti magwiji wa kisayansi ndani ya nchi yetu ambao binafsi ninaowajua ni Profesa Benezet Mutaboya wa chuo kikuu cha Sokoine (SUA) Morogoro ambaye ni kati ya wanasayansi wa daraja la kwanza kabisa kuutambulisha ulimwengu kwenye masuala ya 'Wildlife Forensics'. Nakumbuka mwaka 2014 chapisho lake la "The use of DNA tools in Wildlife Forensics" lilishinda tuzo ya kimataifa ya National Geographic (Buffet Award).
Sasa,
Mtafiti adhimu kama huyu wachina wakimuona wanamchukua chini ya hiyo Progamu yao ya "Thousand Talents".
Unaulizwa profesa unataka nini? Unawandikia proposal unawaeleza unachotaka, utawaambia labda wataka kutengeneza maabara yako binafsi, wataka uwe na uwezo wa kulipa posho wasaidizi wako wa maabara, labda pia wataka kusafiri sehemu tofauti za duniani kufuatilia masuala kadha kuhusu tafiti zako… na kadhalika, na kadhalika.
Bila hiyana, wanakukatia 'kibunda' uweze kufanya hayo unayoyasema.
Kwenye miaka ya hivi karibuni hii "Thousand Talents" imeibuka kuwa moja ya vinara wa kumwaga fedha kwa wanasayansi wa watafiti duniani.
View attachment infectiousdiseases_2000.pdf