Kwa nini watupatie bure? Ukiona mtu anakupatia bure ufahamu gharama yake ni kubwa. Vitu vya bure vilikwisha, sisi sio shemeji zao? Mbona wao wanajikopesha bila kuwa na simile, lakini sisi kujikopesha ni mwiko na nongwa. Hiyo Exchange Rate Mechanism (ERM) ndiyo inayomaliza mataifa ya Africa. Hata ile gold standard waliposhindwa kuihimili walibadilisha magoli.
Yes wanatupa bure kwasababu sisi nchi masikini ni tatizo kwao. Mfano, kirusi cha China kimebadilisha maisha ya watu dunia kijamii, kiuchumi , kisiasa n.k. na kupelekea vifo vingi.
Juzi kulikuwa na mjadala nikilisiliza katika radio yangu ya zamani kidogo.
Wataalam wanasema huwezi kufanya control sehemu moja ya dunia ukabaki salama
kwa mfano wakifanya vaccination kwa watu wao kuna uwezekana mutation ikatoa new strain ambayo haitadhibitiwa na chanjo. Tatizo litaanza upya na kuwaathiri wao.
Njia rahisi ni kuhakikisha wanasaidia nchi masikini wakijua wazi hicho ndicho kikwazo kikubwa
Lakini Watanzania tumekuwa wajinga wa kushindwa kutumia logic.
Hivi unawezaje kusema hutaki bure ya Corona Virus vaccine wakati unapokea Bure ya ARV ?
Hivi unawezaje kusema hutaki bure ya Corona virus vaccine wakati unatumia vaccines za bure kutoka Gavi zinazolipiwa na nchi hizo za magharibu?
Kila siku watoto wa Tanzania wanapata chanjo za Bure kutoka nchi za magharibi.
Hivi kama nia ni mbaya hapa si ndipo pakumaliza kabisa kizazi! teh te teh
kila siku watu wanasaini misaada ya bure, lakini leo hawataki vaccine za bure za Corona! teh teh teh
Rais Obama alipoingilia kati kuhusu Ebola watu waliuliza kwanini.
Jibu lilikuwa rahisi hi '' dunia ni kijiji' siku hizi hili litakuwa tatizo la dunia.
Aliwahi na kufanikiwa. Trump kama Bosenero wa Brazili wakajaribu Ujinga kwa gharama za watu wao.
Eti unahoji kwanini wanatoa msaada wa Corona bure , huhoji kwanini Balozi wa nchi moja aje kusimamia uchimbaji wa vyoo katika sekondari, tena DC anakwenda kumshukuru. Hujui hilo! teh teh teh
Huo utaratibu wa certification unafanywa na Serikali ambayo ndio ina mamlaka, sio kuamuliwa na mtu anayekaa NY akifikiria anaweza kutuamulia mambo yetu. Zama za utumwa zilipendwa, Tanzania is not a colony.
NB Tanzania sio masikini.
Ni hivi utaratibu ni wa nchi kuziomba mamlaka zake zipatiwe sample na kufanya analysis.
Hakuna certification ya NY.
Sisi ndio tunahitaji vaccine na tunawajibu wa kupata sample na kuzifanyia analysis.
Pfizer, Modena , Johnson n Johnson na AstraZeneca hawana shida na sisi na wala hawatuhitaji, tunawahitaji
Muhimu uelewe utaratibu wa registration za dawa. Nchi zote dunia zina utaratibu wake equally nasi tuna wetu na hivyo wajibu wa kuomba sample , Literature na Proof ni wa Tanzania inayotaka vaccine si US.
Kitu kimoja unapaswa kujiuliza.
Je, hapa Tanzania tuna hata mashine inayoweza kufanya gene sequencing?
Je, tuna mashine na utaalam wa kuweza ku ''isolate virus protein'' , kufanya analysis ya ingredients za vaccine?
Kumbuka mashine zote za analysis zinatoka nchi za magharibi na hizo ndizo zinatumika kufanya analysis ingawa sina uhakika kama tuna uwezo wa kuzitumia.
Majuzi wenzetu wamepeleka chomba sayari ya Mars,Maili 300 katika speed ya 12,000KM/hr kwa miezi 7
Chombo hicho kimetua chenyewe bila msaada kutoka ardhini.
Huko NASA kuna wataalam wa kila aina.Sasa hivi wanafanya study ya kila sayansi ili kubaini kuna nini huko.
Hawa ndio tunaobishana nao!! teh teh teh! OMG