Covid-19: Madagascar yajisajili kwenye mpango wa chanjo za bure, COVAX

Covid-19: Madagascar yajisajili kwenye mpango wa chanjo za bure, COVAX

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Mabibi na mabwana pana habari za kutia moyo sana tokea kwa wale magwiji wa tiba ambako mh. Kabudi aliwahi kufuata dawa ya kutibu Corona kwa niaba yetu.

Hatimaye Madagascar rasmi wamejisajili leo kwenye ule mpango maarufu wa chanjo za bure COVAX:

IMG_20210401_164930_552.jpg

Kwa mtaji huu hawa tayari si wenzetu.

Hawa watakuwa wameangalia wakagundua kuwa "jamani tutaangamia." Kwamba si siri wajameni, "tutakwisha!"

Ya nini bwana, chanjo ya beberu si hii hapa?

Rasmi Madagascar wamo ndani ya nyumba.

Mh. Rais, makamu wa rais na serikali yote kwa ujumula muda wa kutumia busara ni sasa:

"Mwongozo mpya kuhusiana na gonjwa hili, ni dharura sana kwa wapenda maisha wote."

Chonde chonde ndugu zangu inahitaji jitihada zetu kutokurejea uhuru stadium, japo katika siku hizi za karibuni.

Waachwe wanaotaka kuchanjwa wachanjwe. Maisha ni ya mtu mmoja mmoja tusilamishane kuchanjwa au kutochanjwa.

Ninawasilisha.

Katika hali isiyokuwa ya Kawaida na iliyowashangaza wengi hasa kutokana na Kujimwambafai Kwao na Mikogo mingi Serikali ya Madagascar imekubali kupata Chanjo kutoka WHO baada ya ile yao Kutoonyesha Mafanikio yoyote huku Raia wake wakiendelea Kufa tu.

Chanzo: BBC News ( Swahili )
 
Lord have mercy!

Zile juice alizokwenda kuchukua na kunywa fudenge ku promote sijui mitishamba, yule waziri wa jalalani anajisikiaje akiona hii??😂
Waafrika tuungane!! Tusikubali chanjo za mabeberu!

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida na iliyowashangaza wengi hasa kutokana na Kujimwambafai Kwao na Mikogo mingi Serikali ya Madagascar imekubali kupata Chanjo kutoka WHO baada ya ile yao Kutoonyesha Mafanikio yoyote huku Raia wake wakiendelea Kufa tu.

Chanzo: BBC News ( Swahili )
Propaganda za kuuza chanjo hizi, hatununui, ndio tushasema
 
Katika hali isiyokuwa ya Kawaida na iliyowashangaza wengi hasa kutokana na Kujimwambafai Kwao na Mikogo mingi Serikali ya Madagascar imekubali kupata Chanjo kutoka WHO baada ya ile yao Kutoonyesha Mafanikio yoyote huku Raia wake wakiendelea Kufa tu.

Chanzo: BBC News ( Swahili )

Habari hii ni mbaya sana kwa mijamaa ya mtaa fulani.

Hongera zake mama Mulamula mwendo wa yeye na barakoa alio nao, huo ni msiba mkubwa kwa hiyo mijamaa!

Hiiiiii bagosha.
 
Back
Top Bottom