COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

Hili wala siyo jambo kubwa kivile; ni suala la Wamarekani kujihami... labda tungewauliza data zao labda wao wana namna nyingine ya kujua idadi ya wagonjwa nchini nje ya taratibu za serikali...
 
Hili wala siyo jambo kubwa kivile; ni suala la Wamarekani kujihami... labda tungewauliza data zao labda wao wana namna nyingine ya kujua idadi ya wagonjwa nchini nje ya taratibu za serikali...
Bora tuendelee kukaa kimya. Maana wakiamua kuweka hizo njia tutashindwa hata kuchutama.

Umemuelewa Paschal kwa huyo mwanahabari aliyekufa na kuzikwa.?

Sie kama Jamhuri tumekubaliana kuwa hakuna corona wala hatuhitaji kumthibitishia mtu.
 
Kwa sababu hupimi, huwezi kujua kiwango cha maambukizi. Kwa sababu unasema wanaosikia dalili wajifukize majumbani kwao, huwezi kujua hata idadi ya wanaojifukiza. Halafu unasema maambukizi yamepungua, unatumia kigezo gani? Ramli za wapiga bao?

Taarifa zetu haziaminiki kwa kiwango chochote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo hata mimi nashangaaga sana upewe idadi ya waliokufa ujawe hofu au? ukawafufue
 
Dunia nzima mambukizi ya covid yanaongezeka, Tanzania tu ndio nchi pekee duniani imefanikiwa kutokomeza covid 19? ??? CCM komeni kutumia gonjwa hili kisiasa na kuhadaa wananchi, brewing a disaster.
 
Wafanyakazi wamenyimwa nyongeza na promotions nyingi na ambazo ni haki zao kiutumishi. Hawawezi kuficha taarifa kwa maslahi ya kisiasa. Kazi ipo kwa upendeleo hakuna anayeweza kuwa mwaminifu bila maslahi
 
Dunia nzima mambukizi ya covid yanaongezeka, Tanzania tu ndio nchi pekee duniani imefanikiwa kutokomeza covid 19? ??? CCM komeni kutumia gonjwa hili kisiasa na kuhadaa wananchi, brewing a disaster.
Tukisema tupime watu kama wanavyofanya wengine ni kweli tutaona maambukizi yanaongezeka ila sijui kufanya hivyo kutatoa mchango gani kutofautisha na hali iliyokuwepo sasa?
 
Tukisema tupime watu kama wanavyofanya wengine ni kweli tutaona maambukizi yanaongezeka ila sijui kufanya hivyo kutatoa mchango gani kutofautisha na hali iliyokuwepo sasa?
Tatizo wananchi wamaacha kuchukua tahadhari aina yeyote baada uongozi wa nchi kuwahadaa ugonjwa umetokomezwa.
 
Tatizo wananchi wamaacha kuchukua tahadhari aina yeyote baada uongozi wa nchi kuwahadaa ugonjwa umetokomezwa.
Unataka kuniambia kwamba wananchi wanaona ndugu zao wanaumwa corona na hadi kufa ila wao wanasikiliza serikali inavyowahadaa kuwa corona imetokomezwa?
 
Hivi Kuna watu mna akili za ajabu Sana, Vita ya uchumi ndio nini?
Mikopo ya kujenga reli,umeme mnawategemea wao (IMF,WB)
Kulisha dawa waginjwa HIV)AIDS,chanjo za watoto,umeme b jijini,barabara,afya,kujenga madarasa n.k fedha zinatoka kwao kwa mikopo au ufadhili!

Makusanyo na mapato ya ndani yanatosheleza mishahara na gharama nyingine za uendeshaji serikali.
Waache watoe tahadhali kwa raia wao, sisi tunaficha udhaifu na takwimu. Na Vita ya uchumi isiwe kichaka Cha kuficha udhaifu wa serikali
 
Wazungu hawajawahi kuongopa mjomba
Mkuu Erythrocyte, Mhe. Tundu Lisu aliposema "tumepata Rais wa ajabu sana" nilimuona Tundu Lisu hana adabu na anamkosea adabu Rais wetu. Lakini majuzi aliposimama kuwahutubia watz kuwa Covid19 imeisha tz na Bunge likapitisha azimio la kumpongeza kuimaliza Corona hapa Tanzania, wakati huo huo nikiona marafiki wakifa kwa changamoto za kupumua nilishangaa sana. Ni wiki ya tatu sasa napona taratibu kutoka katika mateso makali ya maumivu na changamoto za kupumua. Lakini haikuwa Covid19, kwani kwa mjibu mamlaka Corona virus haipo Tz.
 
Swala la corona kusema kwamba halipo, ni kujidanganya, lakini kusema pia lipo na linatisha Tanzania Napo pia ni kujidanganya!

Corona ipo Ila haina mamlaka yake katika Taifa la wacha Mungu Tanzania, wenye kuamini tu ndio wanaendelea kujichanganya kila mahali, hawana hofu, wenye hofu inawala vichwa vibaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…