COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

COVID-19: Nani mkweli kati ya Serikali yetu na Ubalozi wa Marekani? Je, Tanzania tunawaogopa sana Wamarekani? Kwanini waseme uongo huu waachwe?

Ubalozi wana haki kutoa taarifa kwa raia wao pia Wana haki ya kupata taarifa za sahihi kulingana na ukweli na vigezo au miongozo ya kimataifa...

Kumbuka taarifa na takwimu za mwazo zilivyokuwa.. kusimamisha upimaji wa Corona. Mbinu zinazotumika. Na Hali ya Sasa .... Kifupi tutegemee Sala na Nyungu.

Wagonjwa wapya wanatagazwa wakivuka Boda, hospitali wagonjwa wa Corona wanapugua...
 
Kidiplomasia ubalozi wa marekani hawakutakiwa kutoa taarifa kama hii badala yake wizara yao ya mambo ya nje ndio wangetoa taarifa kwani inaonekana katika nchi yetu huru kuna mamlaka mbili zinashindana
Ila kiuhalisia Corona ipo na watu wengi wanakufa mbaya zaidi kutokana na kauli za wanasiasa watu wengi wameacha kuchukua tahadhali kwenye mabasi watu wanajazana na pia hawavai barakoa na hata ile namba ya kutoa tahadhali au taarifa juu ya Corona ukipiga inaita hadi inakatika cha muhimu tuelewe Corona ipo kila mtu achukue tahadhali
 
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala fikirishi, elimishi na hamasishi uzalendo za "Kwa Maslahi ya Taifa" ambazo hutolewa kwa mfumo wa maswali, makala ya leo ni kuhusu utoaji wa taarifa za Corona, COVID-19: Nani Mkweli Kati ya Serikali Yetu na Ubalozi wa Marekani?!. Jee Tanzania Tunawaogopa Sana Wamarekani?!. Kwanini Wamarekani Waseme Uongo Mkubwa kama Huu halafu Waachwe tuu hivi hivi?!.

Nimesoma with disbelief hii taarifa ya leo ya ubalozi wa Marekani, kwanini ubalozi unatoa taarifa ya uongo kuhusu hali ya COVID-19 nchini kwetu na wanaachwa hivi hivi?!, Jee hawa Wamarekani tunawaogopa?.

Taarifa yenyewe inapatikana hapa kwa wale wa kimombo
Tanzania International Travel Information

Kama rais Magufuli juzi kasema Corona imepungua, jana Waziri Ummy kathibitisha kwa data, leo Marekani inaibuka na kesema hizo taarifa zinazotolewa na viongozi wetu ni taarifa za uongo, na kutusingizia serikali yetu inaficha data, nani mkweli na nani muongo?.

Kwanini Wamarekani waseme uongo waachwe?!. Kama serikali yetu itawanyamazia hawa Wamarekani bila kuwaonya au kuwachukulia hatua yoyote kwa uongo wao, then waelewa wataelewa nani ni muongo kweli na nani ni mkweli, na pia huu utakuwa ni uthibitisho kuwa Mmarekani tunamuogopa, hata utusingizie uongo gani sisi, tunanyamaza tuu!.

Tanzania na rais wetu Magufuli na serikali yetu tumekuwa tukisingiziwa uongo mwingi na sometimes hata kutukanwa na kudhalilishwa na media za nje, lakini tunanyamaza ama kwa kuwapuuza, ama kwasababu Tanzania kwa sasa hatuna watu wenye the capacity kujibu tuhuma kama za The Economist, lakini enzi za Kikwete, aliposingiziwa na balozi wa Marekani kuwa amehongwa suti, Ikulu yetu haikunyamaza, baada ya kupiga kelele humu, Marekani walikanusha.

Lakini sasa leo rais wetu anasema ukweli, kesho Waziri wetu wa Afya anasema kweli, halafu kesho yake, ubalozi uliopo hapa hapa Tanzania unaibuka na taarifa za uongo kuonyesha serikali yetu inaficha ukweli!, ukificha ukweli maana yake unachoripiti ni uongo!. Sasa huu uongo unaosemwa nchini, na ubalozi fulani, usipokanushwa, itaamaanisha ama tunawaogopa Wamarekani, ama tunachoelezwa na serikali yetu ni .. na wanayoyasema Wamarekani ndio ukweli wenyewe, ilaikitokea hawa Wamarekani ni waongo, swali linabaki "Hivi hawa Wamarekani wanatutakia nini?!. Kwanini watutungie uongo na kuueneza dunia nzima?. What is their motive behind and what do they wish to achieve?.

Paskali
Pasco ukiona wanatusakama wanajua hatuwaogopi
 
Serkali inasema corona corona ipo tuchukue hatua hatua ni jambo la mtu kama ilivyo ukimwi
Kila mtu anajua Corona ipo sana Tz, watu wanaugua kimya kimya na kuzikana kimya kimya pia. Serikali ilichokifanya ni kusitisha kutoa taarifa rasmi (ili kuhalalisha harakati za kimaisha ziendelee) lakini wakati huo huo taarifa za reja reja zikiendelea kuzagaa mitaani.

Hivyo ubalozi wa USA yuko sahihi kwa 100%, na hakuna ajabu yoyote kwa USA kutoa taarifa zenye lengo la kulinda raia wake waliopo hapa Tanzania. Ndio kazi iliyemleta Tanzania, na analipwa kwa kodi za wamerekani. Hatuwezi kumpangia cha kusema wala kufanya juu ya raia wa nchi yake.

Na sisi balozi wetu wa Tz aliyepo kule USA anapaswa kutoa taarifa za kulinda raia wa Tz waliopo huko USA au wanaotaka kwenda USA (ikiwezekana wasiende kabisa!) maana huko Corona ipo na kuna ghasia za maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi. Bahati mbaya balozi wetu huko USA yuko usingizini tu. Hajui anachotakiwa kufanya, sijui anasubiri kuambiwa na kina Bashiru au Pole Pole kitu cha kufanya
 
Umeandika vitu out of context.
Issue hapa ni Corona, wewe unazungumzia vita ya Kiuchumi utadhani Corona ni suala la nchi moja moja au Marekani inapambana kiuchumi na Tz.
Jenga hoja kama Tz tunasingiziwa kuhusu Corona ama la. Hivyo blah blah za maisha ya wamarekani tuwaache wamarekani na marekani yao.

Hata hivyo huwezi kunishawishi kwa lolote kuwa maisha ya kiujumla ya wamarekani yako duni kiasi cha sisi kujilinganisha na wao.

Tuseme ukweli tu, 90% ya sisi watanzania tunatamani tungezaliwa marekani au kuishi marekani maisha yetu yote. Wenzetu wako mbele mnoo kwa kila kitu tukijilinganisha na sisi. Sisi bado tunaishi kukamilisha utaratibu tu (kupumua, kula, Kulala) lakini wenzetu wanaishi kuenjoy maisha.

Wewe unawamini wamarekani kwa taariafa wanazo zitoa?
Lini umefanya tafiti kubaini ukweli wa kinachosemwa na ubalozi wa marekani
Usitake kubisha vitu ambavyo havina ukweli mkuu. Corona isiwe sababu ya watu washindwe kuendelea na maisha mengin
Siasa inagusa vitu vingi, kama utakuwa unajitambua basi utakuwa umeelewa
 
Taarifa zao ziko na ukakasi, mtu mzima huwezi danganwa kirahisi na maelelo ya Ummy, wanajificha kwenye shamba la mchicha bila kujua migongo yao iko nje!

Waje na data, tuone hali ilivyokuwa mwanzo na sasa kwa nini kudanganyana umma! Kwa maslahi ya nani?
Leta idadi kamili isiyo na ukakasi
 
Kidiplomasia ubalozi wa marekani hawakutakiwa kutoa taarifa kama hii badala yake wizara yao ya mambo ya nje ndio wangetoa taarifa kwani inaonekana katika nchi yetu huru kuna mamlaka mbili zinashindana
Ila kiuhalisia Corona ipo na watu wengi wanakufa mbaya zaidi kutokana na kauli za wanasiasa watu wengi wameacha kuchukua tahadhali kwenye mabasi watu wanajazana na pia hawavai barakoa na hata ile namba ya kutoa tahadhali au taarifa juu ya Corona ukipiga inaita hadi inakatika cha muhimu tuelewe Corona ipo kila mtu achukue tahadhali
Wazungu wanajua jpm ndio kiboko yao wanamwogopa
 
Ubalozi wana haki kutoa taarifa kwa raia wao pia Wana haki ya kupata taarifa za sahihi kulingana na ukweli na vigezo au miongozo ya kimataifa...

Kumbuka taarifa na takwimu za mwazo zilivyokuwa.. kusimamisha upimaji wa Corona. Mbinu zinazotumika. Na Hali ya Sasa .... Kifupi tutegemee Sala na Nyungu.

Wagonjwa wapya wanatagazwa wakivuka Boda, hospitali wagonjwa wa Corona wanapugua...
Wamarekani wanaisha kwa corona wenyewe wako bize na kuuwa wafrika
 
Haya pasi- kali hiyo tutamwambia jiwe kwa muundo Wa setikali yetu kuna waziri Wa
(1) mambo ya ndani - wizara yake inafanya kazi nzuri tu ya kubonya watu na hakuna mtanzania anaelalamika
(2) wizara ya mambo ya nje - inafanya kazi nzuri ya kuwasiliana na masangoma Wa nje ya nchi
Na tuna kitengo kimoja cha
(1) msemaji wa serikali - anajitahidi sana kuitetea serikali kwa wananchi
Sasa tutamwambia jiwe aanzishe kitengo cha
(1) msemaji Wa serikali mambo ya nje - na wewe uwe msemaji mkuu hiyo idara
Na ili msigombane na kina johnmbatizaji huyu tuanzishe kitengo cha msemaji Wa mambo ya chato ili msigombanie cheo hicho kimoja na ili kufuta uvumi kuwa chato hakuna ikulu
MAMBO NI MENGI NA MUDA NI MCHACHE - OKO- TOBA. IS AROUND THE ROUND A BOUT
Jpm ameikimbiza corona hadi imeisha ,nyie mnalialia humu
 
Back
Top Bottom