Kafrican
JF-Expert Member
- Jan 26, 2015
- 7,251
- 7,037
Kwa mwezi mzima, USA ilikua na kesi 15 tu, walidhani wako salama na wameishinda corona!
Siku 22 za kwanza, Italy walikua na kesi tatu tu!!, walidhani wako salama!!!!
Siku 21 za kwanza, Egypt walikua na kesi 3 tu, walidhani hali iko sawa!!!
siku 26 za kwanza, Spain walikua na kesi 7 tu, walidhani hali iko shwari!!!
siku 34 za kwanza, France walikua na kesi 14 tu, walidhani madaktari wako ngangari kuzulia virusi!
Italy, USA, France, Germany, South korea zimekua zikipambana na corona kwa siku zaidi ya 52, Nchi za Africa kando na Egypt na SA, zimekua zikipambana na corona hata siku ishirini hazijapita alafu tunajifanya eti huku kwetu hali si mbaya kama ulaya, kumbe hao jamaa siku ishirini za kwanza hali yao ilikua shwari tu kama vile huku tunadhania.
Alafu, Ukiangalia nchi za USA, Italy, France... kuna mahali flani kwa jedwali utaona kesi zao za siku zilikua zinaongezeka mara mbili ya siku iliopita... Hii ni baada ya wao kuacha kufanyia testing kwa wale walio na dalili (symptoms) za corona pekee na badala yake kufanya mass testing ya watu wote walio safiri hata kama ni kutoka eneo moja la nchi kwenda eneo lengine.....
Kwa mfano, USA sahii ndo inaongoza kwa kesi za crona ikiwa ni kesi 188,000 zilizopatikana positive, lakini ukiangalia USA ilianza kufanya mass testing wiki iliopita, kabla hapo walikua hata hawajui hali kamili
hii tovuti inaonyesha nchi zinazoongoza kwa total tests zilizofanya na nchi by 20th march, wakati huu, USA ilikua haijaripoti kesi nyingi kwasababu walikua wameanya tests 103,000 pekee
How many tests for COVID-19 are being performed around the world?
Sahii USA ndo inaongoza kwa kufanya tests kuliko nchi, hakuna nchi inaikaribia kwa test manake wanasema wamefanya 1 million tests, hii ndio maana kesi za USA zimekua zikiongezeka kila uchao hadi kupita kesi za china, Italy, France..etc.....
--------------------
The White House promised an ever-increasing number of coronavirus tests would be available by the end of the month, saying the number of available test kits could be as high as 27 million. But tracking analysts say only about 1 million total tests have been administered nationwide.
The White House promised 27 million coronavirus tests by end of March, but U.S. just hit 1 million
-------------------------
Kenya najua tumefanya tests kama 800 na contact tracing and quaranteen imeika watu 2,000.... Serekali ilitangaza akwamba wataanza kufanya mass testing sijui ni wiki hii au lini, lakini wakianza kufanya, usishtuke ukiona kesi zinaongezeka kwa ma mia kila siku....
current stats as of today, sorted by total cases
sorted by total deaths
-------------------------------------------------------
Kwahivyo tuwe makini, fwateni maaagizo ya serekali manake hao wengine walikua na kesi chache kwa wiki kadhaa hapo mwanzoni na wakafikiri wako salama, Kumbuka huku Africa tukijaza mahospitali kwasababu ya corona magonjwa mengine ambayo yanaua watu wengi yatawanchwa kutibiwa, watu walio na malaria, ukimwi, watakua hawajisumbui kwenda hospitali manake wanaogopa corona kwahivyo watabaki majumbani waugue kimya kimya... kwahivyo hata kama si watu wengi watauliwa na corona, kuna wengi zaidi watakufa sababu corona ilipewa kipaumbele kwa hospitali zote.
Take care, be safe!