Suala hili niliwahi kuliandikia post mahali, lakini nimeonelea kulianzishia uzi ili kulifafanua kwa undani zaidi.
Katika kuhalalisha hoja ya JPM kulisha maparachichi na maboga test kits za COVID-19, Wafuasi wa JPM wamekuwa mara kwa mara wakitumia hoja kwamba hizi mashine sehemu nyingi duniani pia zilionekana kuwa na hitilafu!
Na kwavile hata kwa wenzetu zilionekana hizo hitilafu ndipo wana-conclude JPM yupo sahihi.
Kwa wanaoona taabu kusoma ngoja niwape muhtasairi kwa kusema kwamba, mashine zilizoonekana kuwa na hitilafu sehemu mbalimbali duniani sio hizi alizozikosoa JPM. Zilizoonekana kuwa na hitilafu ni Rapid Diagnostic Testing Kits kwa ajili ya antibody testing wakati alizozilisha maboga JPM ni Laboratory Testing Kits.
Kama huoni taabu kusoma, endelea na maelezo hapa chini.
Ni kweli nchi nyingi including the Ulaya zilirudisha au zililalamika kuhusu mapungufu ya hizo kits, na nchi hizo ni pamoja na UK, Uholanzi, Uturuki, India na zingine.
Tuanze na UK
Sawa na nchi zingine zilivyokuwa zimefanya mizaha, kama ambavyo JPM anaendeleza hiyo mizaha hadi kesho, kuja kushituka UK wakagundua coronavirus ameshasambaa nchini UK.
Out of desperation, UK wakaona kutgemea laboratory test peke yake itachelewesha sana kupata idadi ya maambukizi, na hapo ndipo wakaamua kuagiza Rapid Diagnostic Test Kits. Lengo la UK, ilikuwa ni kusambaza hizi kits kwa wingi ili wananchi waweze kujifanyia testing wao wenyewe kama ambavyo wanawake wanavyojifanyia pregnancy test wao wenyewe.
New York Times, April 16 waliripoti:-
Kabla hatujaendelea, unaona hapo wamesema kwamba ni
home test kits...
Kisha The New York Times wanaendelea:-Lakini kwavile wenzetu huwa hawang'ati maneno, The New York Times hawakuishia hapo na badala yake wakaongoza kilichosemwa na watalaamu kwamba:-Hadi hapo utaona wazi kwamba hakuna haja ya mtu kuwa mtalaamu wa maabara kufahamu kwamba kits zilizoonekana kuwa na faults UK ni tofauti na hizi zilizolishwa oil na Magu.
Fuatilia source yoyote ya kueleweka kuhusu hizo UK kits, utakachoona na hicho hicho kilichoandikwa na The New York Times... Rapid Diagnostic Test Kits.
Na hapa tusisahau hizi Rapid Diagnostic Test Kits zinazalishwa in mass tofauti na zile lab kits ndo maana UK peke yake walinunua zaidi ya kits 2M.
Na hilo lilitokea wakati huko nyuma hapakuwa na hizi Rapid Diagnostic Test Kits for COVID-19 kwahiyo nyingi zilikuwa hata hazijawa approved huku mataifa tajiri wakitaka kuwa na stock ya kutosha kabla demand duniani haijawa kubwa zaidi; na Wachina wakatumia fursa kwa wanasiasa waliokuwa desperate.
Tuje kwa Spain!
EFE News Agency ambayo ni international news agency kutoka Spain wanaandika:-
Hapo kwenye RED kwa mara nyingine utaona wanazungumzia rapid test kits.
EFE wanaendelea:-Hpao tena wanazungumzia suala la rapid test kits, na kwa idadi kubwa namna hiyo unaweza kupata picha zIngetumika tumika vp kwa sababu pamoja na utajiri wao, I doubt kama watakuwa na labs nyingi namna hiyo; na badala yake, kuna uwezekano na wenyewe walitaka kuzifanya ziwe available everywhere kama ilivyo vipimo vya ujauzito.
Sina haja ya kuizungumzia desperation ya Spain manake kwa muda mrefu sana nimewazungumzia huku nikitoa mfano wa Dr. Fernando Simon, Dokta Mkuu wa Matibabu ya Dharula ambae wakati Italy inawaka moto, yeye kwa kujiamini kabisa akasema sio rahisi Spain kukumbwa na hilo na janga.
Again, pitia source yoyote ya kueleweka utaona nako wanazungumzia test kits ambazo Spain walikuwa wanalia lia kupigwa, ni Rapid Diagnostic Test Kits, aka Rapid Test Kits aka Antibody Test kits.
What about India?
Kibwagizo cha BBC kinasema"-Again, ni rapid testing kits.
Kisha BBC wanatutoa matongotongo kwamba:-BBC yenye Waandishi wa Habari wana authority gani ya kusema hizo kits haziwezi ku-test coronavirus zenyewe kama zenyewe?
Shirika la Afya Duniani (WHO) wakitoa Scientific Briefing mwezi mmoja uliopita walianza na kibwagizo kwamba:-Ukifanya majumuisho hapo kwenye RED na Bold Black utaona kumbe kuna laboratory based mlecular testing na rapid and easy to use devices aka rapid testing kits!
Sasa tafakari na jiulize zile kits zilizolishwa mafenesi na tukaambiwa hazitoi majibu sahihi ni laboratory-based-mlecular testing kits au rapid and easy to use devices?
Kwa kutambua pressure iliyopo, WHO wakawapongeza hao manufacturers wa hizo rapid testing kits lakini wakaendelea:-Hiyo bold imewekwa na WHO wenyewe wakisema wazi kwamba hizo kits zisitumike kama ndio final say!
Here come another question! Kits zinazotumika Tanzania na hatimae kupewa sample za mbuzi na hivyo Wafuasi wa Magu kudai findings za Magu zipo right kwa sababu hata kwa wenzetu tatizo lilionekana. Je, ni kits ambazo hazijawa validated for clinical trials?
WHO wakatoa maelezo jinsi ya hizi rapid testing kits zinazovyofanya kazi na kutoa scientific estimation kwamba:-Kumbe Sensitivity rate yake ni 34% to 80%.
Ukifanya homework mwenyewe utaona Spain walilalamika kwamba sensitivity ya hizo kits ni only 30% wakati wao walitarajia ingekuwa at least 80%!
Kisha WHO wakasisitiza:-Again, mnataka kutuambia WHO wameiacha Tanzania iwe inatumia kwenye maabara zake Rapid Diagnostic Testing Kits pamoja na kwamba walishatoa tahadhali huko nyuma kwamba hizi sio za kuzitumainia?!
Katika ulimwengu wa kibepari hata WHO wanaweza kununuliwa na China ili kutoa hayo maelezo hapo juu ili kuwanusuru China na aibu.
What about other sources?
Mwaka 2013, almost 7 years before COVID-19 tovuti ya
Science Direct inaelezea Rapid Diagnostic Testing kwamba:-Again, ina maana testing kits zilizo kwenye mahabara zetu na kukosolewa na JPM ni kama zile ambazo long time zimeshaelezewa zisitumike kufanya final conclusion au ni laboratory testing kits?
Kuna uhusiano gani kati ya kits zilizorudishwa nchi zingine kiasi cha kutumika kama justification ya kwamba JPM yupo sahihi kwa sababu hata kwa wenzetu hizo kits zimeonekana zina hitilafu?!
JPM ni Mwana Kemia. Je, ametuambia
findings zake zimeonesha sensitivity ya zile kits ni asilimia ngapi?
Hitimisho ni kwamba, mnaweza kuendelea kuwalisha ujinga watu kwamba hata Ulaya hizi kits zilionekana zina hitilafu lakini ukweli ni kwamba kits ambazo zilionekana zina hitilafu sio hjzi ambazo ni clinically validated, and approved.
Of course errors lazima ziwepo manake hakuna mashine iliyo 100% efficient. Hata hizi laboratory kits zinakuwa na acceptable margin of errors; kwa mfano, ziwe na Sensitivity ya 95%.
NOTE:
Sina muda wa kufanya proofreading, so pardon any errors!